Thamani ya Yamoto band

Thamani ya Yamoto band

xfactor

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2014
Posts
1,511
Reaction score
1,290
Saidi fella ni mfanyabiashara Katika tasnia ya Muziki na mafanikio ya hii band kwa asilimia zote yeye ndio kayawezesha. Kwa hili nampa Hongera sana

Kilichonifanya niandike huu uzi ni Tukio ambalo limetokea jana ikiwa ni siku ya kuzaliwa ya kiongozi wa band hiyo Aslay, katika siku hiyo ndugu Fella alitoa zawadi ya gari dogo kwa kijana wake. Sambamba na hili Fella ameshatangazia uma kuwa Nyumba za hawa vijana watakabidhiwa mwezi wa saba na pengine Rais akawa mgeni rasmi. Nimpongeze tena Fella kwa hatua hii nzuri

Ninachojiuliza hapa na kilichopelekea kuandika huu uzi ni Je nini thamani ya mziki wa hawa vijana? Mimi sio mtaalam wa kutathimini mziki ila kitu kimoja ambacho nina uhakika ni kuwa hawa vijana wana kipaji kikubwa chenye thamani zaidi ya hili gari na hizo Nyumba watakazopewa. Najua utajiuliza iweje niseme hivi Wakati hizo Nyumba sijaziona, naongea haya kwa uzoefu wa Fella kwani amekuwa akiwanunulia Nyumba wasanii wake Temba na Chege,

Mara ya mwisho nilimuona Fella akimkabidhi Temba Nyumba aliyomnunulia nje ya mji. Kimsingi ile Nyumba ilikuwa ni ya kawaida sana na ni Nyumba ambayo ilikuwa chakavu kwa kiasi fulani. Thamani ya Temba na Chege Sidhani kama ni sawa na Nyumba ya namna ile. Kutokana na hilo ndio maana naamini hata hawa vijana wa Yamoto nao watapewa Nyumba za ubora wa kawaida ambayo si linganifu na thamani ya vipaji vyao.

Kwanini Fella uwanunulie Au kuwajengea Nyumba wasanii wako? Kwanini usiwape hela zao wafanye yao wewe ubaki kuwasimamia na kuwakumbusha umuhimu wa kufanya maendeleo. Wasanii wako sio Watoto kiasi kwamba washindwe kusimamia ujenzi Au ununuzi wa Nyumba zao. Kitendo hiki cha kuwajengea Au kuwanunulia Nyumba kinaficha Mengi juu ya gharama halisi za manunuzi.

Mbona dimond Nyumba yake hamjamjengea Au kumnunulia? Hili ni swali ambalo nawaachia Yamoto band,Chege na Temba. Ifike mahali msanii awe mwajiri wa manager na sio kinyume chake, ndio maana Diamond anafanikiwa sababu yeye kawaajiri Fela na Babu Tale japo mbele ya Jamii huwa anajishusha ili ionekane kama Hao wawili ni maboss zake

ImageUploadedByJamiiForums1431082725.853233.jpg
 
Hata hivyo anawafanyia kitu kikubwa ambacho wasanii wengi wanakikosa kutoka kwa mameneja wao na bendi zao maana hata kama ni nyumba chakavu wengi hawana na wanatamani hata kupata hayo mapagala chakavu.

Kwa upande mwingine ni aina fulani ya UNYONYAJI,Ila kibongobongo poa tu.
 
Ni Kwel kabisa. xfactor Iyo Gari Sio Hadhi yao kabisaaaa....Na Apo cha msingi ange wakatia chao Wafanye yao wenyewe....
 
Said Fella ni mkurugenzi wa kituo cha mkubwa na wanawe.na hayuko peke yake kuna meneja chambuso,babu tale,mh.temba na diamond platnumz hao wote wana share katika kituo hicho.
wasanii wakituo hicho hambao ni yamoto band wanapewa asilimia ya hela zinazo patikana tokana na kufanya shoo.sasa big deal hapo ni nini?
 
Said Fella ni mkurugenzi wa kituo cha mkubwa na wanawe.na hayuko peke yake kuna meneja chambuso,babu tale,mh.temba na diamond platnumz hao wote wana share katika kituo hicho.
wasanii wakituo hicho hambao ni yamoto band wanapewa asilimia ya hela zinazo patikana tokana na kufanya shoo.sasa big deal hapo ni nini?

Umesoma uzi wote mkuu? Kama hawa vijana wangekuwa wanapewa asilimia ya mapato kama ipasavyo Sidhani kama kungekuwa na sababu ya kuwanunulia gari Au kuwajengea nyumba sababu wangekuwa navyo tayari hivyo vyote
 
sasa kama hujui mameneja wa diamond ndio walimnunulia iyo gari.
 
Kuna msemo unaosema miluzi mingi mingi humpoteza mbwa na hawa madogo wakiwasikiliza watu sana ndipo huanza kupotea hii na maanisha kwamba ckubalian na mleta mada, due to the following
pia wao ni watu wazima kwa nin wasikatae kujengewa hizo nyumba pia kuna meneja gani mwingine ameshawah kufanya hivyo? pnc hiv anacho hata kiwanja? yuko wap jebi aliyekua wanaume toka aondoke japo alianza muda ukilinganisha na hawa madogo? Na faida ya Fella itakua ni ipi sasa kama kila anachopata awape hao wasanii na kituo kitajiendeshaje kama hakuna savings kwa kila wanachopata?
 
Gubu ka demu, wewe hata grfrnd wako umeshndwa mnunulia cm.
Wivu wa kike.
 
Najua Fella na Tale si parfect managers kabisa lakini kwenye hoja yako sioni kilicho sahihi kabisa labda kama unaweza kuniambia thamani ya msanii au kundi tunaweza kuipima vipi?
Hivi kama watu wana jengewa nyumba wanapewa usafiri na bado wanalipwa wanapo piga show hivi unataka wafanyiwe nini zaidi?
Kwangu mimi huku tunako enda ni kuwa wachonganishi!

Kama wewe ungekuwa ni mfatiliaji wa muziki wala usinge uliza kuhusu thamani ya Yamoto band kila mtu anajua Yamoto band ilipo na ilipo toka thamani yake ni kubwa sana! Sasa Yamoto band ni moja ya band tano kama sio tatu bora hapa nchini!

Kitendo cha hii band iliyo anza kimzaa kukubalika na kila mtanzania ni thamani tosha..pia kitendo cha wao kupata show nje na ndani ya nchi ni thamani nyingine...!
Mimi nafikiri tumpongeze sana Fella kwa hili maana amefanya mengi na hili la Yamoto band limeonekana wazi!

Kama swala la pesa lazima tukubaliane ni lazima Fella apate zaidi maana yeye ndio mwekezaji na mwenye kiwanda na haitoshi amekuwa hadi akitunga nyimbo ambazo mnazipenda kutoka kwa hawa vijana!

Mimi swala la kuwajengea nyumba limenifurahisha sana na ametumia busara ya hali ya juu maana wasanii wetu wakipata hela hujisau sana!
 
Gubu ka demu, wewe hata grfrnd wako umeshndwa mnunulia cm.
Wivu wa kike.

Hahahaaaa na Hii nayo pia Ni comment na wazi lako Binafsi kama lilivyo langu Kwenye Huu uzi. Hongera Kwa kucomment
 
Mwanzoni walikuwa wanaitwa 'Mkubwa na wanawe'.

Baada ya smash hit single 'ya moto' ndo wakaanza kujulikana kama Ya moto band.

Ule wimbo wa 'Ya moto' ni mzuri sana.

Mwaka jana haukushinda tuzo yoyote ile.

Mwaka huu je?
 
hivi hilo gari kweli kapewa Aslay?? maana naona akikabidhiwa funguo lakini sijaona kadi ya gari. aliyeona kadi aniambiye imeandikwa jina la nani??
 
Back
Top Bottom