Rev.Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,553
- Thread starter
-
- #261
Rev Kishoka,
Kuna mengi sana umeandika na kwa kuwa kwa busara zako na cheo chako umeandika ukiwa na mantiki nzuri ILA BILA SHAKA ULISAHAU NENO ZAMA. KWANI SOTE TUNAAMINI KILA MTU NA ZAMA ZaKE.
Ni msingi mkuu kwenu sasa KUCHAGUA VIONGOZI SAHIHI NA SIO VIONGOZI BORA ILI WAFANYE MAAMUZI SAHIHI kwa mustakabali wa kukuza uchumi wenu.
Shukran
Siku zote, nia ya mtoa hoja ni kuleta mahojiano na ubadilishano wa fikra na mawazo. Kama wengi tungelipokea hili kwa chachu na kwa niliyoyanukuu hapo, basi ni wazi ingekuwa ni rahisi sana kwa dhamira yangu kueleweka pamoja na hoja nyingi nilizojengwa kwa umahiri kumkosoa Kikwete.
Ukweli ni kwamba leo tunapoangalia watangaza nia, kampeni chafu ndani ya chama tawala, lundo la tuhuma na uchafu wa kila namna, kwa nini basi tusishukuru "madhaifu" ya Kikwete kutufunulia Watanzania aina ya watu wanaotaka tunu na dhamana ya kuongoza Taifa ilhali si watu wanaofaa?
Ni moaka lini au kwa ishara gani Watanzania tuendelee kuwa wanyonge na wadanganyika wa kauli tamu huku utendaji hakuna na ukweli hawa wote wanataka kutumikia na kuneemesha matumbo yao na whya wafuasi ?
Mkuu tafadhali, hulka ya binadamu hutokana na hisia zake mwenywe na hakuna kitu kibaya duniani kama mtu anayeiga jambo ama anayetaka kuwa kama wengine. Halafu kuna wale ambao kwa sababu walinyimwa sana UHURU wanapoupata huufanyia kufuru ndio maana nchi za wenzetu swala la sex hufundishwa watoto wakingali wadogo kuelewa ubaya wa baadhi ya vitendo ambavyo vilisadikiwa kuwa ni siri kama kulawiti watoto na kadhalika.Rev Kishoka.
Rev unajua mimi na wewe tumetoka mbaaali sana na kwa kuwa humu bado kupata watu makini katika discussion kama ilivyokuwa kule tulikotoka ambako walikuwepo akina Mdosi Mzalendo. Mtukwao etc.
Binafsi naamini wewe ni mtu mzima yaani upo above 40 yrs na angalau uliuona utawala wa Nyerere ambaye ndio muasisi wa Taifa na kila kitu. Hata hao unaouita utitiri wa viongozi kugombea uraisi zaidi ya 86% ni zao la Nyerere ambaye ndie aliewalea na hata kuwatengeneza kimaadili lakin pia hata kuweka misingi ya CCM. Kwa haraka haraka zao la Kikwete katika hao ni Mwigulu Nchemba na January makamba.
Kwa msingi huo uozo wooote huo ni mbegu zilizopandwa na Nyerere leo ndio mnaingia katika mavuno. Kama ilivyokuwa rushwa au ulanguzi. Nchi ya Tgk kabla uhuru kwa maana wakti wa ukoloni hakukuwa na rushwa wala ulanguzi hivyo vyote aliviasisi Nyerere wakt wa utawala wake na leo vimepevuka na kuweza kuitwa UFISADI.
Sasa mimi nafikiri badala kulilaumu tawi turudi kwenye mzizi ambao ni Nyerere. Kikwete itakuwa ni kumuonea tu.
Kumbuka utawala wa Tgk wakt wa Nyerere ulitukuza sana kuogopwa na kila alilotamka Nyrere haikuruhusiwa na chombo chochote kuhojiwa au hata kukijadili alilotaka lilifanyika jambo ambalo leo hii kila anachofanya au kusemwa na Raisi wananchi wanapata fursa kuhoji na hata kuki[inga hadhwarani sababu ku ni UTANDAWAZI.
Ndio maana nikakwambia KILA MTU NA ZAMA ZAKE.Yaani kila kiongozi na wakt wake. Tuyaache hayo tusifukue mengi buree ni bora tu mupeane moyo KUCHAGUA KIONGOZI SAHIHI na wala msianze kulaumiana na kuangalia mapungufu ya viongozi wenu wakuu waliopita. Kwani waislam tunaamini kila mtu ni mkosefu, lakin m'bora wa mkosefu ni yue anayetubia kwa mola wake.
Maaa salaam
Mkuu tafadhali, hulka ya binadamu hutokana na hisia zake mwenywe na hakuna kitu kibaya duniani kama mtu anayeiga jambo ama anayetaka kuwa kama wengine. Halafu kuna wale ambao kwa sababu walinyimwa sana UHURU wanapoupata huufanyia kufuru ndio maana nchi za wenzetu swala la sex hufundishwa watoto wakingali wadogo kuelewa ubaya wa baadhi ya vitendo ambavyo vilisadikiwa kuwa ni siri kama kulawiti watoto na kadhalika.
Zamani maswala kama haya yalifichwa na watoto wengi walifikia kuingia utumwa wa mwili wao kwa kudhani ilikuwa sawa maana hawakufundishwa kuwa lilikuwa jambo baya kushikwa tupu zako na mtu yeyote asokuwa mama yako. Hivyo ndivyo nilivyoitazama Tanzania ya leo na Ujio wa kina Mkapa hadi JK tumeyaona mengi yalotokana na fursa zilizojitokeza. Fursa za ukahaba, ulafi, ufisadi na kila aina ya mabaya yalokuwa wamefichwa chini ya uvungu na wengine waki wish kuwa na maisha haya..
Tatizo linakuja ya kwamba pamoja na Uleberali uliopo viongozi wa leo hawawezi kutubia mabaya yao ikiwa wao wenyewe wanaona haya ndio maisha bora zaidi ya yale yenye Miiko na Maadili maana wanaamini katika UHURU wa kila mtu kuamua jambo hata kama linamdhuru mwingine. Maadili imekuwa siasa na sii mwenendo wa Binaadam yaani UTU wetu umekuwa na gharama zake. Unaweza kununua UTU wa watu kwa fedha na ukaonekana KIONGOZI SAHIHI kwa sababu unawatoa njaa ama kiongozi sahihi kwa sababu una uwezo wa kupigana.
Ipo misingi ya UONGOZI BORA ambayo inaambatana na miiko yake, hivyo maadili yanakuwa sehemu ya Uadilifu ambao kiongozi anatakiwa kufuata misingi ya kijamii ilowekwa. Ebu tazama leo Lowassa ambaye baraza la Mawaziri lilipitisha mradi wa Richmond usipitishwe badala yake wapewe shirika jingine, yeye kwa maamuzi yake akasema wapewe Richmond leo anadiriki kusema hakuhusika na KASHFA ile tena kwa madaha kabisa akidai hizi ni TUHUMA..Kwake uliona ni maamuzi magumu na sahihi japo kwa mabavu na kuvunja miiko ya uongozi bora!
Nchi za wenzetu, kiongozi yeyote unapoingia katika KASHFA yoyote ile inakuondoa sii Uwaziri pekee hata Ubunge, ujumbe wa kamati kuu na ndio maana ya KUWAJIBIKA. Hivyo hili neno kiongozi sahihi (The right Leader) inategemea na udhuru uliopo maana ukitaka kupigana unamtafuta bouncer, wakati kiongozi bora ni yule atakayefikiria kwanza kwa nini tuende kupigana?