Ninakuelewa mama, ni shughuli asikuambie mtu.Asikuambie mtu kazi za nyumbani baada ya kutoka job yataka moyo. Hao wanaolalamika hautawakuta hata siku moja wakisaidia watoto na homework.
Kwa wiki mbili sasa msadizi kaenda likizo, nina watoto watatu chini ya miaka kumi na ajira juu. Hakuna rangi sioni nasubiri kwa hamu arudi nipumzike kidogo.
Mmmmmh!!!Shemeji unataka hadi niwasifu kwa mapambioo na kunena kwa lugha?
Waulize hopeblessed na Shunie hebu.
Umeongea/umeandika kwa hisia sana.Hapo hapo kuna watoto wawili wa wifi umeambiwa watakaa mpaka wamalize shule, unaona kabisa mkate hautoshi asubuhi, inabidi ukirudi kazini uumue unga wa maandazi na hulali mpaka uyakaange ili watoto wanywe chai.
Kuwa mpole nitakusifia hapa nakupump kwanza..Mmmmmh!!!
Sitaki tena.Kuwa mpole nitakusifia hapa nakupump kwanza..
Wanawake tuna roho ya kipekee sana
Hawa viumbe hawa wanahitaji uvumilivu wa hali ya juu
Kuna vitu vingine vidogo tu mwanaume hawezi kufanya mpaka akuite wewe mwanamke ambae umetingwa na majukumu uje ukifanye
Mungu awabariki wanaume wanaojali wake na familia zao kwakweli
Halafu ujue nimekosea uzi wa kampuni kumbe sio huku bwana.Huyu anaweza kutugombanisha wamiliki, tukajikuta na kampuni tumeisusia.
Sitaki.