Tetemeko la Ardhi Bukoba: Rais aahirisha kwenda Zambia, kuwakilishwa na Makamu wa Rais

Kikwete alikuwa anawajengea nyumba wahanga pa1 na kuwapa pesa na chakula, sasa kwa jamaa tungoje kaulizi za vitisho mikwara kuwaita wahanga kuwa wazembe
 
Sasa akifika huko naomba aweke hekima nabusara mbele. Asiwaambie kuwa wamejenga vinyumba vya ajabu ajabu ndo maana wamekumbwa na maafa. Au asiseme kuwa wamejenga maeneo hatarishi ndo maana wamekumbwa na maafa.

Aelewe kuwa wale bado wako kwenye msiba na hofu na wanachohitaji ni faraja ambapo mambo kama haya yanapotokea faraja kuu hutoka kwa rais... Chondechonde na mada atakayozungumza huko, ajikite kwanye kusaidia tukio huku busara na hekima zikimuongoza. Asiende tena kuongea sijui mambo ya barabara za mwendo kasi Dar wakati yupo Kagera kwenye msiba. Asiongelee mambo ya Mbowe na NHC au mambo sijui ya kuhamia Dodoma.
 
magufuli-620x400-620x375@2x.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameahirisha ziara yake* ya siku tatu Nchini Zambia* ambapo pamoja na mambo mengine ilikuwa ahudhurie Sherehe* za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu, ili aweze kushughulikia tatizo laTetemeko la ardhi lililosababisha vifo vya watu 16, mamia wakiwa wamejeruhiwa na nyumba kadhaa* zimebomoka Mkoania Kagera

Kufuatia kuahirishwa kwa ziara hiyo Mheshimiwa Rais Dkt.Magufuli amemtuma Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Kumuwakilisha katika Sherehe hizo za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu

Sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu zinatarajiwa kufanyika kesho tarehe 13 Septemba, 2016 katika jiji la Lusaka

Jaffar Haniu
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi
Dar es salaam
 
View attachment 398470

kila mtu anajua .

swissme
 
Hongera mheshimiwa Rais..unajali wananchi wako..mungu awape afya njema waliokumbwa na tetemeko.
 
Tungemshangaa kwenda Zambia sio kutokwenda Zambia raia zako wako kwenye majanga wewe unasepa zako bora kashauriwa vizuri kwa Mara ya kwanza
 
Kuna kitu hakiko sawa kabisa hapa. Maafa ya kutisha yametokea tarehe 10. Tarehe 11 zinatoka nyaraka mbili; moja inasema ataenda sherehen uko zambia ya pili inasema hataenda kahairisha. Mmh!!! Haya bana. Mi chichemi.
 
Ni afadhali ashughulikie suala la waathirika wa tetemeko la ardhi kwa sababu lugha kuu ya mawasiliano pale Zambia ni Kiingereza.
 
Back
Top Bottom