Test Your Earliest Memory: How Long Can You Remember?!.

Kweli disc imejaa; hivi ni Anna Kilala au Jane Kilala 🤣
Could be Jane, maana ni miaka mingi, jina la Robert na bike ndio kumbukumbu yangu. If you know them please let me know.
P
 
"Angalia sana hawa watoto " really very sorry mkuu ,tecnivally huwa kuna viashiria vya wapendwa wetu kututoka sema sa ngumu notice hadi litokee ndo unaunganisha dots
 
Very funny
 
miaka mitatu, nachokumbuka ni kuna dada wa kazi alikua akikaa chumba cha pili kutoka tulipokuwa tuna kaa alikunywa sumu, nakumbuka neno la kwanza kujua kusoma nilikua na miaka mitatu pia lilikua 'takataka' mama alifurahi sana baada ya kulisoma.
.
.
nakumbuka pia niliwahi kumwandikia baba barua nikiwa na miaka minne, alimwagiza kijana mmoja nyumbani kufuata markerpen nikamwandikia barua ya kumpa pole na kazi, na kumwambia siioni je ameiweka wapi? baba alifurahi sana na kumwambia mama ninywe nae chai ya maziwa.
.
.
nakumbuka majina ya niliosoma nao vidudu mpaka chuo kikuu, mpaka na space zao, naona bado kuna space, sema kwa sasa hua nikiwaza kidogo tuu kichwa kinauma sana, hapa tuu nimemeza vivian
 
Sijawahi kusahau matukio muhimu toka nikiwa na miaka minne, hadi Sasa nakumbuka hadi nafasi ambazo marafiki zangu walkua wakikaa darasani,hadi majina ya walimu drs la pili still nakumbuka hadi nguo zao pendwa walimu wangu walzokua wakivaa toka la pili nakumbuka vitu vingi sana hadi najiogopa mfano Kama Safari za likizo za kwenda kijijini kwa babu nyingi nazkumbuka Tena toka nina miaka minne hadi barabara tulyokua tunasafaria nayo kpind npo dogodogo naikumbuka jinsi ilivyo Yani Nina kumbukumbu za kutosha ila kinachonishangaza zaidi ni kwamba nasahau sana tarehe au vitu vinavyohusiana na kukumbuka single dijit mf 1,2,3,4 nk pia kinachoshangaza pia ni pale ninapojaribu kusoma kitu flani ubongo unakataa kuhifadhi kabisa lakini ikipita siku moja najikuta kitu kilichokataa kukaa kichwani nakikumbuka ila ni baada ya siku moja...vitu ni vingi.
 
😂😂😂 umenikumbusha kipindi niko vidudu nilikua sijui kuandika jina langu aisee.
Siku iyo ticha akasema kila mtu aandike jina lake nachokumbuka nilikua naangalia kwa binti fulani, ila napo sikufanikiwa japo niliona alichoandika. Kuumba herufi kama vile ikawa mtihani mwingine kwangu😂.

Bahati ikawa kwangu mwalimu hakukagua wala nini, nakumbuka pia kuna chalii alinimwagia uji wake aisee sema mambo mabaya mabaya ndo nakumbuka mazuri hata siyakumbuki.
 
hahaa eti ka unataka kuerase kaginge na gari............
umenikumbusha jirani yangu alipata ajali ya pikipiki sa hivi memory zote zimefutika
kaanza upya tena hata mkewe alikuwa hamtambui imagine mtoto wake ndio kaanza tena
kumfundisha a,e,i,o,u
kumbe haya mambo ya kupoteza kumbukumbu yapo, duh!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…