Tetemeko la ardhi limepita hapa Arusha

Tetemeko la ardhi limepita hapa Arusha

blaza hiyo kitu imetokea lushoto kama dk 15 zilizo pita nilikua nime kaa kwenye kochi nashangaa mtetemo nyumba nzima ila ni kwa kiwango kidogo mnooo!

Arusha limepita kwa kiwango kikubwa mkuu!! Sababu limetikisa kila kitu ndani.
 
Leo siendi bar nasubiri harambee ya CHADEMA live ITV.
Salary nenda kule siasani kuna uzi nimeuweka baada ya kupata fununu za hujuma wa harambee ila kuna vilaza wanatoa povu
 
Last edited by a moderator:
Hapa Dodoma limepita tetemeko dogo la ardhi muda huu na kusababisha watu kukimbilia nje ya nyumba zao kwa hofu.

Hapa napokaa tumetikiswa kidogo na hamna athari kwani ni tetemeko dogo tu.

Aisee mimi mwenyewe nimekimbia nje fasta
 
Mimi nimesikia mtetemeko kwenye kochi nililokalia nikafikiri ni panya anapita
blaza hiyo kitu imetokea lushoto kama dk 15 zilizo pita nilikua nime kaa kwenye kochi nashangaa mtetemo nyumba nzima ila ni kwa kiwango kidogo mnooo!
 
Rais Blaise Compaore wa Burkina Faso amesema atasalia madarakani kwa kipindi cha mpito baada ya miezi 12 ya serikali ya mpito.

Ameyasema hayo wakati akilihutubia taifa siku moja baada ya kutokea machafuko. Wakati ambao pia Mkuu wa Majeshi wa nchi hiyo ametangaza kuivunja serikali ya nchi hiyo.

Katika hotuba yake aliyoitoa kupitia kituo binafsi cha Televisheni, Rais Compaore amesema ameuelewa ujumbe uliotolewa na waandamanaji na kwamba ataondoka madarakani baada ya kumalizika kwa kipindi cha mpito cha miezi miezi kumi na mbili.

Wapinzani na waandamanaji nchini humo, waliandamana na kufanya vurugu kupinga kubadilishwa kwa katiba itakayomwongezea muda wa utawala Rais wa nchi hiyo Blaise Compaore, baada ya kuongoza nchi hiyo kwa miaka 27.

Wamemtaka rais huyo kujiuzulu mara moja.Amiri jeshi mkuu wa jeshi la Burkina Faso Jenerali Honore Traore ametangaza kuvunjwa kwa serikali na bunge la taifa.

Jenerali Traore hata hivyo hakutangaza ni nani atakayechukua uongozi wa taifa hilo.
Jenerali Traore aliwaambia waandishi wa habari kuwa kutaundwa serikali ya mpito baada ya kufanyika mazungumzo baina ya wanasiasa wa upinzani na kiongozi Bwana Campaore.

Jenerali Traore alikuwa akiwahutubia waandishi wa habari baada ya kushuhudia fuzo la maandamano katika mji mkuu wa Ouagadougou.Waandamanaji walivamia majengo ya bunge na majumba ya wafuasi wa rais Blaise Compaore wakipinga azimio lake la kutaka kubadilisha katiba ya taifa ilikumruhusu kuwania kipindi kingine cha uongozi baada ya kutawala kwa zaidi ya miaka 27.

Awali Waandamanaji waliteketeza majengo ya Bunge mjini Ougadougou, na kuwafurusha wabunge .

Runinga ya taifa ililazimika kusitisha matangazo baada ya waandamanaji kuvamia shirika la utangazaji.
Waandamanaji kisha wameelekea Ikulu ya Rais na wanajeshi wamekua wakiwafyatulia risasi.

Vilevile baraza la jiji pamoja na makao makuu ya chama tawala yameteketezwa moto.

Umati mkubwa wa watu umeonekana ukielekea ikulu ya Rais huku uwanja wa ndege ukifungwa.
Rais Blaise Compaore ameomba utulivu ,katika ujume aliotumwa kwa Twitter.

Wabunge wamelazimika kuahirisha kura hiyo ya kubadilisha katiba kumkubalia Compaore kuwania tena Urais mwaka ujao.Watu watano wameuawa katika maandamanao hayo ambayo yametajwa kuwa mabaya zaidi kukumba utawala wa Blaise Compaore.

Awali wanajeshi waliwafyatulia risasi waandamanaji waliovamia majengo ya bunge.
Compaore alitwaa madaraka kupitia mapinduzi mwaka wa 1987.

Amekua akishinda uchaguzi lakini kura hio hukumbwa na utata.
Ufaransa na muungano wa Ulaya zimemuomba Rais Compaore kutobadilisha katiba ili kuwania tena.

4.jpg

3.jpg
2.jpg
 

Attachments

  • 1.jpg
    1.jpg
    42.9 KB · Views: 246
Nilikua ndani ya kivuko cha mv magogoni tunavuka nimelisikia,
 
Back
Top Bottom