Thanksgiving

Thanksgiving

Evarm

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2010
Posts
2,000
Reaction score
1,560
Nawasalimu wana MMU,

Ilikuwa ni siku ya Jumatano saa nane mchana tarehe 21/08/2013, nikiwa Bwagala Hospital ya Kihonda nilimpoteza mwanangu kipenzi Glory. Nilimpenda sana alikuwa ana miezi sita na siku 15 tu na ndio mtoto wangu wa kwanza lakini Mungu alimpenda zaidi yangu. Nimeumia sana kwa hili ila najisikia kutoka rohoni ya kuwa natakiwa kumshukuru Mungu. Najua Jumamosi hii anatimiza mwezi simuoni machoni, sinyonyeshi.... n.k. Nabaki kuangalia nguo zake tu na kulia

Napenda kuwakaribisha KKKT Majengo wana MMU wote walioko kihonda maghorofani, kumshukuru Mungu pamoja nami. Nitatoa shukrani ya pekee kumshukuru Mungu wangu maana alinipa Glory mwanangu(kwangu ni zaidi ya zawadi) na amemchukua.

Karibuni wote mtakaokuwa tayari kumshukuru Mungu pamoja nami.
Evarm.
 
pole mkuu...always Mungu anamakusudi na kila jibu...na ni jambo zuri kumshukuru kwa kila jambo pia...
 
pole sana mkuu Mungu kampenda zaidi, Nami naungana nawe kumshuku Mungu kama zaburi inavyo sema mshukuru Bwana kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake ni za milele.atakufadhili wakati wote na kukupa mtoto mwingine
 
Pole sana mkuu, kazi ya Mungu haina makosa!!ningekua moro lazima ningekuja tu..
 
Dah!!!!!!!!
Pole sana......

Naamini Mungu amempokea huyo malaika!!!!!!
 
Pole sana mamie... Ila kumbuka Mungu hataruhusu tujaribiwe zaidi ya uwezo wetu.
Soma katika 1 Wakorintho 10:13
"Jaribu halikuwapata ninyi isipokuwa lililo la kawaida ya wanadamu ila Mungu ni
mwaminifu ambaye hatawacha
mjaribiwe kupita mwezavyo lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea ilimweze kustahimili."

Pia Mungu ameahidi kutuondolea
huzuni, kilio, kifo na shida zote.

Imeandikwa, Ufunuo 21:4

"Naye atafuta kila chozi katika
macho yao, wala mauti
haitakuwapo tena wala
maombolezi wala kilio, wala
maumivu hayatakuwapo tena
kwa kuwa mambo ya kwanza
yamekwisha kupita."

Pole sana... Mwenyezi Mungu akutie nguvu!!!
 
ni vyema kumshukuru Mungu kwa kila jambo, yeye ndie aliekupa na akaamua kumchukua..pole sana.
 
Asanteni wote, mbarikiwe.
 
Mshukuruni Bwana kwa kila jambo, maana kazi yake haina kosa....
 
Pole sana. Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe...amen.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom