Ni jumapili tulivu ya mwanzo wa mwezi february, mwezi mwekundu, mwezi wa wapendanao. Nikiwa nimeupumzisha mwili uliochoshwa na vurugu za ujana na starehe za jumamosi.
Mara fikra zinarudi miaka kadhaa nyuma na kumkumbuka kipenzi changu "M" , naaaaam! Nilimpenda kweliiii, niliona nimefika mwisho wa kupenda, sikuona sababu za wanaume wanaoangaika na wanawake wa nje (michepuko) huku wakiwa kwenye mahusiano yao, Niliapa kumpenda mbaka mwisho mpenzi wangu "M" .Mapenzi yetu yalifika kwenye peak mpaka kufikia hatua ya kumtambulisha kwa baadhi ya ndugu zangu kwenye familia, kiufupi tulipendana sanaa.
By that time nilikuwa ndio kwanza nimemaliza degree yangu ya kwanza nipo mtaani napambana na maisha huku yeye nikimuacha mwaka mmoja nyuma pale campus, nilihangaika mtaani nikiwa na hopes soon mambo yangu yatakaa vizuri na kuishi ile dream life na mpenzi wangu "M", we both had that kind of lifestyle ya kuspend tukiwa nacho.
The good things about "M" alikuwa muelewa sanaaa, nikiwa na kidogo tulikuwa tunashare, kwenye maisha yetu tuliokaa kwenye mahusiano ya boyfriend/girlfriend hakuwahi kuniomba pesa, hata jero la vocha so ilikuwa jukumu langu kumkumbuka nilipopata vinginevyo hakuweza kuniomba chochote.
Honestly speaking kuna kipindi mtaani mambo yalikuwa yanaenda hovyoo sana ilifika kipindi nakwama mpaka nakosa kabisa hata mlo mmoja wa siku and she was there for me, kiufupi alinipa backup sanaa, "M" hakunitegemea mimi kwa lolote kuanzia kodi ya chumba, mahitaji binafsi mpaka kula yake, binafsi nilijihisi nina deni kubwa kwake, kupambana ili nije siku moja kumtimizia yale aliyostahili.
Well let's make story short, i was far from her, hustle zangu zilikuwa mkoa tofauti na campus so i used to go there kila baada ya muda fulani (kuna muda nilikuwa napitisha mpaka miezi 3) . Baada ya kupiga mishe zangu na kuvuna some amount of money nikisema ngoja nikamsalimie "M", ni kipindi kidogo kilikuwa kimepita.
Baada ya kufika na kukaa gheto (kwa "M" ) kuna hali nikawa siielewi , alikuwa akizungumza na simu wakati mwingi sana usiku na mchana na muda mwingi alikuwa akitoka nje au mbali na mimi, hiyo tabia hakuwa nayo, baada ya kuzungumza nae akasema kuna mtu wa maana sana huwa anazungumza nae na hawezi kuacha calls zake, alinisisitiza sanaa nimuache awe anazungumza na yule mtu then kuna siku atanieleza ukweli.
I was Curious nilimbana sanaa mpaka tukagombana, finally she told me kuwa kuna kipindi alipitia matatizo ya kifamilia, mzee wake alikuwa anaumwa sanaa and he was the only person ambaye alikuwa anamtegemea kwenye mahitaji yake yote kuanzia Tuition fees,mahitaji binafsi, pesa ya chumba (aliwaficha wazazi wake kama amepanga out of campus) na hakuwa na mtu wa kumsaidia zaidi huku akiangalia hali yangu mimi (kwangu pakavu) akaona hata akinambia sitomsaidia chochote (i was broke like hell)
So kuna this Professor alikuwa akimtaka siku nyingi sanaa na alikuwa anamsumbua sana (alishawahi kunambia hii kitu before) so she decided to accept him na alimuhadithia shida zote prof na akawa tayari kumsaidia kwa sharti la kuwa demu wake

basi akakubali kuwa na prof kwa kigezo cha kupima HIV then akawa anatoka na prof kuanzia hapo wakati mimi nipo kwenye harakati zangu,
Alinambia alipanga kunieleza ukweli lakini aliogopa hakujua aanzie wapi, She told me hana hisia hata kidogo na prof na hisia zake zote zipo kwangu, alilia kwa uchungu sanaa huku akiomba nimpe muda mpaka atakapomaliza chuo ili aachane na prof because prof ndio alikuwa sponsor wake anaemuweka mjini and by that time alikuwa amebakisha semester moja na nusu agraduate. Men i was down as ****, hasira ziliisha nikabaki kama fala sijui nifanye nini nilimuonea huruma mpenzi wangu "M" on the other side roho iliniuma kuchapiwa tena na prof ninaemjua

.
Nilikuwa kwenye wakati mgumu sanaa nikashindwa hata nifanye nini nikakubaliana na hali halisi na ombi lake la kuwa na prof, lakini nafsi yangu iliniuma sanaa na kujiona falaa kwa umasikini wangu, niliuchukia umasikini, roho iliniuma zaidi nikifikiria mwanamke wangu akiwa anageuzwa geuzwa kitandani na prof.