Companero
Platinum Member
- Jul 12, 2008
- 5,604
- 1,704
Ngoma ni zaidi ya burudani:
Utamaduni wetu wa nyimbo na ngoma nao ulishambuliwa sana na wakoloni japo ulikuwa na umuhimu sana kwa jamii zetu. Kwa mujibu wa Terrence O. Ranger (1969) katika karne ya 19 ilibidi jamii za Kisukuma na Kinyamwezi zianzishe jumuiya za ngoma/nyimbo za siri. Walitumia jumuiya hizi kusaidiana kimaisha. Sehemu ambazo wamishionari waliingia ngoma zilipigwa marufuku miongoni mwa waumini wapya kwa kisingizio kuwa zinapingana na dini ya Kikristo. Kuna ushahidi wa kutosha kuwa wakoloni walipinga utamaduni wa nyimbo na ngoma kwa sababu ulikuwa ukichochea fikra za ukombozi na si kwa sababu tu waliona kuimba na kucheza ngoma ni kutostaarabika. Hii inathibitishwa na historia ya moja ya nyimbo maarufu za kudai uhuru. Kwa mujibu wa Mfuko wa Utamaduni (2007), mwaka 1958 kule Tabora wimbo wa Kinyamwezi ‘Oho Sasi Chabela Mitwe' uliotumiwa wakati wa ukinzani dhidi ya utawala wa Kijerumani uligeuzwa na kuwa"Oh TANU Yajenga Nchi."