(TETESI)-MACHAME FAILURE MISSION

Nimewaza kama ni kweli haya yanayosemwa, na kama ni kweli jamaa ana kansa ya tumbo kwa asilimia 70% imetengenezwa na huyo bidada alikua akimlisha sumu taratibu
 
Je km Jane naye alikua na mipango ya kummaliza mumewe? Na angefanikiwa? Watoto wasingepata shida?
Hizo ni implications tu Coca, hazitoshi kufanya maamuzi. Ndio maana nikashauri nilichoshauri kwenye aya ya 3.

Huwezi ukaua tu, shida watu wanaamini ndoa ina stakeholders wawili tu(mume na mke), kumbe wapo wengi, mpaka serikali. Kwahiyo ukiwa unafikiria maamuzi magumu, fikiria juu ya hao wote.
 
Hati huwa haibadilishwi kienyeji, kama hati ilibadilishwa na ilikuwa na jina la mmewe lazima mwanaume angeshirikishwa.
Wanaojua ukweli ni hao wawili tu.
Hapana usinidanganye kabisa kuhusu hilo Hati inabadilishwa kirahisi kabisa nishashuhudia hilo mzee mmoja analizwa na mkewe kama masihara tu
 
Kuna vitu bado havieleweki kwenye hii story
Watu wanaendeshwa na mhemko kwenye hii issue.Kama ni kurithi bado mke au mume wote walikuwa na advantage 100% kisheria.

Hata watoto kama ingetokea wazazi wote wametangulia bado walikuwa na advantage 100% kisheria kwenye urithi.

Kuna siri nyuma ya pazia hatuijui kwenye haya mauaji coz kwa sasa mke, mume au watoto kudhulumiwa mali ni ngumu na siyo rahisi.

Unakuta mtu ana shahada halafu anashindwa kuhoji kuhusu mtiririko plus mchakato wa kubadilisha hati ukoje huku mwanandoa mmoja akiwa hai.Kaulizie hapo ardhi uone ugumu wake.

Nb: Tujifunze kutumia akili zetu hata kama ni za kuvukia barabara kuliko hii ya bendera fuata upepo.
 
Em nisanue na serikali inahusika vipi? Niko kujifunza mdogo angu.
 
Mungu sazingine hutoa funzo kwa njia nyingi, hilo ni funzo kwa waliobaki! Kwani km issue ni kuwa mwanaume ana kansa ya utumbo na kwamba angeweza kufa si mali ingebaki ya kwao yeye na watoto wake? Halafu suala la kufikiria mwenzako atatangulia kufa iko nje ya uwezo watu, unaweza ukafa kwa ajali wakati wowote ukamwacha huyo anayeumwa!
 
Kuhusu wanawake wa huko tumeshaongea sana humu jamvini.
 
Je km Jane naye alikua na mipango ya kummaliza mumewe? Na angefanikiwa? Watoto wasingepata shida?
Bwana Kweka alimuwahi tu BI. Urassa ila huenda Jane angemtanguliza, kama move yake kweli ilikuwa hiyo manake kumuua ilikuwa moja ya mipango yake.
 
💯 Kuna mambo hayamake sense kabisa.
 
Bwana Kweka alimuwahi tu BI. Urassa ila huenda Jane angemtanguliza, kama move yake kweli ilikuwa hiyo manake kumuua ilikuwa moja ya mipango yake.
Kwenye hili napenda kusikiliza sana watu nione ufahamu wao, kulingana na maelezo ya dada wa Jane, ni wazi hawa walikua wanaliana timing, atakayewahi kabutua.

Matokeo yake Kweka kabutua.
 
Kuna tumbili zilinishanbulia humu, ndugu zangu nyie ni watu wazima unavadilishaje jina la hati bila idhini ya mume kwanini asinge mshawishi jamaa aridhie mwenyewe? Nyie mna shida sana na nimegundua humu wengi watoto hawawajui wanawake baba yangu mwenyewe Alisha wahi kuwa muhanga wa hayo mambo nilicho kiongea humu nakujua nje ndani nimekiishi
 
Hali ni mbaya sana wanaume wenzangu,shetani amewashika wanawake kwa mikono yote na ndiye anayewafanya wawe hivyo,tuishi na hawa watu kwa akili sana,wanawake wa sasa kwenye pesa huwaelezi kitu hawana huruma na wanaume kabisa kwenye hilo jambo,ndoa nyingi sana zinapumulia mashine kwa hii hali,upendo umekwisha inabakia tu mnaishi kama mtu na dada yake ndani ya nyumba...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…