The Elders: Tanzania tunao? Ukimya wao maana yake ni nini?

residentura

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
7,021
9,609
"The Elders" ni kundi lenye viongozi wastaafu mashuhuri ambalo liliasisiwa na Mzalendo wa kweli wa Afrika,Tata Madiba mnamo mwaka 2007 kwa lengo la kushauri kuhusu migogoro,haki za binadamu,amani na changamoto zingine zinazohusiana na ustawi wa binadamu.

Hawa viongozi wamekuwa mstari wa mbele kuhoji,kushauri na kupendekeza jinsi ya kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili hii dunia.

Napenda kufahamu kama huko Tanzania kuna kundi kama hili au kama halipo,ni kwanini halipo na ni wakina nani wanastahili kuwepo.

Nakumbuka miaka ya 1980s mara baada ya Baba wa Taifa Mwalimu JK Nyerere kustaafu uongozi,alikuwa na kawaida ya kupongeza,kufokea,kuhoji na kushauri hadharani kuhusu mambo yalihusuyo Taifa letu. Nakumbuka alikuwa anatumia lugha kali sana wakati mwingine kukiwa na jambo ambalo anaona haliendi vile inavyostahili.

Swali la msingi najiuliza ni, je,kizazi cha Mwalimu JK Nyerere hakipo,hakijawahi kuhoji/kushauri mambo yalipokwenda kombo kwenye awamu zilizopita? Kama kipo na kiliwahi kuhoji,kwa nini awamu hii wapo kimya?

Kuna filamu moja inayomuhusu binti ambaye alidakwa na wanaume 6 alipokuwa anatembea kurudi kwake usiku,na kisha alibakwa wanaume watano huku mmoja akiwa amekaa pembeni tu akishuhidia bila yeye kushiriki. Baada ya muda fulani wa uchunguzi wa yule binti juu ya watesi wake,aliwafahamu wote na kuanza kumtafuta mmoja baada ya mwingine ili alipe kisasi.

Alipofika kwa yule mwanaume ambaye hakumbaka,alimkumbusha juu ya lile tukio,jamaa akajitetea kuwa yeye hakumbaka,hivyo amuache. Yule dada akamwambia kuwa katika wote wale wanaume sita,yeye ndiye mbaya zaidi ya wote,kwani alikuwa na uwezo hata wa kuwaambia wenzake wasifanye vile,ila hakufanya hivyo.

Akamwambia kama alikuwa anajua kitendo kile ni cha kinyama,kwa nini hakujaribu kuzuia? Binti hakumuua mara moja,bali alihakikisha anateseka sana kwanza kabla ya umauti kumfika.

Hapo tunajifunza kuwa hata kukalia kimya uovu unaoona unafanywa,ni zaidi ya huyo mtenda huo uovu.
Kila mmoja asimame eneo lake na atimize wajibu wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom