Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,808
- 24,449
Malima hakuwa na sifa yoyote ya uongozi ingawa alikuwa mwanafunzi mzuri aanapokuwa na mwalimu mzuri. Alipokuwa akiongozwa na Nyerere alikuwa mwanafunzi mzuri sana, lakini alipoanza kuongozwa na Mwinyi, akawa hajifunzi lolote tena na hapo ndipo alipoanza kuharibikiwa. Alipelekwa Wizara ya Elimu enzi hizo hizo za Mwinyi halafu akajidai kuwa eti ameleta sera ya kutumia namba kwenye mitihani kusudi waislamu wasionewe, jambo ambalo lilikuwa limeachwa nchini na watayarishaji wa mitihani wa Cambridge. Anajua kuwa mtihani wake wa darasa la nane alitumia namba na vile vile mitihani wake wa darasa la kumi na mbili na darasa la kumi na nne alitumia namba, lakini akaja kuzingua watu kwamba "aligundua kuwa" majina ya kiisalamu yalikuwa yakibaguliwa. Hapo alianza kuonyesha kuwa mtu ambaye ni politically bankrupt! Mzee Dr Omar Ali Juma, alikuwa ni kiongozi mwenye busara sana kwa waislamu kuhusu elimu kuliko wanasaiasa uchwara akina Malima waliokuwa wakijitafutia sifa za ulani bila kuwa na product ya kuonyesha.
Alipokuwa akitoa misamaha ya kodi kiholela kwa wafanya biashara wa kiislamu kwa akishirikiana na Ramadhan Nyamka hadi wafadhili wakasitisha kutoa misaada yao je alikuwa haoni madhara yakufanya hivyo kwenye uchumi wa nchi? Baada ya Wizara yake kuchukuliwa na Kikwete ndipo misaada ikaaza kurudi tena lakini wafadhili wakalazimisha kuwe na utaratibu imara wa kukusanya kodi kuanzia wakati huo, jambo lililopelekea kuundwa kwa TRA muda mchache kabla Mwinyi hajamaliza muda wake.
Vilaza wasiojua historia ya mambo sawasawa hupenda sana kuungaunga maneno yanayowafurahisha, na ndiyo maana wengine waliwahi kudiriki kusema kuwa Mkapa ndiye aliyesimamia kodi wakati hiyo ilikuwa ni plani iliyoanza tangu wakati wa Mwinyi kutokana na Malima kutibua mambo wakati akiwa waziri wa fedha.
Fall ya Malima ilitokana na Kikwete kutoa siri za mabaya yake na huenda sasa hivi Kikwete anamtunza Malima junior kumfariji kutokana na fall hiyo ya baba yake.