Thanks GOD, Thanks JF!


Uzuri mmoja ni kwamba Kanali Kikwete hawezi kushauri utungwaji wa sheria ya aina hiyo kwani naambiwa naye hakufanikiwa kuiona nyota ya kijani, sasa unadhani ataanzia wapi?
Mkuu usisahau kwamba mtaji wa mmatumbi ni watoto, na tunazingatia sana maandiko matakatifu "zaeni mkaijaze nchi". Maandiko hayatuelekezi kwenye nyota ya kijani.
 
Mama na mtoto wanaendelea vizuri........... hii ni habari njema. Je wewe mwenyewe unaendeleaje?


Mzee mwenzangu unapenda sana uchokozi.....

Unajua tu kwamba huyo jamaa anaumwa sana kwa muda mrefu sana wa miezi 9-x na bado ataendelea kujiuguza kwa siku nyingine kibao, walau 40+y.....

Sasa kwa nini unamuuliza wakati huwezi kumpatia ushauri nasaha au tiba mbadala??

Babu DC!!
 


Huyo Kanali ameongoka kama Sauli....kwa hiyo lazima atawashikisha adabu wale ambao hamtaki kusikia.....

Kaka huo mtaji mbona siku hizi utakuwahisha kwenye maisha bora negatively....???

Babu DC!!
 
Nakushukuru sana mum kwa upendo wa dhati uliouonyesha na unaoendelea kuuonyesha kwa familia yetu. Nitazidi kukuombea heri ufanikiwe mambo yako na uishi miaka mingi hadi uzeeke utembelee magoti!!

Ahahahahaa.Amen.lakn hadi magoti??! hapo balaa..
Halafu jana mbona ulizima simu?
 
Huyo Kanali ameongoka kama Sauli....kwa hiyo lazima atawashikisha adabu wale ambao hamtaki kusikia.....

Kaka huo mtaji mbona siku hizi utakuwahisha kwenye maisha bora negatively....???

Babu DC!!

Ameongoka lini? si nimeambiwa hadi wakati huu ana watoto hawajaanza hata nursery schoool, sasa hapo kuna usalama kweli?

Huo mtaji ukijua namna ya kuutumia vizuri unapata maisha bora kwenye positive tu. Sasa hivi tunao wachache lakini maisha bora yanasoma kwenye negative, sasa si ni bora kubadilisha figure huenda ikabadilisha matokeo.
 
Hongera sana, Mwita! umepata kijana wa kidigital...hii kumbukumbu yake awekewe. "wa zama za kidigital". inapendeza sana!!
 

Kwa vile nilikimbia yale ma symbol ya calculus na vitu kama hivyo....naomba ninyooshe mikono hata kwenye hizi hisabati zako!!

Mungu awatangulie sana tena...lol!!

Babu DC!!
 
Hongera sana, Mwita! umepata kijana wa kidigital...hii kumbukumbu yake awekewe. "wa zama za kidigital". inapendeza sana!!

Nimewasikia BAKITA leo wanasema kiswahili sanifu ni kidigiti au digiti, kwamba kuita kidigitali au kidijitali ni upotofu.
 
Kwa vile nilikimbia yale ma symbol ya calculus na vitu kama hivyo....naomba ninyooshe mikono hata kwenye hizi hisabati zako!!

Mungu awatangulie sana tena...lol!!

Babu DC!!


Hahahaha mkuu hizi hisabati hazikuhitaji kukumbuka calculus, ni mambo ya "Trai ende era"
Kiongozi we endelea tu kutuombea, mzigo ukiwa mzito tutaomba msaada pale WAMA.
 

kwani wewe haujui zawadi za kisasa? Mi sijui kununulia mtoto wa mtu nguo. Ntajuaje uliagiza uingereza quality stuff? Mambo ya kununulia mtu zawadi anaitupa gereji staki. Nakuja na laptop (najua tu atahitaji kujifunzia), mbuzi ya supu na mzinga wa gongo kwa ajili ya baba. Toooppp!
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…