Terminal ya Clouds FM wanapiga kampeni michango ya Harusi.

Terminal ya Clouds FM wanapiga kampeni michango ya Harusi.

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2017
Posts
6,704
Reaction score
7,409
Halo JF.
Nipo hapa Nyumbani nasikiliza Terminal ya clouds FM radio ya jiji la karaha na raha la Dar.

Wanaonekana kupinga michango ya harusi wakidai sio lazima. Wote Haris Kapiga na Lilian Mwasha na mgeni mwalika wanasema eti nichango ya harusi sio lazima na inabidi ihusishe ndugu tu kama wafanyavyo wenzetu Rwanda na Kenya na pia Uganda.

Sasa najiuliza hivi Harris na Lilian siku wakioa au kuolewa hawakuchangiwa. Wameenda mbali kwa kusema Tanzania ni nchi ya kishamba mtu kusumbua michango hata kwa watu wasio nduguze.

Hiki ni kipindi cha hovyo kabisa clouds FM kwani kila nchi na utamaduni wake. Ikumbukwe pia ujamaa wa MWL Nyerere ulihimiza undugu na kushirikiana na pia kusaidiana kwa hali na Mali.

NB: Mods naomba mada isome wanapiga kampeni dhidi ya michango ya harusi.
 
Michango ya sherehe ni kero sana, ila kama wakati wanaoa na kuolewa walichangisha watu acha na wao wachangie tu.
 
Soon tutaongea lugha moja, ambao bado hamjaoa/hamjaolewa mjipange maana hatutoi michango ng'o labda kwa ndugu wa karibu 😀😀
 
Kweli kuchangia harusi ya mtu ambaye sio wa karibu kabisa ni ushamba. Unachangia laki unapata kinywaji kimoja maana gharama nyingi za ziada (kukodisha magari ya ajabu ajabu, farasi, n.k.) zinapunguza bajeti za vyakula na vinywaji. Tena mara nyingi "wenyeviti wa idara" (k.m. chakula, upambaji n.k.) wanapata "cha juu" kwa kumleta mhusika anayetoza gharama kubwa kuliko inavyostahili. Nimewahi kuona harusi ambazo kamati ya maandalizi imeweka "sherehe ya kujipongeza" kwa sababu michango ilibaki. Yaani badala ya kuwapa maharusi hiyo baki iwasaidie kwenye kodi ya pango au kwenye ujenzi kama tayari wana kiwanja, kamati inazila hizo fedha. Halafu mwisho wa siku baada ya harusi ya kifahari sa-a-na ndoa inavunjika (wakati mwingine hata mwaka haujaisha). Napendekeza muoaji aite tu marafiki wa karibu, wajomba, mashangazi, na wazazi na ndugu upande wa mume na mke. Jumla ya watu isizidi 50. Na gharama isizidi milioni nne. Mradi picha na video ziwepo basi. Kama gharama ni ndogo hapatakuwepo haja ya kuomba michango mingi. Siku hizi unaweza kujikuta una kadi nne au tano zinataka michango kila mwezi. Na ukimchangia mtu elfu 20 anakudharau. Si afadhali kuacha kuchangia kuliko kutoa pesa kibao kila mwezi kuchangia harusi? Mwisho kabisa:- Kwenye mila za makabila mengi ni watu wa ukoo tu ndio walikuwa wanachanga, na kwenye makabila mengi michango ilikuwa ni vitu vya kusaidia maharusi katika maisha yao yajayo (yaani fenicha na vyombo vya ndani) na sio pesa za kwenda kula na kunywa.
 
Soon tutaongea lugha moja, ambao bado hamjaoa/hamjaolewa mjipange maana hatutoi michango ng'o labda kwa ndugu wa karibu 😀😀
Kama ulichangiwa, wewe pia wachangie waombaji
 
Kama ulichangiwa, wewe pia wachangie waombaji
Nitakacho angalia ni ukaribu wangu na huyo mtu baas na pia sio lazima ndo imetoka hiyo. Mtu unatakiwa kuchanga harusi 3 kwa mwezi hiyo pesa natoa wapi? Halafu huku kwetu eti mtu anabariki/kipaimara au ubatizo wa mtoto anakuchangisha..hawa nawatoaga mbio bila aibu.
 
Nitakacho angalia ni ukaribu wangu na huyo mtu baas na pia sio lazima ndo imetoka hiyo. Mtu unatakiwa kuchanga harusi 3 kwa mwezi hiyo pesa natoa wapi? Halafu huku kwetu eti mtu anabariki/kipaimara au ubatizo wa mtoto anakuchangisha..hawa nawatoaga mbio bila aibu.
Watu wanachangisha Hadi sherehe ya birthday Yake au ya mtoto unashangaa Nini?
 
Watu wanachangisha Hadi sherehe ya birthday Yake au ya mtoto unashangaa Nini?
Mtu mwenye akili timamu hawezi changia birthday. Na ukute mwenye birthday ni lijitu lizima
 
Nitachanga kama tu ni mtu wangu wa karibu sana. Nimeshapotezea kadi zaidi ya 50 sasa, nimeshasema sijipi headache tena
Wachaga hawawezi kukuelewa kwao kuchangia Sio swala la hiari ni la lazima utake usitake.Unakuta mwenyekiti anafoka kuwa kima Cha chini hiki hapa utatoa wapi utaiba u utatoa wapi utajijua lazima utoe
 
Back
Top Bottom