Mi natumia sana hii dawa, kuna kitu nimegundua zipo za aina mbili.
Kwa hii ya HERBAL, sanasana ile kubwa utakuta ina manufactured date in full (yaani ina tarehe,mwezi na mwaka ilipotengenezwa)
ukija expire date utakuta ina tarehe ya mwisho kutumika na mwezi ila mwaka hauonekani, hiyo ujue ni fake.
Hizi ambazo hazina mwaka wa ku-expire zinauzwa sana barabarani kwa wale wanaouza kwenye meza mida ya usiku kw baadhi ya maeneo.
Mara nyingi muhuri wake ni maandishi makubwa ukilinganisha na ile ambayo ni dawa ya kweli.
Nilivopita sehemu nyingi barabarani na kuona zote zinafanana nikaamua kuingia dukani na kuikuta hii ambayo ni nzuri muhuri wake upo clear kabisa unasomeka tarehe,mwezi na mwaka kwa sehemu zote mbili (manufactured date na expire date).
Tuwe makini ndugu zangu ni kweli dawa ya whitedent ipo ambayo ni fake.