TFDA ichunguzeni dawa ya meno ya whitedent

TFDA ichunguzeni dawa ya meno ya whitedent

Kwa arusha kwetu ztakua znachakachuliwa matejoo haha au ngarenaro
 
Tanzania Foods and Drugs
Authority fanyieni hili kazi achaneni na Carolight. Hata lamba lamba na
maji ya matunda ya mzee wetu hapo mmeyafungia macho wakati mnajua yana
madhara kibao.

well said, uzuri wapaka carolight wanajua athari zake. Na hata zinavyochomwa daily lakini bado wanajua pa kuzipata.
 
Acha kulakula dawa, unadhani uji huo??

Sent from my Nokia Lumia using Tapatalk
 
Hata mimi niliachana na whitedent kitambo sana maana fizi zilianza kutoa damu na meno yakawa "very sensitive" nikitafuna nyama. Nimehamia Colgate herbal naona kuna "improvement" kubwa.
 
niliacha kutumia whitedent kitambo sana, baada ya kuona hakuna kinachofanyika kinywani mwangu na hiyo dawa na meno kuuma bila sababu. Tumia colgate au dawa nyingine yenye uwezo kama au zaidi ya colgate.
 
acheni kutisha watu me hiyo ndio dawa ninayotumia so unanishauri nikatupilie mbali?duuuh na jana tu ndio nimenunua ile kubwa kubwa!!!!!!!!
Yan ni hatari! mm juzi nimezizoa shoprite kibao, inabidi nikirudi nikazichunguze vizuri.
 
Ukweli ni kwamba whitedent haina formular inayotakiwa kutengeneza dawa ya meno. Wanapunguza ilikuongeza profit. Mathara yako na kweli. Wahindi wako kibiashara zaidi sio kukusaidia wewe mtumiaji.

Source: Mfanyakazi wa whitedent. (Asema ukweli)

Na hawataki kufanya uchunguzi, mara nyingi hupeleka sample ambazo ziko kamili na baadae kubadilisha.
Ucheni kutumia, tfda wataenda na pesa watapewa kama si sample ya whitedent original na baadae watatoa fake kwa watumiaji.
Jiathari.

Sent from Samsung Note III using Tapatalk
 
Ukweli hata mimi nikitumia ulimi wote unatoka vidonda. Haifai
 
Mimi nilihamia kwenye colgate looooong time mno. Sasa kuna wanaotumia dawa za kichina eti zina Aloe vera kwa bei ya buku na mswaki unapewa. jamani watanzania tusipokuwa makini itafikia siku wote tunakuwa vibogoyo au tutapata kansa za midomo ili wachina watawale hii nchi kwa raha zao
 
Ile wanaita whitedent herbel unaweza ukala na mkate ina sukari balaa.
Makamee umenifurahisha sana. Ina maana wanywa viroba hawawezi kutumia hiyo dawa maana itawatia kichefuchefu. Ila kitu kikishafika JF na kikipata michango kama hii ndo serikali itaamka. Nashukura sana JF maana bila hapa hii nchi ilikuwa ishauzwa yote ingawa sasa imeuzwa indirect kwa Wachina na Waobama.
 
Whitedent inachubua meno name ilinletea matokeo hayo,bora mtu uache ubahili dawa nzuri sana nazotumia ni sensodyne na forever
 
Mamlaka ya chakula na dawa tunaomba muichunguze dawa ya whitedent, imekua na athari ya kuunguza mdomo,kupasuka na kuufanya mdomo kupoteza test unapo itumia, nadhani kemikali wanayoitumia siyo nzuri kwa kutumia inaathari,

Mkuu umesema kweli kabisa mimi siku ya kwanza nilijua labda chai imenichoma fizi kuja kustuka nikaitupilia mbali,kwanza ukifungua tu chupa yake inachanika kwenye kizibo.
 
Hizo dawa si salama ingawa tunapuuzia,mi pia ilishanitokea nkaacha kutumia,na sasa natumia colgate basi.
sawa kabisa, ndivyo nilivyofanya na mimi. Kwa nini ung'ang'anie kitu unachoona kabisa kuwa kinakuumiza?Inaonekana ni fake hata kama zitatangazwa mara mia kwa siku kwenye station moja
 
Back
Top Bottom