sielewi kwa nini watu wanakupa pole!! wewe ni shujaa. Hongera sana mkuu Pave kwa kuwa muwazi. Mungu akupe hitajio lako. mzae na watoto.
Unahitaji pongezi, wote wanamudu ujasiri wa namna hii. Hongera mkuu umekuwa wa kipekee katika hili. Mungu akusaidie upate hitaji lako na zaidi akupe ujasiri zaidi!
Mungu akupe haja ya moyo wako Na kukupa Nguvu . Amen .
Mungu akupe haja ya moyo wako Na kukupa Nguvu . Amen .
umepotea sana!
Mnajuana???
Umenikumbusha jamani kuna pakashume mmoja nlimsave soul mate!
Pole saana! Njoo kanisani hapa kuna watu wanapona HIV mkuu.
Unaweza kushinda hili. Trust me sir.
Regards,
Humble african.
Paka shume tena:what:....from soul mate to Paka shume jamani..
Pole Dada yangu najua ali ku disappoint sana mpaka wamwita Paka shume toka soulmate Kwel....
Mimi mbona sipati wa kuniita hivyo jamani at least na mimi nijione nimo kwa wanaopendwa....Duuh mi ndio mpendaji tuuu....
Kama ni kweli basi naamini nami itakuwa hivyo, nitakuja
Unauliza makofi kwenye kituo cha polisi
Amepotea vipi kwa ile comment yake?
Umenikumbusha jamani kuna mtu mmoja nlimsave soul mate!
utani mwingine bana!
Lakini uwe mwangalifu sana usije ukatapeliwa. Maana makanisa mengi wanatafuta watoa sadaka. Wanaweza kukufilisi kwa kutake advantage ya tatizo lako na baadae kukuacha katika hali mbaya zaidi. Uwe na taadhari kubwa na utumie akili zako vyema.
Najaribu kujiweka kwenye viatu vyako, kwa kweli wewe ni jasiri. Kila kitu hutokea kwa makusudi maalum. Mungu aendelee kukuimarisha na akupatie haja ya moyo wako. Pole sn
Mungu akuongoze mkuu.
Nimekutwa na HIV mwezi wa 11, 2014. Yawezekana nimepata maambukizi katika kipindi kinachoanzia mwezi wa 8, 2014. Nimeogopa na kujitahidi kulinda afya yangu siku zote lakini imeshakuwa hivi.
Sijui imekuwaje nawaza sikustahili hali hii lakini ndio imekuwa. Sijafikiria kuwaambia ndugu au rafiki wa karibu kwa kuogopa kuwaumiza kimawazo zaidi yangu. Kwa sasa nahitaji kukamilisha sehemu ya maisha yangu, kwa kupata mwenza.
Mwenye sifa zifuatazo:
- Muislamu au awe tayari kuwa muislamu.
- Asiwe mtoto, na asiwe anakaribia miaka 40.
- Awe na afya njema , na haijalishi kama ameanza kutumia dawa.
- Awe tayari kuolewa (akinipenda) na kupata watoto.
- Awe anajituma na asiwe na tabia ya uvivu iliyokithiri.
Baadhi ya wasifu wangu:
- Sina mtoto na sijawahi kuoa.
- Ninakazi na elimu ni shahada.
- Ninajitegemea katika maisha ya kawaida, ni msaada kwa baadhi ya ndugu zangu na, ni mchapa kazi na mpenda maendeleo.
- Nina miaka 35, lakini watu huniona nina umri mdogo zaidi.
- Umbo la wastani, urefu ni kama sentimeta 165 (55), rangi ni nyeusi kiasi.