Masanja
JF-Expert Member
- Aug 1, 2007
- 5,282
- 10,304
Waungwana katika pita pita yangu, nimekutana na hiki Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji University kilichoko Mbeya. I dont know much about it. Mweye details atupe. But naona hakijapata usajili kamilifu ingawa kinaendelea na juhudi za kutoa elimu. Hakika ukiangalia by all standards ni kwamba kina mapungufu mengi. LAKINI je watanzania tufanye nini kusaidia vyuo kama hivi? ambavyo si tuu vina upungufu wa elimu, lakini pia hata uwezo wa kuattract wanafunzi makini unakuwa haupo. Kipi kifanyike? NAJUA wote tuna kiu ya kusaidia elimu hapa nyumbani. Ni vema juhudi kama hizi tusizibeze bali tuwape mawazo ni namna gani wanaweza wakawa nyenzo bora mbadala ya kupigana na umaskini.
By the way kwa mlio nje na mna elimu zenu, naamini huu ndo mwanya muafaka wa kuchangia maendeleo ya taifa letu kwa kussuport by any means, kama kuja kufundisha, kuwalink na universities huko nje, Kuwasaidia na exchange programme kama zipo nk. Nimefarijika kuona Prof. Mbonile wa UD kaenda kufundisha pale, sijui kwa nini, lakini naamini vyuo kama hivi vitafaidika na utalaamu wa wasomi kama hawa.
Link yake ni hii: http://teku.ac.tz/index.php?option=com_frontpage&Itemid=1
Tuwasaidie, tusiwabeze.