The Big Match 2020: Magufuli VS Tundu Lissu

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
35,921
2,000
Ni wazi kulingana na mazoea ya Chama cha Mapinduzi, Rais Magufuli atasimamishwa kugombea 2020 nafasi hiyo tena. Tujaribu kutabiri mpambano huo wa 2020 kama Wapinzani ndani ya UKAWA wakimsinamisha Lissu kama mgombea hali itakuwaje? Ikumbukwe kuwa UKAWA bado hawajampendekeza mtu yeyote kusimama hivyo bado sio dhambi kuwajadili watu tofauti na anayefit tunamshawishi asimame.

Kwa vile wasifu wa JPM tayari unajulikana basi tukiweka wa Lissu italeta raha.
Hii itakuwa vita kati ya HAPA KAZI TUU na HAKI NA UTU KWANZA
 

Kibstec

JF-Expert Member
May 21, 2016
1,205
2,000
Ni wazi kulingana na mazoea ya Chama cha Mapinduzi, Rais Magufuli atasimamishwa kugombea 2020 nafasi hiyo tena.
Tujaribu kutabiri mpambano huo wa 2020 kama Wapinzani ndani ya Ukawa wakinsinamisha Lissu kama mgombea hali itakuwaje? Ikumbukwe kuwa Ukawa bado hawajampendekeza mtu yeyote kusimama hivyo bado sio dhambi kuwajadili watu tofauti na anayefit tunamshawishi asimame.
Kwa vile wasifu wa JPM tayari unajulikana basi tukiweka wa Lissu italeta raha.
Hii itakuwa vita kati ya HAPA KAZI TUU na HAKI NA UTU KWANZA
hahahahh....ikitokea hivyo NI LISSU 2020 hakutakuwa na kitu kinachoitwa CHADEMA au UKAWA KATIKA NCHI HII...maana mwenye CHADEMA na wenye CHADEMA wanajulikana......MGOMBEA UKAWA WA MAISHA ANAJULIKANA NI EDDO na hivi T.B JOSHUA kamwambia agombee tu .....sasa jaribuni kumtibua ETI mlete LISSU kama hatawaelewa......YAANI UKIFIKIRIA UWEPO WA LOWASSA NA SUMAYE NDANI YA CHADEMA hauwezi amini kabsa uwepo wa hiki chama kikiwa IMARA 2020.....ni suala la MUDA tu

Yaani yale yaliyokuwa yakiitesa CCM miaka mingi iliyopita NDIO sasa yanaenda ITESA CHADEMA VILIVYO..........Na kilicho inusuru CCM kupotea ni kwamba INA HAZINA ya WATU WENYE AKILI ZAO.....sasa kwa upande wa CHADEMA HILI HALIPO BADO WACHANGA SANA........mlikosea sana kubadili gia 2015.....Leo hii tungekuwa tunasema MENGINE.......
 

Brigadia

Member
Nov 8, 2016
44
95
Nasikitika tu kwamba Lissu atapoteza kila kitu. Ubunge atapoteza na Uraisi hatapata. Labda iwepo tume huru.
 

zugimlole

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
1,903
2,000
Mtamrudishia Manvi hela zake

Naona unapima upepo mje mbadilishe gia angani

Mzee wa watu kutwa kucha anajiandaa 2020 leo mnataka mmpige chini
 

yello masai

JF-Expert Member
Jan 8, 2016
2,587
2,000
Hakuna wa kuiondoa CCM, hata wakiniweka mimi nigombee. Siri ya kuiondoa ni kuwa na tume huru ya uchaguzi.
 

Uliza_Bei

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
3,183
2,000
Chadema na EL ndiyo kifo chao....walete mgombea mshindani ama waendelee kushiriki uchaguzi
 

zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
11,914
2,000
Mkuu lissu is a oerfect match kwa hali ya kisisasa ya sasa tunahitaji mtu radical kweli kweli type ya alfonce mawazo hivo nikubaliane na wwe lissu apewe ikiwezekana uenyekiti wa chama ili atusaidie kudai katiba mpya upya, tume huru, awe frontline kupinga udikteta na naamini anaweza maana ni mtu asiyeogopa kuthubutu na kwa yeyote atakayekuwa mgombea wa UKAWA hata kama hatokuwa lissu ila lisu anaweza saidi sana hasa kampeni za 2020 na hapo itasaidia kumpata rais wa kwanza wa upinzani kma uchaguzi utakuwa huru na haki.
 

Easyway

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
2,606
2,000
Mgombea wa UKAWA 2020 ni Edward Ngoyai Lowasa hatutaki uchochezi.
Bilioni zake 10 alizompa Mbowe ili awe mgombea wa UKAWA 2015 bado zina thamani mpaka 2020.
 

zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
11,914
2,000
Chadema na EL ndiyo kifo chao....walete mgombea mshindani ama waendelee kushiriki uchaguzi
Sina shida kabisa na lowassa kuwa mgombea 2015 maana alifaa kwa wakati ule ila kwa wakati wa sasa chini ya utawala wa chuma wa magufuli inabidi upinzani uweke mgombea chuma ambaye ccm utamuogopa sana na hta akitishia maandamano tu ccm yenyewe wanahaha kma alivo odinga hapo ndipo sera nyingi za upinznai zitasikilizwa na kufanyiwa kazi ila kwa mwendo huu wa kujaza wanadiplomasia kma mbatia sijui lowassa mbowe na safari haitosaidia kupambana na utawala huu wa magufuli wa kidikteta
 

zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
11,914
2,000
Maana yake chadema wanatuambia 2020, watakuja na sera za

kurudisha posho zote kwa watumishi

Kurudisha wote waliotumbuliwa kwa ufisadi

Kufunga mahakama ya mafisadi

Kwa sera za kilofa namna hii nani atawachagua??
Hivi unasomaga ilani za uchaguzi za vyama vya siasa kabla ya uchaguzi. Hayo yaliandikwa wapi kwenye ilani ya uchaguzi ya chadema 2015?? Tuache ushabiki wa kejeli na tujkite kwenye kujibu kwa hoja juu ya mada iliyopo mezani
 

ntamaholo

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
12,303
2,000
Lissu? Magufuri ndiyo mkweli, anatunyoosha akili zilizolala lala. Lzm aendelee. Lisu kama anataka asiharibu cv yake, ajiandae kwa mwaka 2025, atakuwa amejijenga vya kutosha
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
35,921
2,000
Hakuna wa kuiondoa CCM, hata wakiniweka mimi nigombee. Siri ya kuiondoa ni kuwa na tume huru ya uchaguzi.
Katiba mpya lazima lakini na mgombea wa kupambana na Magufuli mwenye uwezo, nguvu, hoja, ujasiri na asiyeogopa kitu ni lazima pia.
Tujiulize kwa nini ccm wanatujenga mawazo kuwa Lowassa ndio mgombea wakati vikao havijampitisha?
Tusiingie mtego huo, nafasi ya mgombea bado iko wazi
 

ntamaholo

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
12,303
2,000
Mkuu lissu is a oerfect match kwa hali ya kisisasa ya sasa tunahitaji mtu radical kweli kweli type ya alfonce mawazo hivo nikubaliane na wwe lissu apewe ikiwezekana uenyekiti wa chama ili atusaidie kudai katiba mpya upya, tume huru, awe frontline kupinga udikteta na naamini anaweza maana ni mtu asiyeogopa kuthubutu na kwa yeyote atakayekuwa mgombea wa UKAWA hata kama hatokuwa lissu ila lisu anaweza saidi sana hasa kampeni za 2020 na hapo itasaidia kumpata rais wa kwanza wa upinzani kma uchaguzi utakuwa huru na haki.
We jidanganye tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom