The Bashite Effect: Ministerial responsibility VS State responsibility

Duh, nimeisoma mwanzo mwisho, pamoja na kutokujua kesho yangu. Nimeipenda na kuilewa vizuri sana, tatizo wanazani wataweza kuuficha huu moto wanaokoka. Sawa watauficha nje tusiuone, je hata moshi watauzuia nje usitoke?
 
Bishop Dr Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, kama mtumwa wa Yesu Kristo alishatoa unabii juu ya huyu ndugu Daud Albert Bashite a.k.a Paul Makonda kwamba;

Huyu aondolewe katika nafasi hiyo ya kuongoza mkoa mkubwa kama DSM, hajafikia level hiyo....

Na kwamba, huyu ndugu si kwamba hastahili ama hafai kuwa kiongozi, ila wakati wake wa kushika nafasi kubwa na nyeti kama hiyo ulikuwa bado haujafika. Alistahili kuendelea kusubiri...

Kwamba, kama Rais anamhitaji kuwa karibu naye, basi isingekuwa vibaya akampa kazi ya usimamizi wa usafi wa vyumba na kufagia viwanja vya Ikulu huku akijiendeleza kimasomo kujenga na kupata ufahamu wa mambo, afuzu na kutunukiwa vyeti vyake halali na kujifunza uongozi hadi atakapokuwa tayari kwa nafasi kama hiyo....

Mtumwa wa Yesu Kristo Mch. Josephat Alimalizia kwa kuonya kuwa, kama mamlaka iliyomweka hapo alipo itapuuza ujumbe huo, basi taifa lijiandae kulipia ujinga wa Bwana Bashite dearly....na tunaona kidogo kidogo tunaanza kuona huku mamlaka yake ya uteuzi ikiwa imepigwa ganzi!!

Hopefully, si muda mrefu unabii utatimia kwa ukamilifu wake maana Mungu akisema, huwa hageuki nyuma.....akisema jambo huwa linakuwa!!
 
Braza Malcom wakisoma hapa kwa makini wataacha ule msemo 'Rais ana nia nzuri ila anaangushwa na wasaidizi wake'. Wamekuwa wakitaka kutuaminisha kuwa Serikali na Rais hawahusiki na matendo mabaya ya wateuliwa.
 
Hahaha!! Hii mada itabidi nimalize kazi kwanza kisha nitarudi!

Halafu Malcom unajua ukini-tag kwenye thread huwa sipati notification? Hii thread yenyewe nimekutana nayo tu by chance!

BRB!!
 
Hahaha!! Hii mada itabidi nimalize kazi kwanza kisha nitarudi!

Halafu Malcom unajua ukini-tag kwenye thread huwa sipati notification? Hii thread yenyewe nimekutana nayo tu by chance!

BRB!!
Huu mchongo nilishasanua mapema tokea ule uzi wetu wa Elimu. Sasa wewe fanya kurudi
 
Mkuu nikushukuru kwa bandiko lako, naomba nibangaize senti sumuni
Usomi unatafsiriwa vibaya.

Elimu ni zaidi ya sifa za kitaaluma, certificate hafanyi awaye kuwa msomi. Tatizo la Vijana wa Tanzania si damu kuchemka ni kukosa 'exposure'.

Kwa kukosa hicho, wengi hawaelewi 'scope' ya mandate wanazopewa.
Hawasomi vitabu, magazeti au kufuatilia habari za dunia


Uelewa wao ni mdogo sana. Hawaelewi nini kinaendelea duniani na 'sensitivity'

Kuna mwingiliano mkubwa wa siasa, uchumi, usalama na mambo ya jamii

Vijana hawaelewi 'Diplomacy' ni nini na inafungamanisha vipi majukumu yao

Rais Mkapa aliwahi kusema wakati wa JK, kuwa u-DC ilikuwa kazi inayofanyiwa 'vetting', akashangaa siku hizi inatolewa tu. Alitoa kauli hiyo wakati wa teuzi za ma-DC na nakumbuka mojawapo ilikuwa ya Kinondoni
Hadi siku tutakapoingia katika matatizo
Hatuna jinsi, utaratibu wetu ni mbovu. Hakuna checks and balances
Shukrani ndugu Nguruvi kwa huu mchango wako mkubwa. Naamini turatibu tutafika.
 
Malcom Lumumba

Mkuu nimeongelea suala la 'sensitivity' nadhani si wote wataelewa. Naomba niliweke sawa

RC X alipoamua kijiji kizima kuwekwa mahabusu ilikuwa habari ya dunia.
Ilibaki kuwa kichekesho kama vituko vya kawaida duniani tunavyosikia pia, ni suala ''local''

RC X akisema kijiji Y kina magaidi wa Alshabaab,si suala local. Linakuwa la kitaifa na kimataifa. Sababu ni moja, ugaidi ni suala ''sensitive' katika dunia, haliwezi kubezwa

RC akIkataza watu kutumia vyoo, hilo linabaki kuwa local na kituko kimoja katika dunia

RC akiruhusu ndugu zetu wa jamii ya albino ' waachwe tu' linakuwa la kitaifa na kimataifa. Mauaji au mateso ya ndugu zetu albino ni jambo ''sensitive'', haliwezi kupuuzwa na dunia

Madawa ya kulevya ni suala la kitaifa na kimataifa(sensitive. Unapoliongelea kama suala ''local' kuna impact katika image ya nchi. Unaeleza dunia tatizo la kitaifa kwa njia local

Kwa mwenye kujifunza kila siku kwa kusoma, kusikiliza, kudadidisi n.k. anaelewa nini ni jambo 'sensitive' ni lipi local na ukubwa wa madhara. Vijana wetu hawana weledi huo

Mwl Nyerere alifanya mambo ambayo tukiyaangalia leo tunaona alikuwa na maono sana
Vijana wa form 6 waliajiriwa kisha kwenda jeshini. ''Walijifunza uongozi'' na nidhamu za kazini

Mwl alianzisha chuo cha uongozi Mzumbe(IDM) ambacho wazee wengi wastaafu walipitia
Chuo kilitoa mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu kwa viongozi. Tumekiua leo hii

Wakati wa Mwl, uongozi ulizingatia ngazi, uzoefu na sifa katika kazi.
Sasa uongozi umekuwa ni kama 'chambo' au zawadi. Tunavua kila kitu kwa kokoro

Ndiyo maana tunajiuliza, katika zama hizi kuna haja ya kuwa na katiba bora.
Kuna maswali ya kujiuliza. Hivi kwanini DC au RC aletwe kutoka Dar es Salaam?

Kwanini mwenyekiti wa CCM achaguliwe na watu wa Wilaya na mkoa husika na si DC na RC?
Kwanini viongozi wateuliwe bila kuthibitishwa na mamlaka nyingine ili wawajibike kwa ukamilifu?

Mjadala si suala la Ushoga. Wengi wanachanganya na kuchanganyikiwa.
Kinachojadiliwa ni namna gani suala hilo limeanza na lilipofikia.

Jibu ni rahisi, suala zima halikuangaliwa kwa kuzinga 'scope na mandate' ya kazi, ''sensitivity ya kauli'', impact katika diplomacy, impact yake kwa nchi n.k.

Kwa kioo hicho, ni CEO gani wa dunia atakubali kuajiri Wtz waitie taasisi yake katika matatizo?

Katika Admin na management Watz tupo nyuma na tutaendelea kulalamika Wakenya na South Africa wanachukua kazi zetu. Tutazuia vibali vya kazi bila kujua, ''wachawi'' wetu ni sisi wenyewe.

JokaKuu
 
Awali ya yote naomba niseme kwa yakini kwamba, LONG LIVE PAUL MAKONDA as Dar es Salaam Regional Commissioner!! Chonde chonde Mheshimiwa Rais wetu mpendwa, Daktari John Pombe Magufuli, nakuomba sana, tena sana wapuuze hawa akina Malcom Lumumba wanaopenda kumsemanga RC wetu!! Hawana lolote hawa... wivu tu na husuda ndio vinawasumbua!

Nasema hivi... tuachieni Makonda wetu bhana, nyie watu vipi!!

Halafu mara Makonda hivi, mara Makonda vile... ebo! Wivu tu! Mheshimiwa Mkuu wa MKoa wa Dar es salaam, Paul Makonda mi nasema hivi... ENDELEZA VIMBWANGA baba hadi waiapate pate!! Mtu akiona fundo kwenye koromeo, mkatie hata tiketi aondoke Dar es salaam, ala! Hivi hawajui kwamba una uwezo wa kumwamisha mtu yeyote ndani ya jiji lako kisha akarudi kwao Kolomije?!

Endelea kutuvuruga baba... halafu kuna vimbelembele wengine hata Dar es salaam yenyewe hawajawahi kufika lakini kila siku Makonda! Makonda! Ebo!!

Hivi kama si Mheshimiwa Paul Makonda na vimbwanga vyake mngejuaje kwamba, fanya ufanyalo na hata bila kujali wadhifa wako, ukimgusa tu Paul, Mheshimiwa Rais wetu anakutupa kulee...dadeki!!

Hivi kama sio Mheshimiwa Paul Makonda, mngejuaje kwamba Mheshimiwa Rais anaweza kumshikisha adabu mtu yeyote atakayembugudhi RC wetu hata kama Paul anaamua kuchukua kikosi cha askari na kuvamia kituo chochote cha habari kitakachopinga kufanya anachotaka yeye!

Mnabisha? Kamuulizeni Nape Nnauye!

Hivi kama sio Mheshimiwa Paul Makonda mngefahamu lini kwamba, provided nawe ni mwanawe anayependezwa nae, basi Mheshimiwa Rais hawezi kukufanya chochote hata ukitaka kukwepa kodi for taxable goods ingawaje moja ya makosa makubwa kwa kiongozi wa umma ni ukwepaji kodi!

But eh, don' ever try this at home cuz' that right is exclusively reserved for our Dar es salaam Regional Commissioner, the elite himself, Paul Makonda!

Hivi kama sio Paul Makonda, mnadhani hii misembwe misembwenye na mkangara mikangaranyiko ya huko serikalini tungeifaidi namna hii?!

Hivi kama sio Mheshimiwa RC wetu Paul Makonda mngeweza kushuhudia kwa macho yenu jinsi Afisa Usalama wa serikali anavyoweza kutoa silaha ya moto hadharani tena mbele ya vyombo vya habari na kutaka kumripua RIIIPUU, Mbunge aliyechaguliwa na wanachi?!

Muulizeni Nape alivyonusurika kufumiliwa ubongo mbele ya kamera!

Mheshimiwa Paul Makonda ni chachu iliyo-balance vizuri chumvi, ndimu na pilipili kiasi kwamba inaweza kuonesha vema kabisa unafiki uliotukuka wa nanii yulee... SIMTAJI NG'O!! Mnataka nimtaje halafu ajue kwamba namsimanga halafu aache kuendeleza mahaba niue kwa mwanae anayependezewa nae!!!

Itoshe tu kusema kwamba, the existence of Paul Makonda in the government provides a million reasons to suck this government!

Sijamaliza...
 
THE BASHITE EFFECT:
Nchini Tanzania kuvunja muungano ni jambo rahisi sana kuliko kumfukuza kazi Makonda.


Uongozi ni sayansi,
Sayansi ni muunganiko wa kanuni mbalimbali za kitaalamu zilizothibitishwa kitaalamu katika nyanja husika. Hivyo basi kama unataka kukokotoa hesabu za magazijuto ni lazima ufuate kanuni zake za kitaalamu ambazo zimethibitishwa kitaalamu.


Basi uongozi hauna tofauti kabisa na kukokotoa hesabu za magazijuto, ukifuata kanuni lazima ufanikiwe na usipofuata lazima utafeli tu. Lakini tofauti kabisa na sayansi nyingine za dunia hii, UONGOZI WA KISIASA ni sayansi ngumu sana kuliko zote kwasababu ili kupata majibu yake haitegemei pekee utashi na mchango wa kiongozi wa kisiasa, bali pia utashi na mchango wa watawaliwa.

Sasa ili kuhakikisha hili linafanyika sisi kama watanzania tuliamua kutengeneza Sheria, Kanuni na Taratibu za kiutawala. Bahati mbaya sana leo hii tumeamua kuzikanyaga kwa makusudi kwa kutumia msemo wa "kunyoosha nchi" bila kufikiria mbali kwamba uongozi ni sayansi ambayo ni lazima isomwe vizuri na kanuni zake zifuatwe ndiyo nchi huweza kwenda mbele. Hapa haitajalisha kwamba wewe una nia njema na nchi au una uchungu sana na nchi. Usipofuata kanuni na taraibu zilizowekwa na hata kukufikisha wewe madarakani lazima utaingia tu kwenye shimo "You are doomed to fail".

Historia inatufundisha kwamba hii imekuwa ndiyo Sheria Kuu ya Uongozi tokea miaka 5000 iliyopita (Kabla ya Kristo)ambapo ustaarabu wa kwanza wa binadamu ulianza kujengeka huko Mesapotamia. Kibaya zaidi na kinachoogopesha ni kwamba dunia imebadilika sana hivyo kuongezea kanuni mpya sana katika sayansi ya uongozi. Dunia ya wakina Mfalme Koreshi wa Umedi, Mfalme Charlamagne wa Roma, Mfalme Napoleon wa Ufaransa hadi Kaiza Wilhelm wa Ujerumani ni tofauti sana na dunia ya wakina Kagame wa Rwanda na Magufuli wa Tanzania. Hii dunia ya karne ya ishirini na moja ni mbaya sana kwasababu hakuna tendo utafanya au neno utasema katika uongozi lisilje kuwa na madhara mazuri au mabaya kwa wananchi wako na dunia nzima kwa ujumla: Huu ndiyo utandawazi wenyewe.

Sasa hayo ya juu ni kujenga msingi tu, kilichonileta leo hii hapa ni hili swali moja tu:
Hivi inawezekanaje vitendo vya muhuni mmoja anayejiita Paul Makonda viweze kuhatarisha na kutishia mustakabali mzima wa mfumo utawala wa nchi hii bila hata viongozi wa nchi kustuka kwa namna yoyote ile ? Ndiyo, huyu ni muhuni kwasababu mpaka sasa serikali imeshamkana mara tatu mbele ya ummah kwa vitendo vyake viovu ambavyo vilihatarisha usalama na amani ya nchi hii. Watanzania ni watu wasahaulifu sana lakini hebu tuweke kumbukumbu zetu sawa juu ya huyu mtu kukanwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano:


Mosi, alivamia kituo cha habari kwa kutumia vyombo vya dola na kuwateka waandishi wa habari huku nchi nzima na dunia ikishuhudia.
Mwitikio wa kwanza wa Serikali ulikuwa ni kwenda kulaani kitendo hicho na kusema siyo cha Serikali bali cha mtu huyu kiongozi binafsi.
Aliyefanya hii kazi ni Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo wa wakati huo Ndugu Nape Nnauye. Lakini baada ya lile tukio Nape alitumbuliwa na likatokea songombingo la yeye kutishiwa silaha ya moto na moja ya askari wa usalama ambaye inasemekana alifanya hivyo chini ya maelekezo ya huyu Mhuni anayejiita Paul Makonda. Baada ya lile tukio Raisi wa nchi Mzee Magufuli alikemea vyombo vya habari huku akimkana tena Makonda na kusema hivi "Waandishi wa habari wanaripoti vitu vya kichochezi kwenye magazeti utadhani Serikali ndiyo ilibariki kitendo hicho (Cha Nape kutishiwa Bastola)"


Pili, aliingiza makontena yenye bidhaa zake binafsi kinyume kabisa na sheria za nchi na akakataa kulipa kodi huku akizitishia mamlaka za Serikali akiwemo Waziri wa fedha na mipango kwamba atawashitaki kwa Raisi wa nchi kwa kosa la kuwa wazalendo kwa nchi yao. Hili kwenye utawala tunaita ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu mno "First Degree Insubordination". Sakata likaendelea Raisi wa nchi akainuka na kumkana kwa mara ya pili na kusema kwamba zile siyo bidhaa za Serikali hivyo Mkuu wa Mkoa ni nani hata asilipe kodi. Hivi umewahi kujiuliza madhara ya muda mrefu ya hili songo-mbingo kiutawala ?? (Nategemea waungwana wote washaelewa)

Tatu, juzi tena serikali imemkana kwa mara ya tatu mbele ya nchi na dunia nzima kwa ujumla kwamba kile kitendo cha kuwasaka mashoga ni matakwa yake yeye kama Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na siyo msimamo wa Serikali. Nahisi yeye na washauri wake walishindwa kutofautisha kisheria kati ya "Vitendo vya ushoga" na "Kuwa shoga" au kwa lugha ya kiingereza tunasema be failed miserabaly to draw a distinction between "Homosexual acts such as having carnal knowledge of the member of the same sex group against the order of nature" and "Being a homosexual". Je, vitendo vya ushoga ni makosa kisheria ?? NDIYO ni makosa kisheria, tofauti kabisa na maadili ya watanzania na Sheria haitambui ndoa ya jinsia moja. Hivyo tutaendelea kuvikemea hivyo vitendo kwa nguvu zote: Lakini Je, unahisi mbinu ambazo Paul Makonda alizitumia katika kuwasaka hawa watu zilikuwa ni sahihi ?? (Hili nakuachia ujibu mwenyewe)

Hayo yote niliyoyataja hapo juu yanatupeleka kwenye Kanuni mbili za Kisheria na Kiutawala kama ifuatavyo:
1. Kanuni ya Ministerial Responsibility
2. Kanuni ya State Responsibility


A: MINISTERIAL RESPONSIBILITY
Hii ni moja kati ya kanuni muhimu sana ya Kikatiba ambayo hujenga msingi wa utawala wa nchi. Kanuni hii inataka Serikali nzima kuwajibika kwenye Bunge kwa vitendo vyote ambavyo imevifanya. Hivyo kitendo cha kiongozi moja Serikali "The Executive" akifanya jambo bovu kiutendaji basi inayowajibishwa ni Serikali yote (Collective Responsibility). Au mara nyingine kanuni hii humwajibisha waziri husika katika kila majukumu anayofanya ndani ya wizara yake "Individual Ministerial Responsibility". Pengine kueleweshana zaidi Serikali haiwajibiki kwa Bunge bali wananchi, ila inaenda kwa Bunge kwasababu bunge huwakilisha wananchi wote na kwasababu kitendo cha demokrasia ya moja kwa moja "Direct Democracy" hakiwezekani kwenye nchi ya watu zaidi ya milioni 50. Japo zamani huko Ugiriki ya kale sehemu kama Athens viongozi wote wa Serikali waliwajibika moja kwa moja mbele ya Ummah kwasababu idadi ya wananchi haikuwa kubwa sana kama ilivyo leo hii.


Upande wa pili, kutokana na kukua na kukomaa kwa utawala hapa duniani Serikali hii kanuni haifanyi kazi tu kwa mawaziri. Hivyo jina lisikuchanganye kabisa. Hii hufanya kazi kwa kila kiongozi wa Serikali ambaye anapokea amri kutoka kwenye muhimuli wa Serikali "The Executive". Hivyo basi inagusa hadi matendo ya Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya hadi Wakurugenzi. Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kwenye Ibara ya 35(1) inasema kwamba kila kiongozi wa Serikali atafanya kazi kwa niaba ya Raisi"

Sasa hivi wakina Dr Mahiga na Dr Kilangi wanavyotuambia kwamba yake anayofanya Paul Makonda siyo matakwa ya Serikali huku Serikali inanyamaza kimya bila kumchukulia hatua yoyote ile, wanaamaanisha kwamba Dar es Salaam inatawaliwa kwa Sheria tofauti na zile za sehemu nyingine au Dar es Salaam ni nchi huru ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama ambayo Vatican iko huru ndani Italy ??? Huu ni upumbavu wa Karne. Katika sheria za utawala ili kuonesha kwamba Serikali haijabariki vitendo vya viongozi wake basi ni lazima ichukue hatua ya kumfukuza au kumpa adhabu. Marehemu Mzee Kingunge akiwa Waziri alishawahi kukataa waziwazi kuunga mkono Serikali ya Mzee Nyererena kilichofuata Chama na Serikali kumwambia ajiuzuru. Mifano iko mingi sana kuanzia wakina Mzee Emilio Mzena, Mzee Ali Hassan Mwinyi na Mzee Lowassa.

Hawa wazee ilibidi wafanye hivi kutunza heshima ya Serikali, Sasa huyu Makonda ambaye amekanwa wazi wazi lakini hafanywi kitu tutaaminije kwamba anachofanya hakina baraka za serikali ?? Hivi mmetuona sisi watanzania ni wajinga sana eeh ??

Makonda anahatarisha usalama wa nchi pamoja na uongozi wake maana mwisho wa siku jumba likianguka lawama zote atakayebeba ni Raisi Magufuli kwasababu viongozi wote wanafanya kazi kwa niaba yake kama Katiba isemavyo. Huyu Makonda asipochukuliwa hatua stahiki mapema basi atakuwa ni chanzo kikubwa sana cha anguko la Serikali ya Magufuli.

B: STATE RESPONSIBILITY
Hii ni kanuni ya kwenye Sheria za Kimataifa, Sayansi ya Siasa na Diplomasia inayosema kwamba Serikali ya nchi fulani itawajibishwa kwa vitendo viovu vya mawakala wako dhidi ya nchi nyingine, mali zake au makampuni yake. Hapa mawakala wanaweza kuwa Mawaziri, Wanajeshi au Majasusi ili mradi tu wawe kwenye nafasi ya kuiwakilisha nchi yao na maslahi yake. Nitoe mfano Mzuri tu mwaka 1988 majasusi wa Libya walilipua ndege Pan Am Flight 103 na kusababisha vifo vya wasafiri 243 na wahudumu 16. Libya alikana kuhusika lakini Ghadaffi aliambiwa kwamba kama Serikali haijahusika basi lazima ionyeshe ushirikiano katika kuwakamata hao majasusi waliofanya hivyo


Upande mwingine mwaka 1985 Serikali ya Ufaransa iliingia kwenye mtafaruku baada ya kulipua meli ya New Zealand (The Raibow Warrior) ambayo ilikuwa inaende kuzuia majaribio ya Silaha za kinyuklia za Ufaransa ambayo yalikuwa yanahatarisha mazingira. Serikali ya Ufaransa ilikana kutokuhusika na tukio hivyo kuwakabidhi majasusi waliohusika na kuwapa adhabu ya kifungo cha miaka kumi kwasababu walifanya kitu ambacho Serikali haikuwaagiza. Ina maana Serikali ya Ufaransa ingekataa uhusika bila kuchukua hatua yoyote ile ingeonekana kwamba imehusika moja kwa moja na kile kitendo.

Turudi kwa Paul Makonda: Hivi mngefanya nini kama huyu jamaa angeanza kuwakamata na kuwafanyia vurugu raia wa kigeni ambao wanasemekana ni mashoga waliofunga ndoa wakiwa huko nchini kwao na kuja hapa Tanzania kikazi au kiutalii ?? Sitetei Ushoga lakini hebu tujiulize vizuri kuhusu hili suala. Hivi mataifa ya nje yangetuelewa ? Au tungefanya kama ambavyo Waziri Hamis Kigwangalah alipendekeza "Machoko Wasiingine nchini kwetu na tuwazuie huko Airport". Kwanini tusifuate Approach ya Urusi kuhusina na Ushoga. "Not recoginised, Not segregated, Un-Violable as long as You don't Ask and Don't tell" Kuna ugumu gani hapa ?? Au mnaogopa ??

Tukiangalia kwa mapana mpaka sasa inaonyesha ni dhahiri Paul Makonda ni kichaa aliyepewa Rungu, ana nguvu kubwa sana kisiasa na anaweza kufanya jambo lolote lile hapa nchini. Kama huyu mtu hatafungwa lijamu mapema huko mbeleni anaweza kufanya vitu vya ajabu mno. Hivi ingetokea kwamba kawadhuru raia wa nje na hata kupoteza maisha unategemea nchi itakuwa kwenye hali gani ??

Au hata huko mbeleni akafanya kitu chochote kibaya dhidi ya makampuni au raia wa kigeni (Maana Hashindwi kabisa) tena hasa kipindi hichi ambacho Chama cha Mapinduzi (CCM) kinaamini kwamba kinapambana na mitandao ya Kibepari ndani ya nchi unategemea nchi itakuwa kwenye nafasi gani ?? Bado hamuanini tu, katika hili ninalosema ?? Hebu ngoja niwape mifano ya mwisho na tufunge ukurasa:

Mfano wa kwanza, Mzee Edward Lowassa alikuwa ni mwanasiasa mwenye nguvu sana hapa nchini, mwaka 2014 akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi ya Bunge aliwahi kuongea Kauli ambayo ilitaka kuiingiza nchi kwenye matatizo. Kuhusu Malawi alitishia na kusema kwamba "Liwalo na liwe" huku huo haukuwa msimamo wa nchi na mwenye mamlaka ya kusema hivyo ni Amiri Jeshi Mkuu pekee. Mzee Jakaya alipoenda kwenye kikao cha SADC aliikana ile Kauli kwa kusema kwamba yeye ndiyo Amiri jeshi hivyo Lowassa apuuzwe. Kama Malawi ingekuwa ni nchi yenye nguvu kama Ethiopia sidhani kama tungekuwa kwenye mahusiano mazuri mpaka leo hii.

Mfano wa pili, Vita ya kwanza ya dunia iliyoua mamilioni ya watu ilianzishwa na kijana mdogo, mwenye akili mbovu na fupi kama Paul Makonda. Gavrilo Princip alikuwa ni mwanaharakati anayepigania Uhuru lakini kwenye genge lao la Kigaidi al maarufu kama The Black Hand walidanganyana wamuue mwanamfalme wa Austria Hungary bwana Ferdinand. Walivyomuua Serikali ya Bosnia ikajidai kutaka kukana kuhusika huku ikiwalinda hawa magaidi kama ambavyo Serikali yetu inamlinda huyu muhuni. Kilichotokea ni kwamba nchi nzima ilivamiwa na mataifa makubwa kisa kigenge cha wahuni wachache tu

NB: Unaweza kusema nimewaza mbali au kubeza ninachosema hapa lakini kama mtu alidiriki kumfanyia shambulio mtu mzalendo, mzee, Makamu wa Raisi Mstaafu, Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Mstaafu na Mwanasheria Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba uandhani kuna kitu ambacho mtu wa namna hii anaweza asikifanye ??? Tena kama alifanya wakati hana hata ushawishi, je leo hii alivyokuwa na baraka za Raisi wa nchi kufanya anachokitaka atashindwa kufanya lolote hapa nchini ???

Juzi pale Mlimani Raisi umesema tuwavumilie hawa vijana kwasababu damu inachemka lakini nia yao ni njema tu, Sisi tunasema hivi:

Mosi, Nchi inaongozwa kwa kanuni na taratibu tena tunategemea hawa vijana wasomi ndiyo wawe mstari wa mbele kutii sheria.

Pili, Tuwavumilie mpaka lini wakati kila siku matendo yao ndiyo yanaongezekana kasi ??

Tatu, Je tuwavumilie hata pale ambapo wanatishia Usalama na mustakabali wa taifa hili ambalo umelipokea likiwa na utulivu ??

Nne, Hawa vijana wako wakivuruga nchi yetu na kuumiza maelfu ya watanzaia wewe kama Raisi utakubali kubebe wajibu ??

CC: chige , zitto junior , Kiranga
Imekaa vizuri mkuu.Ni political analysis ambayo imefanya mjadala wa haki na wa haja.Big Up...!
 
Andiko zuri lenye rejea za kutosha

Ukitizama suala la RC Makonda kiundani utaona ni kama toto kubwa (a big baby) linalofanya jambo mbele ya baba likikanywa na majirani linaenda kujilizaliza.

Tutaona mengi, easy furahiday
Exactly... Angekuwa na busara, huyu DAB angeimarika zaidi kisiasa kwa kuwa hakuna alichokikosa. Amekuwa akifanya kila kitu; lakini kwa UPUMBAVU,UPOFU na KULEWA KWAKE MADARAKA,amechagua kufanya in negativity way badala ya kuwa positive. Hili ni tatizo...na ni mkulu pekee ndiye anayeweza kuliondoa.Otherwise, tuombe uhai, tutaona mengi.
 
Mchuma janga hula na wa kwao..
Watu zaidi ya milioni 50... Hatima ya maisha yetu na mahusiano mema na watu wengine... Yanachafuliwa na Joji Poji.. Na mwanamfalme mpendwa..

Uongozi si majigambo, vitisho na visasi.. Uongozi ni busara, ushirikiano na kuthamini michango ya wengine..
Exactly
 
Hadi milele Makonda yuko SAHIHI 100% kuhusu ushoga. Yaani jitu linajiita Great thinker kwa hoja za oooh anahatarisha uhusiano na Jumuiya za kimataifa. Huu ni upumbavu kiwango cha SGR. Umaskini, UNAFKI na UDHANDIKI ndio ugonjwa wa mwafrika. Ant makonda watapiga sana kelele kuhusu hili na naamini hata angekuja na ya kuwalinda mashoga bado madesa mithiri ya biblia yangejaa humu kuonesha hayuko SAHIHI. Iwe vikwazo iwe nini lzm kama taifa tuwaoneshe hao mabwana zenu kuwa Tanzania hatutaki USHOGA. Great thinker hana haja ya kuleta fake story za mara clouds mara nape ili kutetea hoja za Kishoga. Tena nyie mnaotetea hili jambo MNALAANA.
Kwa hiyo, agenda hiyo imeishia wapi? Tatizo ni kuibua agenda nyingi na hazifiki mwisho. Kwa mfano, dawa za kulevya, watoto/akina mama waliotelekezwa, waliojenga mabondeni, DNA, usafi kila....pale DSM, kutembelea maeneo mbalimbali kusikiliza kero za wananchi....n.k ni baadhi ya agenda alizokuja nazo DAB lakini hakuna hata moja iliyofika mwisho. Hapa utagundua kwamba jamaa ni shida.
 
Back
Top Bottom