Thamani ya Damu ya Lisu

mzee wa kijiwe

JF-Expert Member
Jun 25, 2012
947
684
Wapinzani haswa chadema ndio wanufaika wakubwa wa damu ya Lisu,

Ipo hivi, kabla ya Lisu kumwaga damu yake, wapinzani hawakuwa na thamani kubwa mbele ya soko la ununuzi wa binadamu,

Ikumbukwe kuwa baada ya damu kumwagika, njia pekee iliyotumika kufuta hasira na uelewa wa watu ni manunuzi ya wapinzani, ilibidi wanunuliwe kwa gharama yeyote na hii ilisaidia sana kupooza hasira za wote ambao wangefuatilia jambo hilo,

Biashara hii kwa sasa haina soko tena, awamu ya pili inategemewa kuanza rasmi pale Lisu atakapo kanyaga tena Tanzania, hapo tujiandae maana mbele ya pesa lolote laweza tokea, wasio na bei ghafla wanaweza kupata bei.

Damu ya Lisu ina thamani kubwa sana, bado kuna watu wataishi na kusomesha watoto kupitia damu hiyo,

Wapinzani ndio wanufaika wakubwa

Hongera Lisu kwa kutimiza miaka miwili tangu damu yako imwagike, wengi wanaishi kupitia damu yako
 
Back
Top Bottom