Hapa nimetoka kapa. Ngoja nikaoge na maji bariiidi nikirudi niisome tena labda nitaielewa hii thread ili nianze kuichangia.Kuna wanawake wanaoamua kutokuolewa na wanapendelea kuwa na mabwana, hawa mabwana either wanakuwa waume za watu, waliofiwa na wake zao au wanaume waliochelewa kuoa.
Faida za kuwa mistress:
- Hufui nguo za mwanaume, akitoka kazini anapitia kwako, nguo anaenda kufua mke wake, house boy au anafua mwenyewe weekend.
- Hupiki chakula, mara nyingi anakutoa kwenda kula sehemu sehemu.
- Ananunua zawadi maaana anapenda kukupa furaha muda mwingi.
- Huna kelele za mawifi kukuchukia, mama mkwe hakupendi, hujui hata ndugu zake.
Alafu ukizaa kinaitwa haramu hata kama sio kweli,
Alafu ukipata mimba itabidi utoe ili asigombane na mke wake manayake wewe ni mbuzi wa kafara,
Haya tupe na hasara tupime kwenye mizani msawazo
Unajua maisha ni mtihani, tunakosea pale tunapo copiana formula.
Sure, ndo maana nikasema always kila mtu atasifu alichochagua.
Huwezi kuwa umechagua maisha ya ndoa ukaja hapa kuanza kuponda habari za kuoa wakati bado uko kwenye ndoa na huna mpango wa kuacha.
Vivyo hivyo kwa aliyechagua mwenyewe kuwa single, hawezi kuja kuuponda huu mfumo, labda tu awe amelazimishwa.
Yap, hii formula ya kuolewa na kuishi raha mustarehe wengine imewafanya wameishia kwenye ndoa zenye matatizo.