Anayejua historia ya hawa jamaa Ku klux clan

incredible terminator

JF-Expert Member
Aug 1, 2016
2,229
3,525
Nimekua mfuatiliaji mzuri wa makala kadhaa za umafia, utemi na ugaidi, Kuhusu binadam waliochafukwa na roho, Japo kwa kiasi nilikuja kugundua kuwa hakuna binadam anaezaliwa akiwa mafia, Wengi wa mamafia na watu hatari ni Jamii ziliwatengeneza kutokana naEffect mbalimbali za kimalezi namakuzi, na Changamoto za kimahusiano ambavyo vililetelezea kusababisha Athari za Kisaikolojia na baadhi ya binadam kugeuka wanyama na kuwa hatari zaidi ya uhatari wowote,

Mara nyingi Killers au kwa lugha rahisi Wauaji ni watu ambao wanatekeleza matendo hayo kwa kufurahia, Kuna Muuwaji mmoja Katika Historia niliwahi kusoma maisha yake aliitwa ROBERT SCORT, Raia wa Collombia Unaambiwa Jamaa alikuwa anafurahia kuuwa kuliko chakula, yaani siku ambayo aliifurahia maishan mwake ni siku ambayo alipata kuuwa wanawake wengi, Mwamba aliuwa hadi alipokuja kukamatwa na FBI lakini alikuwa ashatekeleza mauaji zaidi ya wanawake 1000,

Pia juzi juzi tumepata kisa cha Dada mmoja kigori wa tik tok nchini Kenya alivyokutana na The killer huko dating site na kisa jamaa baada ya mizagamuano kamaliza kampiga dem visu nakumuua hapo inasemekana jamaa huwa anatekeleza mauaji muda mwingine endapo victim wake ameshindwa kumlipa kiwango cha pesa anachokuwa anakitaka.

Kuna hili kundi la Ku kulux clan huwa nawaona pia wanatajwa kama kikundi kilichokuwa cha watemi wauwaji na mafia ambao walijikita katika Itikadi za kiimani kama kuna mdau yeyote mwenye Documentary ya hawa mafia atusimulie kidogo kuhusu hawa jamaa.
 
Ku kulux Clan ni kikundi cha Kigaidi cha Kikristo kule Marekani kwa Binen. Walikuwa wanauwa wote ambayo siyo Wazungu. wanaamini binadamui halizi ni Mzungu na hivyo hawakutaka jamii zingine kuishi Marekani zaidi ya wazungu. Walikuwa wanaua Waafrika, Waarabu na Wayahudi na jamii zingine ambazo siyo Wazungu.

Gogole "The Ku Klux Klan, commonly shortened to the KKK or the Klan, is the name of several historical and current American white supremacist, far-right terrorist organizations and hate groups."
 
Kuna kitabu ninacho ila ni hard copy kinaitwa Modern World history 2nd edition cha . Ben walsh kinaelezea hawa kuku klax , mbali na kuwa genge la mafia. Pia lilikuwa linatumika kisiasa na marekani ku deal na wale wote mashuhuri kwenye jamii ambao walikuwa na elements za ukomunist ndani ya ardhi ya marekani wakati huo. Hili kundi lilipata umaarufu baada ya gavana mmoja anayeitwa george McCarthy alipounda tume iliyojulikana kama UN-american activity ambayo ilikuwa na kazi ya kuwabaini wale wote ikiwemo wanasiasa waliokuwa na political affiliation na ukomunisti . Sasa hawa ku klux walikuwa kama kikosi kazi cha ku deal na hao watu ikiwemo blacks . Na ku klux walikuwa na back up support ya CIA. Hiyo ni dokezo fupi tu kuhusiana na hao jamaa.
 
Overseas, yeah, we tryna stop terrorism
But we still got terrorists here livin'
In the USA, the big CIA
The Bloods and the Crips and the KKK...
Verse ya Will.I.am hiyo kwenye where is the love

Hao KKK ndio Ku Klux Klan...walikuwa wauaji wa watu wasio wazungu Marekani pia wanasiasa wa kikomunisti! Na hao The Bloods and the Crips walikuwa kama KKK
 
Lilikuwa ni genge ila lilitumika kisiasa zaidi, yaan serikali ilitoa sapoti japo hadharani ilijifanya kulikemea.
Walikuwa wanapambana na
1; ukomunist
2;watu weusi
3; ukatoliki ( hasa watu kutoka Ireland)
 
Kuna movie inaitwa BlacKkKlansman, imewagusia hao jamaa kiundani kidogo. Kuna Black American polisi na myahudi polisi waliingia kwenye hicho kikundi kufanya upelelezi, based on true story.
 
Overseas, yeah, we tryna stop terrorism
But we still got terrorists here livin'
In the USA, the big CIA
The Bloods and the Crips and the KKK...
Verse ya Will.I.am hiyo kwenye where is the love

Hao KKK ndio Ku Klux Klan...walikuwa wauaji wa watu wasio wazungu Marekani pia wanasiasa wa kikomunisti! Na hao The Bloods and the Crips walikuwa kama KKK
People killin' people dyin' children hurt can hear them crying,can you practice what you preach,and send some guidance from above,father father father help us.... Ilikiwaga' ringtone yangu hiyo.
 
Back
Top Bottom