TGIF: Yote tisa ngoma ni za Wasukuma, Wangoni na Wamakonde! hamtaki!!

Dah...zinanikumbusha mbali! Maeneo niliyokulia zaidi nilikuwa napenda kwenda kutizama mdundiko na pia ngoma zilizokuwa zikiambatana na kutolewa kwa mwali ("kunemwa").

Sijui ni kwa nini tumezitupa ngoma hizi....tungeziboresha na kwa kutumia teknolojia iliyopo zingeweza kututambulisha zaidi. Napenda nyimbo (au hata tune) za wagogo(hasa sauti na mpangilio wake!).
 
Ngoma za kisuuma Oyeeee
Pamoja na bugobogo, kuna aina zingine kama hizi

Balengi - hii huhusisha watu wenye upeo zaidi(grit thinkers)
ambao nyimbo zao husheheni maudhui mazito, kama unataka kufikisha ujumbe kwa jamii au majiagambo kati ya mahasimu.
Kwa anayeelewa lugha huwa ni nzuri sana, hupendelewa na watu wazima na wazee kwa ujumla.

Bagika, hawa nao huhusisha maudhui na kuchamngasha kidogo hupendelewa na watu wa kati

Bagalu(sukumani hip hop for gangsters) kila aina ya ubabe uo hapo

Bunungure - hii siwezi hata ielezea labda ni pop kama wacko jacko,
Full actions mwanzo mwisho, utaona kila aina ya manjonjo

Bugobogobo, ni kama hiyo hapo juu.
Hii huhusika hata wakai wa ilimo
Si unajua wasukuma hulima kwa ngoma wakiwa wengi(luganda)

Rais atajumuisha mambo ya kadete

Na karibuni Bujora- Mwanza mwezi wa sita kwa ajili ya maonesho hayo.
Huko sherehe kubwa ya mwaka ni Bulabo(sikukuu ya ekaristi takatifu) sababu ndio msimu wa mavuno na watu wamepumzika.
 
afadhali hata umesema kajitahidi...lol

Ngabu kuna mtu mi namuulizia, na naimani wewe lazima ujue alipo...lol!!
mara nyingi huwa nyie wawili mnashutumiwa pamoja...lol!

Nani huyo?

Manake nshafananishwa na watu wengi sana.

Kuna siku moja nilikuwa mall namind bizness zangu kitoto cha takribani miaka mitatu hivi kikanikimbilia huku kikiniita 'daddy daddy'....almanusra nizimie!
 
Nani huyo?

Manake nshafananishwa na watu wengi sana.

Kuna siku moja nilikuwa mall namind bizness zangu kitoto cha takribani miaka mitatu hivi kikanikimbilia huku kikiniita 'daddy daddy'....almanusra nizimie!

hahahahaaaa cha kukuzimisha nini baba wewe badala ungefungua mikono ukajitwalia katoto jamani?

anyway hapa si kufananishwa bana (na wewe sijui unafanana na wangapi?)
yule mwenzio mnayepigaga naye soga za mlimani, ukiacha Companero...lol!!
 
Aisee huko WI hata kuishi sijawahi.

Nashauri urudi ufanye tena utafiti wako lol.

utafiti nilikuambia umeshakamilika, ka-inzi kalitumwa mpaka jijini atlanta huko jimboni jojia na kalifika mpaka kwenye jili la mizuri huko kwa mtakatifu luizi

ps. katika ile group yenu iliyounganisha sinza road na simba road kulikuwa na jamaa fulani white kiasi jina limenitoka, alikuwa na dada bomba sana - hebu nikumbushe
 
Back
Top Bottom