TEWUTA yasema TTCL pia iliporwa Chuo cha Posta na Simu

radika

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
20,450
Reaction score
32,291
Dar es Salaam. Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Huduma za Mtandao wa Mawasiliano Tanzania (Tewuta) kimepongeza hatua ya Rais John Magufuli kumtaka Waziri wa Fedha kuanza uchunguzi kubaini ukweli kuhusu ubinafsishwaji wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).

Katibu Mkuu wa Tewuta, Junus Ndaro amesema chama hicho kinatambua fika kuwepo mchezo mchafu uliosababishwa na Watanzania wachache wenye uchu wa fedha wakisaidiana na wawekezaji kupora rasilimali hiyo ya Taifa.

Ndaro amesema leo Alhamisi Desemba 28,2017 kuwa, kwa muda mrefu chama hicho kimekuwa kikitoa malalamiko kuhusu ufisadi huo serikalini lakini hakikusikilizwa.

“Tunampongeza Rais Magufuli kwa kuthubutu kutamka pasipo shaka kuwa taarifa alizonazo zinaonyesha kampuni ya Airtel ni mali ya TTCL, jambo hili tulilipigia kelele kwa muda mrefu,” amesema.

Ndaro amesema mara zote hawakusita kutamka kuwa Celtel ambayo sasa ni Airtel ni mali ya TTCL iliyoporwa pasipo kulipwa chochote.

“Wafanyakazi tunatambua kuwa TTCL haikuporwa Celtel pekee bali ilinyang’anywa pia Chuo cha Posta na Simu hali iliyosababisha tukose mahali pa kupata mafunzo,” amesema Ndaro.

Kutokana na kuanza uchunguzi wa sakata hilo, Ndaro amesema viongozi wa Tewuta wako tayari kutoa kila aina ya ushirikiano kuhakikisha Serikali inashinda na kuirudisha Airtel mikononi mwa TTCL.

“Tuna ushahidi wa kutosha na tuko tayari kutoa ushirikiano kwa Serikali katika hatua zote kuleta haki iliyopotea ya Kampuni ya Simu Tanzania,” amesema.

Chanzo: Mwananchi
 
Hakika hakuna JIWE litakalosalia juu ya JIWE jingine
 
Hawa ni waongo, kwa nini siku zote hawakwenda mahakamani kama wanaushahidi? shame on them
Ungekuwa umewahi kuwa mtumishi wa umma ungejua ni ngumu kiasi gan kuwafungulia mashtaka wakuu wako wa kazi, jpm kwa hili apongezwe.
 
Hakika hakuna JIWE litakalosalia juu ya JIWE jingine
Kwa kutajwa, hakuna litakalosalia....
Ila kwa kuyafanyia kazi almost yote yatasalia juu ya mawe mengine.....
1. Mwenye nyumba sabini yupo wapi? Lakini alitajwa
2. Mwingine si tuliambiwa kuna mtu aliamua kufuta kesi ya kukutwa na "mavazi"...
3. Wale wa NSSF, walikula mishahara ya bure mwaka mzima.. lakini walitajwa
4. Kuna mmoja kule TANESCO Mtwara alitimuliwa "kwenyeTV", lakini yupo mpaka kesho anadunda na kazi
5. Makinikia tumeishia wapi?
6. Mishahara hewa imetupunguzia gharama za mishahara?
7. Vyeti feki vimepunguza gharama za mishahara?
8. Bombadia si bado inashikiliwa? Pamoja na kuambiwa ETI LISU NDO SABABU
9. etc etc
 
Kila sehemu akigusa anajua atamkuta lowasa, kumbe analikuta like jamaa la miraba minne, zee la zama za ukweli na uwazi basi mzee wa mafutashitulesheni anaanguka kifudifudi
 
kumbe anamtafuta lowassa
 
CCM wanatafuta Kiki ya kumalizia mwaka!
Viwanda vimewashinda hata salon ya kiume hawajajenga,
Makinikia pamoja na kum_sacrifice Tindu Lissu wamegonga mwamba,
Bandarini wamefyeta mikia
Madawa ya kulevya uligeuzwa kuwa kitega uchumi cha Makonda...alijipatia BMW brand new ya mtuhumiwa na bado anatesa na akina Wema ambao aliwatuhumu
Wengine wamepandishwa vyeo kwa kumsaidia Makonda kuvuna mamilion ya madawa ya kulevya!
Vyeti fake ndio wameiweka serikali ya CCM mfukoni mwao"dady"hafurukuti kwa mwanaye!
CCM ni usanii mwanzo mwisho!
 
Hawa ni waongo, kwa nini siku zote hawakwenda mahakamani kama wanaushahidi? shame on them
Hawa ni waongo, kwa nini siku zote hawakwenda mahakamani kama wanaushahidi? shame on them
walifungwa midomo na tawala zilizopota wengi waliishia kuwekwa ndani na kupata misukosuko kazini.kwa hili limeanzishwa na mkuu mwenyewe hamna wakuwatisha tena
 
Waliosababisha madudu haya yote ni wanachama wa chama cha mapinduzi yaani ccm na wapo katika chama mpaka sasa hii nchi kila uchafu umefanywa na wanachama wa ccm
 
Back
Top Bottom