Thadei Ole Mushi na tabaka la elimu linavyoendelea kumdidimiza maskini

Kingjr2

JF-Expert Member
Sep 8, 2018
644
1,271
TUNA TABAKA KUBWA LA ELIMU AMBALO HALIONEKANI

Na Thadei Ole Mushi.

Mwaka 2017 niliandika kuwa Shule bora zote za Serikali wanaosoma huko asilimia 95 ni watoto wa matajiri au wenye unafuu wa kiuchumi. Hapa nazungumzia shule kama Mzumbe,Ilboru, Tabora boys, Tabora girls, Kilakala, na nyinginezo ambazo huitwa vipaji maalumu.

Unajua kwa Nini? Twende sawa...

Ili uingie kusoma pale Ilboru Sec, au Kilakala, au Tabora boys na nyingine zenye sifa hizo lazima Kama ni Form one unaingia lazima uwe umefanya maajabu huku primary kwa maana ya Kupata A zote Tena A za kueleweka. Kama ni Advance unaenda kujiunga nayo lazima huku O level ufanye maajabu ya one ya Saba na si vinginevyo. Kama nadang'anya mtanirekebisha.

Nani mwenye uwezo wa kupata A zote au one ya Saba O Level?

Wanafunzi wengi wanaofikia viwango vya kujiunga na shule hizo kwa kuwa ufaulu wao ni wa juu sana Basi wanaofanikiwa kuvuka hapa na kujiunga na shule hizi Basi Kama hajotea shule zinazoanza na St Basi atakuwa katokea pale Feza, Kemobos, na Nyinginezo ambazo Ada yake inaanzia milioni Moja point five.

Nini linatokea baadaye?

Kwa kuwa Pale mzumbe na shule nyingine za vipaji Maalumu nilizotaja ni Mboni ya Serikali, Basi serikali inawapelekea mahitaji yote muhimu ikiwemo waalimu wazuri na kila hitaji muhimu linalotakiwa kwake kufaulu wanapata.

Kinachokuja kutokea hapa ni Mahitaji haya muhimu bado yanaenda kumkuta mtoto wa tajiri au mwenye hali nzuri kiuchumi ambaye yupo hapa kwa kuwa alisoma shule nzuri huku chini.

Inakuja kuwaje huku juu?

Wakimaliza form Six hawa waliosoma shule hizi za vipaji maalum wanafaulu vizuri sana kwa masomo yote hata yale ya Science.

Bodi ya mkopo wanajitokeza hadharani wanasema waliofaulu masomo ya Science ndio watakaopata kipaumbele kwenye mikopo. Mkopo hapa unamkuta tena yule mtoto wa tajiri huku yule wa maskini ambaye aliona Arts ndio kimbilio lake akakomaa na kiswahili, history, Geo na mengineyo pale shule ya kata anaambiwa arts sio kipaumbele kwa sasa. Angelipata maabara na waalimu bora angelifaulu si angelifaulu huyu?

Mtoto huyu wa maskini anajikongoja hata kwa kuuza mwili wake ili amalize Degree yake ya Ualimu au nyingine yoyote ya michepuo ya arts.

Nini kinachokuja kumpata baada ya vurugu zote za kusoma huku chini?

Anamaliza anasikia wanaotakiwa kuajiriwa ni wale waliosoma science kwanza. Yule mtoto wa mwenye afadhali ya kiuchumi anakutana na ajira tena.

Mwisho unajua tunawaambiaje?

Tukisimama majukwaani tunawaambia wakajiajiri

Natamani kila Mbunge awe na mtoto anayesoma shule ya kata jimboni kwake. Hii iwe Sheria watumishi wote wa Umma watoto wao wasome shule za kawaida Tena maeneo walikozaliwa.

Huenda tukaliona hili gape.... Tuendelee kujipongeza kwa matokeo ya Form Six lakini tuwekeze kwenye utafiti kujua watoto Hawa waliofaulu wametokea shule zipi huku chini.

Ole Mushi.
0712702602.
 
Back
Top Bottom