Wimbi la kuwateua waandishi wa habari kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi ikiwemo ukuu wa wilaya, mkoa, ubunge, ukurugenzi n.k linazidi kushika kasi tokea awamu ya nne hadi awamu hii ya uongozi.
Tutegemee nini kwa waandishi waliopo au wanaotarajia kuingia katika tasnia hii muhimu ya habari hasa namna ya uandishi, utangazaji na namna ya uripotishaji wao wa habari kupitia vyombo vya habari km vile TV, radio, magazeti na mitandao ya kijamii?
Jamani, hakuna haja ya kukuza mambo pasipo sababu...waandishi wa habari ni watanzania kama ilivyo kwa waliopo kwenye taaluma nyingine...hebu niulize: Teuziza madaktari wa magonjwa ya binadamu kunaashiria nini? Teuzi kwa wasomi wakiwemo madaktari kunaashiria nini? Teuzi kwa wanajeshi kunaashiria nini? Teuzi kwa makada wa CCM kunaashiria nini? Teuzi kwa walioshindwa kwenye uchaguzi kunaashiria nini?.....Teuzi kwa waalimu kunaashiria nini?....