The Bold: Shukrani Wakuu

The Bold: Shukrani Wakuu

Hatimaye mwaka unaisha, wengi wametoa shukrani zao kwa namna mbali mbali.. Nadhani utakuwa ni uungwana nami nikisema asante kwa mambo kadha kwa members humu, for the big love and support..

Nawakubali sana members wote humu, ila hawa wafuatao wamenigusa kwa namna ya pekee sana mwaka huu..

- Heaven on Earth

Kiujumla: ni moja ya member ambao wamekaa katika viwango vyao vya ubora kwa muda mrefu sana (kama cr7, lol).. Na mwaka huu michango yake kwenye nyuzi mbali mbali imebakia kwenye ubora zaidi

Binafsi: nahisi inawezekana hata yeye mwenyewe ameshasahau.. Miaka 2 iliyopita niliwahi kupost uzi contraversial sana humu! Baadae kuna "wahusika" wakaanza kuniandama, nikaja kushare na members humu kuwa kuna watu wananifuatilia duuuuuuhh kama kawaida watu wakapuuzia na kukejeli daaaahh nikaumia sana.!
Lakini huyu sista ni moja ya watu alinitia moyo sana.. Mara kwa mara alinijulia hali na kwa kweli ilinitia moyo..

Ipo siku huko mbeleni nitashea nanyi kilichokuwa kinaendelea huko nyuma ya pazia katika yangu na hao mabwana kwa takribani mwaka mzima niliopotea hapa..
Imepita miaka miwili, sikuwahi kukushukuru, nichukue fursa hii kukwambia asante sana HOE.. Unaweza kuhisi ulifanya kitu kidogo but ulinitia moyo sana..

- The Boss

Kiujumla: huyu ni moja ya watu wenye busara zaidi humu JF, mwaka huu bado amedhihirisha ubora wake kwamba 'he is truly the boss'.. Mtu makini sana

Binafsi: ni moja ya watu wakwanza kabisa kunitia moyo humu kunishauri namna ya kutumia talanta yangu kufanya kitu kitakachokuwa na return kubwa kiuchumi..
Nimeufanyia kazi ushauri wake huu na matunda yamenza kuonekana na pia zaidi Mungu akipenda mwanzoni kabisa mwakani 'we goinn' make headlines'..

- 'Tag list' ya The Bold

Kwenye nyuzi zangu zote hawa memba huwa nawamention kwenye post # 2. (Pia nimewamention hapo chini post # 2) Hawa member kwakweli wametisha sana mwaka huu.. Ni wao ndio wananifanya licha ya pilika pilika za maisha, lakini najitahidi nipate muda niandike makala na kuziweka humu! Wananiispire sana, and nawaheshimu sana bcz they got my back.. Salute kwenu wakuu!!

- Kiranga

Kiujumla: huyu ni specie adimu sana kukutana nayo duniani.. Ni great thinker haswaaaa! Hata kama hukubaliani na hoja zake lakini lazima utasema moyoni huyu mtu yuko njema kichwani.. Mwaka huu pia ametisha zaidi

Binafsi: kiranga pia ni moja ya watu wa mwanzoni kabisa kunitia moyo na kunishauri namna ya kuhakikisha napata pia faida ya kiuchumi kwa talanta hii.
Pia mwaka huu alinipa ushauri adhimu namna ya kulinda 'identy' ya makala zangu kwa tekniki maalumu sana na ya kiakili zaidi..

Pia nilipoingia kwenye mgogoro na gazeti ambalo lilichapa makala yangu bila makubaliano, kiranga alitumia muda wake kunishauri namna gani nipambane mpaka nipate haki. Na ushauri wake ukazaa matunda, jamaa wakakubali tumalizane mezani kwa kulipa fidia.

Salute sana mkuu.. Nakuheshimu mno.

- Nifah

Kiujumla: huyu bibie watu wa dizaini yake huku kwetu tandale tunawaita 'kiraka'. Yani kila mahali anafiti.. Ukimkuta jukwaa la siasa unaweza kuhisi mdee ameingia na ID fake, ukimkuta MMU utadhani Diva the bauwse, ukimkuta jukwaa la michezo utadhani Dr. Liki abdallah (binti pekee ninaye mfahamu anapenda mpira kiasi hiki)... kila jukwaa unalomkuta comment zake ziko "on point".

Asingelikuwa team kiba ningemfananisha na Chibu dangote (chibu anaimba, anapiga vyombo, choreographer, director etc) ila kwa kuwa yuko "team malalamiko" wacha tu nimfananishe na Rucky baby..

Binafsi: Mwaka jana huyu binti tuliwahi kusigana katika mijadala humu jukwaani na kwakuwa sote ni binadamu hasira zikatawala na matokeo yake tukawa maadui wakubwa sana kwa kipindi kirefu sana... Mungu mkubwa, siku hizi silali pasipo kumtakia usiku mwema!! Ama kweli life is an interesting journey! you never know where it takes you

The Bold.

Note: New thread on the way
NOTE:- I'M WAITING FOR THE NEW THREAD.....BIG UP BRO...
 
Ongera sana Mkuu within one hour uzi umejaa comments namna hii, Ahsante kwa kushukru japokuwa najua ujaweza ku-tag wote lkn Shukrani zako tumezipokea.
 
Man yaani tangu ulipoanza kuandika makala zako umekuwa maarufu sana humu jf. Bahati mbaya kila uzi unaoweka humu nakutaga nimechelewa kuuona. Kwa sasa kila siku, kila baada ya masaa kadhaa lazima nichungulie kama umeweka uzi.

Napenda aina ya uandishi wako. Yaani hata ungekuwa mjinga wa kiwango cha juu akisoma lazima aelewe.
Keep it up mkuu.
Ukipata nafasi niwekee story ya jamaa mmoja akiitwa Abbuu Nidal.
 
Kiranga ni kichwa kikali sana..kila mtu anajua hili japo wachache wanaweza kulisema hili kwa uwazi..
The bold unajua kufafanua jambo lolote kwa ubora wa Hali ya juu sana..
Najua utapata madili ya kutosha..lakini usitusaau jf..mara moja moja unakuja jf nakutupa visa..maana mtambuzi nae alitutosa jf tukaikosa mikasa yake ya kesi zilizotikisa..barikiwa The bold
 
Back
Top Bottom