Kiongozi kila aina ya engine ina code yake.
Mfano,
Engine za vvti ndio zinakuwa na code ya 1G na cc zake zinakuwa mara nyingi hazizidi 2000
Angalia verrosa.
Engine za d4 zinakuwa na code ya JZ1 au 2,
Zenye 1Jz huwa na cc 2400
Zenye 2jz huwa na cc 2900
Angalia brevis na verrosa.
Engine nyengine zina code ya ya 3s,1az.
Ishu inakuja kwa mafundi wetu wa Kibongo ukimwambia akupe hizo tofauti inakuwa shida na ukitaka ushauri kutoka kwake atakwambia nunua 1G iwe kavu. Utaijuaje kavu, angalia bamba la nyuma utaona taa zake hazijaungana na buti. Basi inakuwa tafrani tu.
also mtaalam wa umeme,funguo original ya brevis ilivunjika, nikabadilisha na ku transfer ile mashine ya key to my new key, programed it and ikawa inawasha gari, but remote haifungi mpaka nifunge na kufungua kitasa manually, others wananiambia ni imobilizer problem, wengine wanasema mashine ile iliyowekwa sio yenyewe kwenye ufunguo, na inaboa kweli kila wakat kufungua kwa kuchomeka ufunguo kwenye kitasa, kuna utaalam wwote naweza kufanya au ndio ishakula kwangu, maana nlipeleka jamaa wa ku diagnose kwa mashine akachemka, alifanikiwa ku unprogram tu, akifika a certain point inagoma kufika asilimia 100...any help or advice will be ,much appreciated.
naomba nijue ulaji wa mafuta kati ya d4 na vvti, mafundi wengi wanasema d4 inakula sana mafuta naomba ufafanuzi
also mtaalam wa umeme,funguo original ya brevis ilivunjika, nikabadilisha na ku transfer ile mashine ya key to my new key, programed it and ikawa inawasha gari, but remote haifungi mpaka nifunge na kufungua kitasa manually, others wananiambia ni imobilizer problem, wengine wanasema mashine ile iliyowekwa sio yenyewe kwenye ufunguo, na inaboa kweli kila wakat kufungua kwa kuchomeka ufunguo kwenye kitasa, kuna utaalam wwote naweza kufanya au ndio ishakula kwangu, maana nlipeleka jamaa wa ku diagnose kwa mashine akachemka, alifanikiwa ku unprogram tu, akifika a certain point inagoma kufika asilimia 100...any help or advice will be ,much appreciated.
mkuu sio kweli inaonekana wewe na hao mafundi bado hamjaelewa nini maana ya d4 na vvti.
ukishajua maana yake basi huwezi uliza swali hilo kamwe.
pumbavu Sana mafundi uchwara
Ni kweli kabisa unayosema mkuu, mafundi wengi wa kibongo hawapo updated na teknolojia mpya. Mimi natumia Toyota Opa yenye engine ya D4 mwaka wa tatu sasa haijaniletea matatizo yeyote. Tatizo kubwa tu nililowahi kulipata ni kuwa gari ilikuwa inakataa kukaa sailensi kama kwenye foleni hivi ilikuwa ikizima, muda wote ilikuwa inataka lazima niwe ninakanyaga accelerator hivyo nikiwa kwenye foleni ilikuwa ikinilazimu niweke neutral ili niwe ninakanyaga accelerator.
Nikahangaika sana kwa mafundi wa mtaa wa lindi, mikocheni, maomeni na kwingineko, walikuwa wakibahatisha mara waninunulishe plug, nosel, fuel pump na vitu vingine bila mafanikio. Lakini baada ya kusearch kwenye mitandao yenye forums mbalimbali za magari nikaja kukuta kumbe watu wengi walipata tatizo kama hilo kwa engine ya aina hiyo na solution kumbe ni kubadilisha air cleaner. Fasta nikaenda pale msimbazi kituo cha bahresa nikanunua air cleaner... baada ya kuifunga mpaka leo tatizo lile likawa limetokomea.
Sasahivi gari yangu inakaribia km 100,000 za milage, nilishakuwa na corolla yenye engine ya 5A ambayo imeandikwa wazi kabisa kuwa ibadilishwe timing belt kila baada ya km 100,000. Sasa kwenye Opa yangu yenye D4 sijaona hayo maandishi wala sehemu yenye hiyo timing belt, sasa nauliza je hilo ya kubadilisha timing belt pia linaaply kwenye engine ya D4? pia naomba hapo kwa mafundi wako wanaofanya mainternance hizi kisomi hasa isiwe wale wa DT DOBIE na Toyota Tanzania ambao bei zao wanaoweza kuzimudu ni ma STK, SU na DFP
Kwa nchi yetu hii ya ujanja ujanja huwezi tegemea kituo kimoja tu cha mafuta katika uhai wa gari yako yeneye D4 engine. Uchakachuaji ni mwingi mno. ili kupunguza pressure kwa kukabiliana na hali hiyo ukijumlisha hatuna mafundi professional, nunua gari yenye kuweza kumudu hali mafuta yaliyochakachuliwa na mafundi wa miembeni. Achana na D4 utajilaumu. Nunua VVTi au 3S 4A 5A nk.
Nini Tofauti ya mafuta haya Uleaded, super na petrol