ZirlovimovicZirkov
Senior Member
- Sep 3, 2025
- 168
- 311
Wakuu salaam
Nimekuja kwenu tuweze kujadili hili swala.
Kwa miaka mingi Dunia imekua ikiendeshwa na Sheria ya supply and demand (Yaani uwingi wa kitu na uhitaji wa kitu). Leo nakuja kwenu tujadili Je! hii Sheria inaweza kufa? Nimepata msukumo wa kuuliza hili swali baada ya kuona mambo yafuatayo -:
1. Kuundwa kwa sarafu ya kwanza ya kidigital
Yes! Mwaka 2008 ndio iliundwa sarafu ya kwanza ya kidigital na mtu aliyeitwa SATOSHI NAKAMOTO na akaamua kuiita BITCOIN.
Bitcoin ndio sarafu ya kwanza ya kidigital ikiwa na token milioni 21 tuu Dunia nzima huku duniani kukiwa na watu zaidi ya bilioni 5 kwa wakati huo.
Tukitumia Sheria ya supply and demand tunaona kwamba mtengenezaji wa BITCOIN alitumia vizuri Sheria ya supply and demand kwa kutengeneza token chache kabisa ili atengeneze demand.
Kwasasa muelekeo wa Dunia nzima ni matumizi ya mifumo ya kidigital hasa mifumo ya Blockchain, Tunaona sasa Marekani anapambana kuipitisha Sheria ya fedha za kidigital "CLARITY ACT" pia tunaona mpango wa Kila nchi kuwepo na CBDC ( CENTRAL BANK DIGITAL COIN) pia tunaona mambo ya tokenization of shares. Hii yote ni maandalizi ya kwenda katika mfumo wa malipo ya kidigital hasa hasa matumizi ya crypto currency katika shughuli za Kila siku.
Sasa swali langu linakuja hapa kwamba kutokana na kukubalika kwa sarafu ya kidigital na Dunia kujiandaa na matumizi yake, Je! Kwanini sarafu zingine zisingekuja na mbinu kama ya BITCOIN yaani kutumia Sheria ile ile ya supply and demand kwa kuanzisha sarafu lakini wakaweka tokeni chache kuzidi BITCOIN ili kutengeneza demand kubwa zaidi?
Binafsi nimeona sarafu nyingi zilizoanzishwa baada ya BITCOIN zimekua na token nyingi kuzidi hata Bitcoin. Je! hawa hawakuwaza kutumia Sheria ya supply and demand?
Tukitumia kigezo cha ukubwa wa demand Yaani watu tunaona kwamba Bitcoin imevunjwa vunjwa kwenye vipande vidogo "unit called SATOSHI" ambavyo vinaitwa SATOSHI. Sasa hata hawa waanzilishi wa sarafu mpya nafikiri ilifaa watumie Sheria ya supply and demand kwa kutengeneza sarafu yenye token chache lakini wao wanafanya tofauti yaani wametengeneza sarafu lakini zinatokeni nyingi kuzidi sarafu ya kwanza. Sasa je! kutokana na hili la sarafu mpya kuwa na tokeni nyingi wanataka kuua Sheria ya uwingi na uhitaji?
2. Kukua kwa teknilojia na matumizi ya akili bandia AI
Baada ya 2008 tulianza kuona mabadiliko makubwa sana ya kidigital, hasa ujio wa social media, matumizi ya smartphones na pia matumizi ya websites yaliongezeka sana.
Kutokana na vichocheo hapo juu tumeona mabadiliko makubwa na maendeleo ya haraka sana. Kutokana na kukua kwa teknolojia na matumizi ya mitandao tumeona sasa watu sasahivi wanafuata mizigo wenyewe China, bei zimekua hazina tofauti tena kati ya muuzaji wa kariakoo na muuzaji wa kule kijijini aliyekua anafuata mzigo kariakoo. Kutokana na ukuaji wa teknolojia kumekua hakuna tena usiri katika bei za bidhaa kitu ambacho teknolojia ikikua zaidi itakua hakuna utofauti wa bei.
Je! hili nalo haliwezi kuchochea kufa kwa Sheria ya supply and demand?
3. Ujio wa 3D printing
Hii ni teknolojia ambayo ipo lakini bado haijawa kwa wingi sana. Lakini kutokana na kukua kwa teknolojia nafikiri hii nayo inaweza kuwa kitu Cha kawaida na watu wengi wakaweza kuimiliki hasa huku Dunia ya tatu.
Ujio wa 3D printing teknoloji haitaweza kuua kabisa Sheria ya supply and demand? Maana watu wote tutakua censored na mahitaji yetu yatakua yanajulikana Sasa je? Huoni kama Kila mtu atakua hana uhitaji wa kukitafuta kitu kama Sheria ya uwingi na uhitaji inavyosema???
Mwisho niweke mawazo yangu.
Binafsi naamini Sheria ya supply and demand ni tayari imeshapitwa na wakati na hapa tulipo ni tunamalizia kufukia kaburi lake. Sheria ya SUPPLY AND DEMAND is already replaced with FIRST TO COME FIRST TO BE SERVED.
Ndio binafsi naamini Sheria ya supply and demand ilishakufa na imekua replaced na Sheria ya wakwanza Kuna ndio wakwanza kuhudumuwa/kuteka soko. Naweka na mifano ya hii Sheria mpya niliyoiona
1. Ujio wa Android na IOS
Wote tunajua Mfalme wa simu alikua ni NOKIA. Nokia yupo wapi Leo? Nokia alishindwa kuelewa kitu kidogo tuu kwamba Dunia ilikua bado inamuhitaji ila haikua inamuhitaji kama Nokia yule wa mfumo wake wa SYMBIAN, kilichomshinda Nokia ni kujua uwezo uliopo katika Android na smartphones. Nokia akachelewa kusoma mchezo na hata alipokuja kugundua hilo bado akaja na mbinu ya kizembe eti kutumia WINDOWS kwenye simu, hapo ndio alipotea mazima.
Huawei simsikii tena baada ya kuwekewa vikwazo na Marekani asitumie mifumo ya Android kwenye simu zake, hivi ni nani ananunua flagship za HUAWEI? namuona VIVO akitamba kuliko HUAWEI. Mchawi alikua ni Android tuu.
2. TESLA
Magari ya umeme ni mengi lakini ukimiliki Tesla unaonekana unahadhi ya pekee. Unajua kwanini? Elon Musk alitangulia kuliona hilo mapema wengine wote watafuata nyuma yake.
3. Bitcoin
Hakuna coin itakuja kuishusha Bitcoin kwasababu Bitcoin alishatangulia na wengine wote itabidi tuu wafuate nyayo zake.
Mifano ni mingi naamini hata wewe mchangiaji mwenzangu unayo, haya tutiririke hapa huku tukijenga hoja juu ya maada tajwa.
Karibuni wakuu