The green river serial killer

Ezio Ezio

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
423
649
220px-Gary_Ridgway_Mugshot_11302001.jpg

Gary Leon Ridgway
Mimi nitaeleza kidogo kwa namna ninavojua juu ya huyu serial killer.
Gary alizaliwa 18 February 1949, eneo moja linaitwa SALT LAKE CITY, UTAH. Wazazi wake ni Thomas na Mary Ridgway na alikua mtoto wa 2 kati ya watoto 3. Maisha yake yalikua na changamoto toka akiwa mtoto na mara kadhaa inasemekana alishuhudia mama yake anavompelekesha baba yake, ambae alikua anafanya kazi ya udereva
Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo, naweza sema hivyo sababu Gary alianza kuonesha roho ya ukatili toka akiwa na miaka 16 tu baada ya kumshawishi mtoto wa kiume na kumpeleka kwenye pori/miti kisha akamshambulia kwa kumchoma kisu kwenye mbavu na kujeruhi hadi ini la yule mtoto, bahati nzuri yule mtoto alipona.

Gary alimaliza shule ( high school) mwaka 1969 na alimuoa Claudia Craig, mpenzi wake wa shule.

Pia alijiunga na U.S NAVY, na alienda mpaka Vietnam katika kutumikia jeshi, kule alikua akijihusisha sana na ngono zembe kitu kilichopelekea kupata ugonjwa wa gonorrhea, alikasirika sana kwa kuona kama wale makahaba ndio wenye kosa ila bado hakuacha kufanya nao ngono zembe.

Ndani ya mwaka ndoa yake na Claudia ilivunjika na akaona mke mwingine ambae mara kadhaa alilalamika kuwa Gary alikua mbabe na amewahi kumkaba koo mara kadhaa, japo alioa tena ila hakuacha kununua makahaba na mara kadhaa alimlazimisha mkewe wafanye mapenzi hadharani au maeneo ambayo baadae ilipatikana baadhi ya miili ya wahanga wake. Kuna kipindi mkewe uyu 2 alidai Gary alikua akisoma Biblia na alikua analia akiwa anasoma.

Jamaa huyu inasemekana alikua anapenda sana sex na alikua anadai hata mara kadhaa kwa siku, pia alikua na tabia ya kuchukia sana makahaba lakini pia alikua haezi kuacha kuwatumia, nadharia ziko kua hii ilatokana na mafundisho ya dini kumhukumu kwa anachofanya lakini pia kibinaadamu kushindwa kujizuia tamaa zake.

Katika kipindi cha mwaka 1980-1990 inasemekana alikua keshaua wanawake zaidi ya 71 hii ni kutokana na maelezo yake kwenye mahojiano na sheriff Dave Reichert mwaka 2001 na mauaji hayo aliyafanyia Seattle na Tacoma huko Washington.
Baadae ilionekana jamaa kaua watu wengi zaidi ila tu kasahau idadi, na wengi kaua 1982-1984 na wengi wa wahanga walikua makahaba au wale waliotoroka familia zao na hawana kwa kwenda.

Njia kuu ya kuua alipenda kutumia kumkaba mtu hadi kufa(strangled) kisha kutupa miili yao kwenye eneo lililokua na miti miti karibu na green River ( na ndio the green river serial killer ilitokana na eneo hilo ambalo mingi ya miili ya wahanga wake ilipatikana)
Inasemekana alikua akifanya nao mapenzi/ kuwabaka kabla ya kuua na mara kadhaa alikua anarudi eneo hilo na kufanya tena mapenzi na wale marehemu / ile miili ya aliowaua kisha anatupa bablishi(gums) au vipisi vya sigara na hata vikaratasi ambavyo viliandikwa na watu wengine / kutumiwa na watu wengine. Muda mwingine alienda kutupa miili ya wahanga wake miji mingine ili tu kuchanganya polisi wasimjue/kumpata kirahisi.

Kutokana na kuzidiwa na ujanja polisi waliwahi kwenda kuomba ushauri juu ya saikolojia ya serial killers na namna ya kumdaka toka kwa serial killer mwingine maaraufu ambae alikua anangoja siku yake ya kuuwawa kwa kupigwa shoti ya umeme, serial killer huyu si mwingine bali ni Theodore au Tedy Bundy kama alivojulikana na wengi.
Gary Ridgway aliwahi kamatwa 1982 kwa tuhuma za kujihusisha na makahaba, mwaka mmoja baadae yaani 1983 akawa mmoja wa watuhumiwa wa green River serial killer.
Mwaka 1984 akiwa bado mtuhumiwa alichukua polygraph test na akapass. Polygraph test ni kifaa kinachopima shinikizo la damu, mapigo ya moyo, ngozi kwa maana unyevu, mfumo wa upumuaji na vyote hivyo vinapimwa wakati unaulizwa maswali so ukiongopa mashine itajua na jamaa akapass yani.

Baada ya FBI kufanyia marekebisho mfumo wa hizo mashine baada ya miaka kadhaa inaonekana kiuhalisia jamaa alifeli ila ndio kwa tekinolojia ya kipindi kile jamaa alionekana kafaulu.
April 7 1987 polisi walichukua nywele na mate vya Gary kwa ajili ya vipimo na bado wakashindwa kabisa kumlink kama muuaji.

Mwaka 1985 Gary alianza mahusiano na Judith Mawson na mwaka 1988 akamuoa rasmi, Judith amesema kwenye interview mara kadhaa kuwa muda wote alioishi na Gary hakuwahi kuhisi kama ni muuaji. Pia Gary alisema kipindi alichukua na Judith alipunguza sana kuua kitu ambacho Judith anajivunia kwa kusema kuwa kitendo chake cha kua mke bora kwa Gary kimeokoa maisha ya wengi kwa kumfanya bwana Gary kupunguza kasi yake ya uuaji.

Tarehe 30 November 2001 katika eneo la Kenworth truck factory ambako jamaa alikua akifanya kazi kama mpaka rangi za kupulizia ( spray printer) Gary Leon Ridgway alikamatwa rasmi kwa tuhuma za mauaji ya green River baada ya zile sample za nywele na mate zilizochukuliwa mwaka 1987 kuwa chanya kuwa jamaa ndie haswaa anaweza kuwa muuaji.

Baada ya kusumbua polisi kwa zaidi ya miaka 20 bwana Gary sasa 40 ilikua imefika, mapema mwaka 2003 Seattle tv ilitoa taarifa kuwa Gary kahamishiwa kwenye chumba chenye ulinzi mkali ( maximum security) katika jela ya king country jail, na wakati huo mawakili wa Gary walikua wakifanya mpango ili Gary akubali mashtaka na kutoa ufafanuzi wa namna alivoua na alikoficha miili mingine ili asihukumiwe hukumu ya kifo.
Tarehe 5 November 2003 Gary alikiri kuhusika na mauaji ya wanawake 48 pamoja na kuonesha alificha wapi miili mingine hivyo kujinusuru na hukumu ya kifo.

December 18 2003 Gary alihukumiwa vifungo vya maisha mara 48 bila msamaha wala rufaa, pia alihukumiwa miaka 10 jela kwa Kupoteza ushahidi makusudi, hivyo 10 x 48 = 480, ikawa katika vifungo vyake vya maisha mara 48 pia aliongezwa miaka 480 ya kupoteza ushahidi iwapo kwa muujiza atavimaliza hivyo vifungo 48 vya maisha ( hahaha kidding) .

Kuelezea alivyowadanganya wahanga wake alisema alikua akiwaondoa kabisa wasiwasi kuwa hawahitaji kingono, hivyo waliamini na kwenda nae kwa kujidai awapa tu msaada na alipenda wale waliotoroka familia zao na makahaba sababu ilikua rahisi kuwaingia.
Naomba niishie hapa kwa leo.... amani iwe nanyi.
 
Back
Top Bottom