The Article of Union between the Republic of Tanganyika and the Peoples Republic of Zanzibar

Twende mbele zaidi maana kuna kizazi hakitaki kujua historia wala kuangalia historia:
Tanzania: Polity Style: 1964-2010

22 Apr 1964 The Articles of Union between the Republic of Tanganyika and the People's Republic of Zanzibar are signed at Zanzibar, providing for the union of Tanganyika and Zanzibar

25 Apr 1964 The Articles of Union are enacted in Tanganyika and Zanzibar 26 Apr 1964 An Act to ratify the Articles of Union between the Republic of Tanganyika and the People's Republic of Zanzibar, to provide for the government of the United Republic and of Zanzibar, to make provision for the Modification and Amendment of the Constitution and Laws of Tanganyika for the purpose of giving effect to the Union and the said Articles, and for matters connected therewith and incidental thereto (No. 22 of 1964) becomes effective on the Union Day

26 Apr 1964 - 11 Dec 1964 Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar = United Republic of Tanganyika and Zanzibar

29 Oct 1964 a decision of the Cabinet to change the name to Jamhuri ya Muungano wa Tanzania = United Republic of Tanzania is publicly announced

11 Dec 1964 An Act to change the name of the United Republic (No. 61 of 1964) becomes effective upon publication [1]

11 Dec 1964 - Jamhuri ya Muungano wa Tanzania = United Republic of Tanzania 



Angalieni hizo tarehee..
 
Marehemu Prof. Haroub Othman akielezea suala hili la uhalali wa Muungano anasema hivi:

Under both the 1962 Republic of Tanganyika Constitution and the Zanzibar Presidential Decree No.5 quoted above, the two Presidents had the powers to enter into international agreements on behalf of their governments. What is also important is that the Union Agreement was ratified by both the Tanganyika Parliament and the Zanzibar Revolutionary Council. Contrary to what some writers have said, the Nyalali Commission was satisfied that the Revolutionary Council met to ratify the ‘Articles of Union’. Both Abdulrahman Babu and Khamis Abdallah Ameir, the two former Umma Party leaders who were in the Revolutionary Council at the time, have confirmed that the matter was discussed in the Council, and while there were reservations on the part of some members, these were ‘quashed’ by Abdallah Kassim Hanga who made an emotional intervention to support the Union.

Bado watu wanahoji uhalali wa Muungano?
 
Jee endapo muasisi wa muungano hayati abeid amani karume angalifufuka muungano huu angauliuataka?1) zanzibar imekuwa kama gofu tu baada ya miaka 36 bila ya karume na miaka 46 baada ya uhuru2) biashara ya zanzibar imekufa baada ya bandari ya zenj kuwekewa mizengwe.3) rais wa zanzibar kukosa hadhi ya kitanzania na kimataifa4) michezo zanzibar imekufa hasa baada ya tff kuikandamiza tff5)tra kuibana zenj6) hisa za biot za zenj kutopata majibu licha ya smz kuomba kupatiwa document7)licha ya serekali inayoongoza na ya ccm, lkn tofauti ya mishahara kati wafanyakazi wazenj na muungano ni kitendewili.
1.Mkuu MS, umecharaza sana hoja yako, japo kimsingi inaeleweka.

2.Mi natamani wazee hawa waasisi wangekuwepo hadi leo, maana walichoasisi wao ndo hicho kimetumika weee, na sasa kinakufa, hakuna mabadiliko.

Viongozi wetu wa sasa wameshindwa kuboresha muungano ili at least uwe na sura ya kisasa zaidi...Kama tulianza na serikali mbili baada ya Muungano, kwanini wasilifanyie kazi hili tukasonga kwenye serikali moja baada ya miaka46?..

Tunaongelea juu ya EAC, AU etc, kwanini tusingalianza na kuunganisha serikali za bara na visiwani?..
Huyu mzee anagalifufuka angezimia na kurudishwa tena kaburini!
 
wala siyo siri kama watu wengi wanavyoamini... hivi kuna mtu kawahi kuuliza kama makubaliano hayo hayapo Ikulu ya Dar na Zanzibar? kuna mtu kauliza kama mkataba huo haupo Umoja wa Mataifa? tunaambiwa kuwa mwanasheria mkuu alipoulizwa alisema kuwa yeye hana.. lakini kuna mtu kauliza kama Mwanasheria Mkuu wa Tanzania anao - clue.. na yeye hana!! Mtu mwingine atasema kwa vile wamesema hawana ina maana "haupo"; lakini swali sahihi ni je walitakiwa kuwa navyo!!!?

kuna watu hawana kazi za kufanya, wao ni kuropoka tu kila siku!
 
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hadi sasa una kila dali za muungano wa kisovieti (USSR).Yaani matatizo yaliyoko yanashabihiana na matatizo yaliyovunja muungano wa soviet ya Zamani.JK ni Mikhail Gorbachev ila we sema tu kuna nguvu kidogo iliyokosekana kutoka Zanzibar
 
Lakini hii document iko too open! Inaonyesha ni kitu kilifanyika chap chap! Pia inaonyesha Karume alikubali kushushwa cheo to vice-President...at least for the interim period! Sasa sijui Urais alikuja kurudishiwa kinyemela?
 
Watanzania tunatimiza miaka 46 ya muungano wakati hali ya jamii kisiasa uchumi na elimu vikiwa katika hali ile ile ya miaka 46 iliyopita , taifa likiwa chini ya umiliki wa watu wachache wanaoweza kutoa mwongozo kwa watawala wetu nini wanataka , kwa ujumla nchi imetekwa na tabaka la matajiri, je tuliongana ili tule pamoja umaskini wetu? au tuishirikiane katika kuuza kwa wageni rasilimali zetu? au kujenga mazingira ya ubaguzi wa kipato?
lazima tutafute malengo ya muungano na kwanini hayafikiwi?
 
Mi naona hata aibu kutamka hiyo miaka (46)..Natamani tungesema ni miaka 2 ya Muungano!
Ni muungano gani usioleta tija huu?...Mawazo mapya yalikufa na kuzikwa na akina Karume?
 
Lakini hii document iko too open! Inaonyesha ni kitu kilifanyika chap chap! Pia inaonyesha Karume alikubali kushushwa cheo to vice-President...at least for the interim period! Sasa sijui Urais alikuja kurudishiwa kinyemela?

Soma vizuri Article iii b na vii uone kama Karume alinyang'anywa urais wake!
 
Lakini hii document iko too open! Inaonyesha ni kitu kilifanyika chap chap! Pia inaonyesha Karume alikubali kushushwa cheo to vice-President...at least for the interim period! Sasa sijui Urais alikuja kurudishiwa kinyemela?

hata leo tukitaka kuungana na kuwa Taifa moja Afrika ya Mashariki kuna viongozi watakaobadilishwa vyeo na hata kupoteza nafasi zao. Tatizo kubwa la wanasiasa ni kujua ni wakati gani kukubali kukunja. Nyerere alikuwa tayari kumuachia Jomo Kenyatta Urais endapo tungekuwa tumeungana wakati ule; Karume na Nyerere wasingeweza wote kuwa Marais wa Jamhuri mpya.. Karume alikubali kusacrifice.. that is a mark of a leader!

Tatizo moja linalosumbua Muungano sana sasa hivi ni viongozi kutaka yote na peke yao, matokeo yake hawajajifunza sanaa ya kucompromise!! Kwani George Washington alipopendekezwa kuwa Rais wa kwanza wa Marekani hawakuwepo wengine waliokuwa na uwezo zaidi yake? Walikuwepo na baadaye waliweza kushika nafasi hiyo.
 
Miaka 46...kama matunda basi sasa yangekuwa yamekomaa mpk yanaanguka yenyewe mtini....lakini si muungano wetu wachache wanafaidi wengi wetu tumebakia kuwa watazamaji....Ila yana mwisho!!!
 
sitaki hata kusikia huu upuuzi muungano kwa ridhaa ya nani? sijaona manufaa ya huu mgawanyiko aka muungano
 
Yote tumeyaongea, na popte duniani inaaminika muungano ni jambo la heri ilimradi tu uwe sio wa kusurutishana...hata mababu walisema umoja ni nguvu, hivyo mi binafsi sidhani kama napinga swala la watu kuungana. Ila nadhani Watanzania hasa wa kizazi hiki kuna haja ya kuwapa majibu ya maswali haya mawili yayokinzana ili kuupa uhai mpya muungao huu (kwani nyakati zimebadilika hivyo kun haja ya ku -uhuisha {revamp} muungano huu katika mioyo ya Watanzania) maswali la kujiuliza ni haya mawili:

(a) Muungano huu umemsaidia nini Mtanzania wa kwaida mpaka sasa ili awe na sababu ya kuulinda??

(b) Muungano huu umemuongezea Mtanzania kwa kawaida matatizo gani ya kumfanya auvunje????

Tukiyajibu haya tutapata sababu na muelekeo wa kimsingi kuhusu mustakabali wa muungano huu....

Sayonara!!!
 
Back
Top Bottom