The Law of the Child Act, 2009

Magpie

Member
Aug 26, 2009
70
7
WanaajamiiForums, kuna sheria hii mpya ambayo imekuaa signed na Mh. JK Nov, 2009 ina mambo mengi
mazuri kwa maslai ya mtoto wa kitanzania, hasa kumlinda kwa mambo hatarishi kama yalivyo oanishwa kwenye S. 17 of the Act (child protection), inakataza mtoto kuingia kwenye kumbi za disko, bar na night club pia ina kataza mtoto kuuziwa sigara, pombe au dawa za kulevya.

Na nilichokipenda zaidi ni hiki kuhusu kuwatumia watoto katika shughuli za harusi mpaka usiku, sheria hii imeweka wazi katika S. 158 (c) kuwa ni makosa kuwatumia watoto katika shughuli za fashion show ua harusi zinazo fanyika usiku.

masikitiko yangu ni kwamba japokua sheria hii imekuja kujaribu kutetea maslai ya watoto, lakini ya pata miezi sita sasa toka isainiwe na Mh rais hakuna wizara au wadau husika katika maswala ya haki za watoto waliojitokeza na kuipigia debe ila watanzania kwa ujumla wao wajue kwamba sheria hii ipo na inakusudia kulinda vitu gani, maana hadi hii leo inasikitisha kuona watoto wakitumiwa hadi usiku kwenye shughuli za harusi.

sipigii debe sana ishu ya watoto kwenye kumbi za starehe maana hili lina matatizo yake katika utekelezaji wake maana Tz hatuna ID ambazo zinaweza kumtambulisha mtoto au mtu mzima, maana sheria inataamka wazi kuwa mtoto ni yule aliekua chini ya miaka 18.
 
Ni sheria nzuri sana, na malengo ya serikali ni mazuri pia, tatizo ninaloliona ni usimamizi wa sheria hii na ukweli kwamba katika familia nyingi kutokana na umasikini watoto wanatumika kama chanzo cha mapato pia mmomonyoko wa maadili ndio hasa unaowafanya baadhi ya watoto kukesha kwenye sehemu za statehe aidha wakistarehe au wakitumika kama chombo cha starehe.
 
Nakubaliana na wewe 100% dawa nadhani ilikuwa ni kuondoa tatizo na sio kuondoa matokeo ya tatizo.N ahili ndo tatizo kubwa sana la sheria zetu hapa tanzania.
 
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto bado amekula usingizi, anafikiri Sheria itajitekeleza yenyewe? Ipo haja ya kuwa na Taasisi (eg TAMWA) au vikundi vya kutetea haki za watoto kama ilivyo kwa Wanawake!
 
Buchanan kama un soft yake tuwekee hapa tafadhali.Mwanzoni tulipata bill tu.
 
Ila kwa mtazamo wangu japo kwa ufupi,ulinzi wa mtoto kwa kiasi kikubwa ni wa jamii nzima.Sisi kama jamii ndio wenye kujua madhara ambayo yanawapata watoto kwa kiasi kikubwa.Na pengine tunachangia katika madhara hayo kama vile kuwatumikisha katika ajira mbaya,kutowalea vizuri,tamaa zenye kusababisha mimba zisizotarajiwa nk.Kwa maoni yangu kilichopo ni sisi tulio na uelewa kuyakemea na pengine kuyaweka wazi.Kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeisaidia serikali.
 
Kama kuna mwenye kopi ya sheria hii aturushie mtandaoni tafadhali

Tangu JF ifanyiwe marekebisho nimeshindwa kabisa ku-attach file/document. Naomba mnisaidie namna ya ku-attach ili niwapatie soft copy ya Sheria hiyo.
 
Back
Top Bottom