Kleptomaniacs,
Naamini na yawezekana nikawa niko sahihi, 3/4 ya wabunge, Bunge la jamhuri ya Muungano wa TZ wana makazi Dar. Hilo tuliache. Pengine ingawa Kitila Mkumbo ametuomba tuwe na subira na press conference ya Zitto na mwenzake Serukamba, lakini nachelea kusema kuwa, wale ni vijana wa sasa, damu changa, waleta mabadiliko katika majimbo yao. Wakiungana pamoja kuhusu 'common interest' tofauti ya vyama lazima waiweke kando,nawafagilia kwa hili. Kweli kuna wabunge wa kibondo (yeye anakula kuku kwani ni Naibu waziri) na yule wa kasulu(sijui aliko) ambao kwenye majimbo yao suala la umeme labda wananchi wao wanauona umeme wa generators za wafanya biashara, hawa jama wa kibondo na kasulu, wanashughulika na mambo yao na hawana muda wa kuungana na wenzao wa kigoma mjini na kasikazini kudai umeme. Ebu tusubiri matokeo ya press conference then tutasema