The best way to rescue our crown jewels | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

The best way to rescue our crown jewels

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by geek, Nov 11, 2009.

 1. g

  geek Member

  #1
  Nov 11, 2009
  Joined: Feb 12, 2009
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu,

  Njia mojawapo ya kuokoa makampuni yetu nyeti kama TANESCO, BANDARI, TRL, TTCL, ATCL na mengineyo, ni kuya-list kwenye stock markets za Dar Es Salaam, Nairobi na Kampala. X-market listing.

  Badala ya kuwaachia wageni waje kutuvuruga, tuna uwezo wa kuendesha makampuni haya kwa nguvu ya shareholders (wazawa na wageni), badala ya serikali kusimamia - tunajua haina mpango wala nia ya kuyafanya yawanufaishe watanzania, lakini mjadala lazima uanzie mahali. Hata kama kuna wageni wataruhusiwa kununua hisa sawa, ili mradi uamuzi ufanyike kwa voting process.

  Serikali mpya itakayokuja, iwe CCM au CPT, ikizingatia dira hiyo Tanzania itabadilika ghafla.Jiulize tunapoteza muda kiasi gani? Tunapoteza fedha kiasi gani?

  Najua sheria za Tanzania zinapinga kufanya cross market listing, kwa kisingizio cha kuepusha capital flight. Lakini hivyo ni visingizio vinavyofanya watanzania wazidi kudumaa na kuogopa biashara za maana.
   
Loading...