Ndugu wana JF
Napenda kuleta thread hii kwenu ili tuweze kuichambuwa na kujua nafasi ya Raisi wa Tanzania katika sakata la Dowans
kwani tangu imetolewa hukumu ya tanzania kutakiwa kuilipa kampuni tata ya dowans mamilioni ya shilingi hatuja msikia Raisi ama hata waandishi wake kulizungumzia swala hili zaidi ya wanaharakati na baadhi ya wasomi kukemea na kutokukubaliana na ulipaji wa pesa hizo
imefikia wakati baadhi ya wanaharakati wamemtaka Rais Jakaya Kikwete kuvunja ukimya na kuzungumzia suala hili.
Na inasemekana Nchi inayumbishwa na kikundi cha watu wachache, waroho wa madaraka, wabinafsi, wasiojali maslahi ya taifa na ambao wanajiita ni Watanzania (Gazeti mwananchi).
Swali linaloniumiza hapa ni kuwa UKIMYA WA RAISI WA TANZANIA JUU YA SAKATA LA DOWANS UNAMAANISHA NINI? Je amekubaliana na hicho kikundi cha watu wachache wanao yumbisha nchi? ama amekubaliana na ulipaji wa mabilioni ya pesa kwa Dowans, ama anatafakari jinsi ya kupambana na hili sakata?
karibuni Great thinkers
MSEMA UKWELIIIIIII HAPENDWIIII DAIMAAAAAAA
Mapinduziiii daimaaaaaaa:A S 27: