Thamani ya mke

Thamani ya mke

Hii story ni nzuri sana na inafundisha ila mara nyingi hata watunzi wengi siku hizi wanaiga makosa yale yale ya bongo movie...haiyumkiniki mtu anamiliki gari ashindwe kuajiri house girl,wanawake wengi hata uwe humjali vipi ila akishajua una uwezo hizo kelele atakozokupigia kwamba mletee msaidizi lazima ufanye.akili yangu inagoma kuelewa hili hapo ningetegemea nione mwanaume mwenye kipato cha kawaida akihusika ila tofauti na hivyo utamu wote unaisha.
 
Inawezekana na mtu asichizi kabisa.
Mia kwa mmoja mkuu na awe mtoto mmoja ila zaidi ya hapo ni uongo,unakuta huyu analia njaa yule kajisaidia anataka kusafishwa huyu anataka mcheze halafu wote wanalia...wanawake tuwaheshimu sana majukumu wanayoyatekeleza kwa familia zetu sio madogo.
 
Frankly speaking Mke anathamani kubwa Sana, basi Tu wanaume tunatamaa.

Na wanawake Wako strong Sana kuliko hata sisi wanaume Ni vile Tu mfumo dume unatulaghai.

Kuna wimbo mmoja wa Lucky Dube nimesahau jina lake ila anasema tunawasifu mashujaa kila siku ila tunawasahau WANAWAKE, kwa maoni yake Ni kwamba Mwanamke ndiyo Shujaa kuliko mashujaa wote dunia.

Wanawake Mnaojielewa Mbarikiwe Sana.
 
Amen
 
Mmmh!
Kuna kipindi nilikaa nyumbani bila msaidizi wa kazi... Mimi ndo nikawa beki tatu... Najikuta kwa siku nna masaa mawili tu kupumzika!
Uamke asubuhi ufanye usafi na kuandaa chai... Hujakaa vizuri uanze fikiria vya kupika mchana... Unamaliza kupika, baada ya kula unaosha vyombo... Unapumzika kidogo na kuanza mishe za kuandaa chakula cha usiku... Mnamaliza kula usiku uoshe vyombo!!! Hapo bado hujafua nguo na shughuli zingine za kwenda sokoni na kutengeneza juice... Na hiyo ni nyumba isiyokua na watoto!!!

Mwanaume wa kawaida hawezi fanya yote hayo...
Ndio maana wakipigaga kelele kuwa working wives ni wavivu huwa nawaangalia tu na kuishia kuhurumia hao wanawake waliobeba hiyo mizigo.
 
Frankly speaking Mke anathamani kubwa Sana, basi Tu wanaume tunatamaa.

Na wanawake Wako strong Sana kuliko hata sisi wanaume Ni vile Tu mfumo dume unatulaghai.

Kuna wimbo mmoja wa Lucky Dube nimesahau jina lake ila anasema tunawasifu mashujaa kila siku ila tunawasahau WANAWAKE, kwa maoni yake Ni kwamba Mwanamke ndiyo Shujaa kuliko mashujaa wote dunia.

Wanawake Mnaojielewa Mbarikiwe Sana.
Ameen
 
Mmmh!
Kuna kipindi nilikaa nyumbani bila msaidizi wa kazi... Mimi ndo nikawa beki tatu... Najikuta kwa siku nna masaa mawili tu kupumzika!
Uamke asubuhi ufanye usafi na kuandaa chai... Hujakaa vizuri uanze fikiria vya kupika mchana... Unamaliza kupika, baada ya kula unaosha vyombo... Unapumzika kidogo na kuanza mishe za kuandaa chakula cha usiku... Mnamaliza kula usiku uoshe vyombo!!! Hapo bado hujafua nguo na shughuli zingine za kwenda sokoni na kutengeneza juice... Na hiyo ni nyumba isiyokua na watoto!!!

Mwanaume wa kawaida hawezi fanya yote hayo...
Na wanaume wengine Wana dhana ya kwamba ukitafuta house girl ni uvivu uzembe. Wanachukulia kirahisi sana yani laiti wangejuaaaaaa mungu anawaona tu na hapo uwe mfanyakazi sasa ndo balaa
Na hata hao wamama wa nyumbani pia they need to rest sometimes nasio kufanya kazi kama punda
 
Huo ni ukweli aisee niliona story moja kwenye TV kuhusu Baba kufanya kazi za mke nyumbani kwa wiki tu. Alishangaa sana ni kwa namna gani mkewe anaweza kumudu kazi zote hizo na pia kwenda kazini kuwajibika.
Na hapo ndipo mnapofahamu kuwa ule mchanganyo wa nyama na kabechi mara nyingi si kwakupenda, ni kwakuwa nyama ilikuwa kidogo mama anafanya maarifa.
 
Back
Top Bottom