The Bold: Shukrani Wakuu

Habibu B. Anga

JF-Expert Member
May 7, 2013
6,557
25,671
Hatimaye mwaka unaisha, wengi wametoa shukrani zao kwa namna mbali mbali.. Nadhani utakuwa ni uungwana nami nikisema asante kwa mambo kadha kwa members humu, for the big love and support..

Nawakubali sana members wote humu, ila hawa wafuatao wamenigusa kwa namna ya pekee sana mwaka huu..

- Heaven on Earth

Kiujumla: ni moja ya member ambao wamekaa katika viwango vyao vya ubora kwa muda mrefu sana (kama cr7, lol).. Na mwaka huu michango yake kwenye nyuzi mbali mbali imebakia kwenye ubora zaidi

Binafsi: nahisi inawezekana hata yeye mwenyewe ameshasahau.. Miaka 2 iliyopita niliwahi kupost uzi contraversial sana humu! Baadae kuna "wahusika" wakaanza kuniandama, nikaja kushare na members humu kuwa kuna watu wananifuatilia duuuuuuhh kama kawaida watu wakapuuzia na kukejeli daaaahh nikaumia sana.!
Lakini huyu sista ni moja ya watu alinitia moyo sana.. Mara kwa mara alinijulia hali na kwa kweli ilinitia moyo..

Ipo siku huko mbeleni nitashea nanyi kilichokuwa kinaendelea huko nyuma ya pazia katika yangu na hao mabwana kwa takribani mwaka mzima niliopotea hapa..
Imepita miaka miwili, sikuwahi kukushukuru, nichukue fursa hii kukwambia asante sana HOE.. Unaweza kuhisi ulifanya kitu kidogo but ulinitia moyo sana..

- The Boss

Kiujumla: huyu ni moja ya watu wenye busara zaidi humu JF, mwaka huu bado amedhihirisha ubora wake kwamba 'he is truly the boss'.. Mtu makini sana

Binafsi: ni moja ya watu wakwanza kabisa kunitia moyo humu kunishauri namna ya kutumia talanta yangu kufanya kitu kitakachokuwa na return kubwa kiuchumi..
Nimeufanyia kazi ushauri wake huu na matunda yamenza kuonekana na pia zaidi Mungu akipenda mwanzoni kabisa mwakani 'we goinn' make headlines'..

- 'Tag list' ya The Bold

Kwenye nyuzi zangu zote hawa memba huwa nawamention kwenye post # 2. (Pia nimewamention hapo chini post # 2) Hawa member kwakweli wametisha sana mwaka huu.. Ni wao ndio wananifanya licha ya pilika pilika za maisha, lakini najitahidi nipate muda niandike makala na kuziweka humu! Wananiispire sana, and nawaheshimu sana bcz they got my back.. Salute kwenu wakuu!!

- Kiranga

Kiujumla: huyu ni specie adimu sana kukutana nayo duniani.. Ni great thinker haswaaaa! Hata kama hukubaliani na hoja zake lakini lazima utasema moyoni huyu mtu yuko njema kichwani.. Mwaka huu pia ametisha zaidi

Binafsi: kiranga pia ni moja ya watu wa mwanzoni kabisa kunitia moyo na kunishauri namna ya kuhakikisha napata pia faida ya kiuchumi kwa talanta hii.
Pia mwaka huu alinipa ushauri adhimu namna ya kulinda 'identy' ya makala zangu kwa tekniki maalumu sana na ya kiakili zaidi..

Pia nilipoingia kwenye mgogoro na gazeti ambalo lilichapa makala yangu bila makubaliano, kiranga alitumia muda wake kunishauri namna gani nipambane mpaka nipate haki. Na ushauri wake ukazaa matunda, jamaa wakakubali tumalizane mezani kwa kulipa fidia.

Salute sana mkuu.. Nakuheshimu mno.

- Nifah

Kiujumla: huyu bibie watu wa dizaini yake huku kwetu tandale tunawaita 'kiraka'. Yani kila mahali anafiti.. Ukimkuta jukwaa la siasa unaweza kuhisi mdee ameingia na ID fake, ukimkuta MMU utadhani Diva the bauwse, ukimkuta jukwaa la michezo utadhani Dr. Liki abdallah (binti pekee ninaye mfahamu anapenda mpira kiasi hiki)... kila jukwaa unalomkuta comment zake ziko "on point".

Asingelikuwa team kiba ningemfananisha na Chibu dangote (chibu anaimba, anapiga vyombo, choreographer, director etc) ila kwa kuwa yuko "team malalamiko" wacha tu nimfananishe na Rucky baby..

Binafsi: Mwaka jana huyu binti tuliwahi kusigana katika mijadala humu jukwaani na kwakuwa sote ni binadamu hasira zikatawala na matokeo yake tukawa maadui wakubwa sana kwa kipindi kirefu sana... Mungu mkubwa, siku hizi silali pasipo kumtakia usiku mwema!! Ama kweli life is an interesting journey! you never know where it takes you

The Bold.

Note: New thread on the way
 
the bold mimi nakukubali sana!pamoja sana vitu vyako huwa adhimu huwezi kuvipata mahali popote nakuombea maisha marefu huko mbeleni maana tunahitaji kama wewe muendelee kuwepo big up sana
 
Mungu wangu! Am speechless.
Sikuwahi kufikiri kama ipo siku nami nitakuwepo katika list yako ya kukumbukwa!
What a honour?
Asante sana The bold.

Ni kweli kabisa, nakiri tulikuwa maadui wakubwa sana.
Kila tulipokutana ktk threads tuliumana kwelikweli, namshukuru Mungu kwa busara alizokujaalia maana siku zote ulijishusha wewe.

Nakupongeza kwa aina ya makala ulizoamua kuja nazo ndizo zilizonifanya niweke silaha chini na kuomba kuimaliza vita.

Kupitia kwako nimejifunza mengi kubwa zaidi ya yote ni kumheshimu kila mtu.
Nilikuchukia kipindi kile,sikuwahi kufikiri kama una akili kubwa kiasi cha kunifanya nianze kuvutiwa nawe.
Hivi sasa nimebadilika sana,namheshimu kila mtu humu JF,nimeamua kwa nia ya dhati kuachana na vita vya maneno na members humu.

Never say never,nobody knows tomorrow...
Leo hii wewe niliyekuchukia ndiye kitu cha kwanza kunijea ktk akili yangu kila niamkapo.
Lazima nikutafute nikutakie asubuhi njema ndipo mambo mengine yaendelee.

Nakutakia kila la kheri katika makala zako za kusisimua,daima nitakuwa nawe bega kwa bega.
You got my full support my love...
#TheBoldIsMine#
 
Back
Top Bottom