Ndugu yangu Solomon David na wana JF, Kikwete hayuko kimya - anajitahidi kujibu kila tuhuma inayoelekezwa kwake tena anajibu kwa style ile ile moja anayoijua. Kwa tuhuma nyepesi nyepesi anavyo vyombo vingi tu vya kumjibia kama Makamba na CCM, magazeti ya Uhuru, Habari Leo na Daily News, TBC, Habari Corporation na kadhalika. Kwa tuhuma nzito kidogo wako akina Rweyemamu, Ngeleja, Werema, Zitto, Celina na wote wale ambao wako tayari kuwakana hata mama zao wazazi kulinda mkate wao. Kwa tuhuma nzito sana na wananchi wanaposogea karibu na ukweli ndipo hapo Jakaya Mrisho Kikwete anapovua joho lake na kuvaa sura yake halisi.
Kwa kuwatumia FFU, mtutu wa bunduki, mabomu ya machozi na maji ya upupu kuwanyamazisha hao wananchi, Jakaya Mrisho Kikwete anajaribu kuufukia ukweli kuwa Richmond na Kikwete ni kitu kile kile ! Adui wa Tanzania si Rostamu wala Lowassa, hawa ni wapambe tu - adui wetu namba moja ni Jakaya Mrisho Kikwete, Raisi wa Jamhuri ya Muungano, Kiongozi wa Serikali, Mwajiri Mkuu, Mwenyekiti wa chama tawala, Jemadari Mkuu wa majeshi yetu na Mlinzi Mkuu wa Katiba yetu na Usalama wetu ! Bahati mbaya hivi sasa amegeuka na kuwa Msaliti Mkuu wa wananchi.