The Commedy production ndani ya Bunge

BadoNipo

Senior Member
Jul 4, 2008
170
28
Kundi la Ze Comedy lililojipatia umaarufu nchini kwa maigizo yao, jana lilikuwa miongoni mwa wageni waliofika kujionea vikao vya Bunge vinavyoendeshwa mjini hapa. Wasanii hao walitambulishwa kwa wabunge baada ya kipindi cha maswali na majibu asubuhi.

Naibu Spika Anne Makinda, wakati akiwatambulisha wageni hao aliosema ni maalumu, alisema wamefika hapo kwa mwaliko wa wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam. Wabunge walipiga makofi wakati wa utambulisho huo ambao awali Naibu Spika hakutaja majina yao, hadi mbunge mmoja alipotaja kuwa ni Ze Comedy, ndipo akawataja kwa majina.

Wasanii waliotinga ndani ya Bunge hilo ni pamoja na kiongozi wao, Emmanuel Mgaya ‘Masanja’, Lucas Mhuville ‘Joti’, Sekioni David ‘Seki’, Mujuni Sylivery 'Mpoki', Isaya Mwakila ‘Wakuvanga’. Wakati wakitambulishwa wakiwa ndani ya suti za Kimagharibi, baadhi yao walivaa miwani ambayo imekuwa ikiwatambulisha wakati wanapofanya maigizo yao kwenye televisheni.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Wakuvanga alisema wamekuja bungeni kwa nia ya kujifunza jinsi chombo hicho cha kutunga sheria kinachofanya kazi zake. Alisema walichojifunza ni kwamba baadhi ya viti vya wabunge vinakosa wabunge; wabunge wanafikiria kwa kufumba macho na wakati mwingine hutaniana.

Wabunge walifurahi sana, pia walijumuika nao katika chakula cha mchana.

Source: Habari leo
 
wanatafuta kuoenewa huruma ili waruhusiwe kuonesha vionjo vyao TBC
 
wanatafuta kuoenewa huruma ili waruhusiwe kuonesha vionjo vyao TBC

Hamna cha huruma tayari walikwisha karibishwa TBC na serikali ilijua ni implications gani zitajitokeza once wapo huko kwa hiyo hamna huruma cha zaidi ni huyo anayewakwaza kuanza kazi zao huko TBC ashughulikiwe mapema then watu wapige mzigo maana hapa its Mengi vs. Serikali mimi sitashangaa siku moja huyo kiherehere wa juu JK akiongea kuhusu hili maana huyu Mengi alishazua jambo kipindi fulani na Masilingi mpaka Mkapa akaongea.
 
Kila mtanzania anaruhusiwa kwenda bungeni kuangalia shughuli za bunge jinsi zinavyoendeshwa.

naamini muda si mrefu tutaanza kupata tena vitu vyao.
 
Zecomedy ni wasanii kama wasanii wengine tu. Kwa maana hiyo wana uhuru wa kwenda bungeni.
 
In fact kwenda kwao Bungeni ni kutmebea laini mwenye masikio alishasikia kwamba kuna watu wanawabania vijana hao na kutaka kuwaaribia maisha yao.Lakini atafanikiwa huyo mchaga aliyeshindwa hata kukaa na mke
 
Shida hapa jf watu wanaingiza hoja za ki ze komedy maana hoja ni kwamba amekwenda bungeni kwa mwaliko wa wabunge wa Dar na inawezekana ni kwa familiarization tu ya mambo ya bunge, sasa watu wameanza kuingiza uongo wao kwamba wamekwenda kulalamikia tatizo lao na EATV na ajabu wanaolalamika badala ya kuitaja EATV wanamtaja Mengi.
Jamani muacheni Mengi. Maana yeye hana shida na hao Ze comedy bali wao ndio wana shida maana hawataki kufuata sheria. Wanataka kufanya mambo ki comedy. Basi shida zao asibebeshwe Mengi.
 
Back
Top Bottom