Lord Diplock MR
JF-Expert Member
- Mar 16, 2015
- 1,446
- 3,319
* JINAMIZI LA NYUMBA ZA SERIKALI, KUITIA HASARA SERIKALI NA MSI ZATUA CC/NEC...
* NYARAKA MUHIMU NA ZA SIRI ZA MUSSA MAGUFULI, SUNDI MLOMO NA SEKELA MWANDOSYA KUTUMIWA NA WAJUMBE WA CC/NEC KUMALIZA KAZI....
Sasa ni wazi mbio za John Magufuli na Prof, Mwandosya zimefikia kikomo baada ya nyaraka muhimu ya madudu yao kupatikana.... Nyaraka hizo ziko tayari kabisa kutumiwa na wajumbe wa CC pamoja na wajumbe wa NEC (kama watapenya).....
Magufuli kwa miaka kadhaa sasa amekuwa akiandamwa na kashfa kubwa ya kuuza nyumba za serikali kiholela, pamoja na kuuza nyumba hizo, waziri Magufuli alidiriki kumuuzia mdogo wake anayefahamika kwa jina la Mussa Magufuli...
Nyaraka za Mussa Magufuli ambaye ni mdogo wake Magufuli zinaonyesha aliajiriwa kwa masharti ya muda kupitia Kumb. Na. GC: 165/467/01/109 na Wakala wa Majengo Tanzania, idara ya "Bussiness Support"... Huku akiwa mwajiriwa wa masharti ya muda na akiwa na siku 9 tu kazini tokea tarehe 26.09.2004 aliyoajiriwa alipewa nyumba 2, na waziri Magufuli katika plot No. 3034, 3082 kinyume na utaratibu, sheria na makubaliano ya serikali....
Sasa ni nyaraka hizo za FP 280 (Agreement for sale) zimenyakwa na leo zitawasilishwa ndani ya Kamati kuu, ili kuonyesha uovu na madudu yaliyotendwa na Magufuli akiwa waziri wa ujenzi...
"Unajua katika siasa utasikia kashfa nyingi sana, za kweli na uongo, ila tunavyopata nyaraka muhimu kama hizi mtu unajua uanzie wapi kujenga hoja... Na sio kusikia maneno ya mitaani mitaani tu"..... Amesikika mjumbe wa Kamati Kuu akiongea jana usiku...
Pamoja na hilo la Mussa Magufuli pia kuna nyaraka muhimu sana kuhusu Sundi Mlomo ambaye upataji wake nyumba naye ulighubikwa na mashaka zimenaswa na zitatumiwa ipasavyo kuonyesha jinsi gani watu wasio staili walimilikishwa nyumba kinyume na utaratibu.
Nyaraka hizo zenye kurasa zaidi ya 42 nazo zitatumiwa ipasavyo...
Katika nyaraka za awali nilizofanikiwa kuziona ni kwamba Stanley Manongi ambaye alikuwa mtumishi wa NSSF aliomba kuuziwa nyumba iliyopo mtaa wa Ubungo Camp yenye Namba UC/HS 8. Lakini barua ya tarehe 9.07.2005 iliyokuwa ikienda kwa wakala wa majengo ilionyesha waziri huyo alimnyanganya Manongi nyumba hiyo na kumpa msichana huyo (Sundi Malomo) ambaye wakati huo alikuwa ni mwanafunzi wa chuo na sio mwajiriwa wa serikali..
* Prof Mwandosya......
Pamoja na nyaraka hizo nzito za Magufuli kutua kwa wajumbe wa Kamati Kuu na wajumbe wa Halmashauri Kuu, vile vile nyaraka kabambe za Sekela Mwandosya zimenaswa na tayari ziko mikononi kwa wajumbe hao kama uthibitisho wa wazi na usio na chepe ya shaka katika uuzaji wa TTCL dhidi ya MSI....
Pamoja na nyaraka hizo pia kuna ushahidi tosha kabisa jinsi Sekela alivyokuwa analipiwa tuition fee na MSI, na mbaya zaidi katika Bank statement za Sekela zinaonyesha trasaction nyingi zilizokuwa zinaingia, kwa haraka haraka mwaka 2002 tu ziliingizwa zaidi ya dola za Kimarekani elfu 80 kwenye akaunti ya Sekela binti wa Mwandosya.... Na uingizaji wa fedha uliendelea kwa miaka mingine kama kawaida....
NB:.... Nimeambatanisha baadhi ya nyaraka hizo, pamoja na magazeti yalivyoibua madudu haya serikalini kipindi hicho....
Yaani badala ya kuweka nyaraka unatuwekea gazeti la Rai, hili gazeti linatumika kwa ajili ya lowasa na kuwachagua wengine nachukia sana vyombo vinavyonunuliwa!