Tendwa Unasubiri nini kukifuta Chama Cha CUF?

Kakende

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2012
Posts
2,741
Reaction score
1,233
Lipumba akiwa kwenye nyumba ya ibada alidhibitisha kuwa mwaka 1995 aliombwa agombee Urais ili kuwakilisha watu wa Imani yake. Pia Mwaka 2010 Yeye na viongozi wa dini yake walizunguka nchi nzima ili kumuokoa Kikwete dhidi ya mziki mzito wa CHADEMA. Pia Amewataka watu wa dini yake wajipange mwaka 2015 ili waokoe jahazi kupitia CUF.

Sasa kwa MANENO KAMA HAYO YA LIPUMBA ni wazi kwamba CUF ilianzishwa maksudi kwa ajili ya watu wa imani fulani. CUF ni sawa na Chui alievaa ngozi ya Kondoo. Mimi niliwahi kuvutiwa na Sera za LIPUMBA wakati fulani.

Kwa ushahidi wa wazi kama huo, TENDWA UNASUBIRI NINI KUFUTA CHAMA HIKI HATARI AMBACHO HAKIWAKILISHI WATANZANIA WA IMANI ZOTE?
 
Angekifuta kwanza chadema kwa kusigina katiba yake,kumlazimisha zitto kabwe kujitoa kwenye kinyan'ganyiro cha uwenyekiti.live watanzania wote waliona.maana ya cdm ni chama demokrasia na maendeleo.swala la lipumba si la kweli ni la kuungaunga.
 
Hapo kwenye RED, hiyo ndiyo tunaita kutapatapa. In short Mwenyekiti wenu LIPUMBA siku ile aliizika CUF, sijui hakujua kama kuna VIDEO SHOOTING?, Maskini Liprofeserriiiiiii wa UCHUMIDINI
 
Angekifuta kwanza chadema kwa kusigina katiba yake,kumlazimisha zitto kabwe kujitoa kwenye kinyan'ganyiro cha uwenyekiti.live watanzania wote waliona.maana ya cdm ni chama demokrasia na maendeleo.swala la lipumba si la kweli ni la kuungaunga.

Zitto akihojiwa anasema CHADEMA hakuna mgogoro, nyie mlioko nje mnalazimisha kuwa Zitto anaonewa, au nyie ndiyo wasemaji wake?
 
Tendwa anacho fanya ni kukenua na kutuonesha mwanya wake, na kula pesa ya wananchi, sioni umaana wowte wa yey kuwa hapo...kuna siku alikuwa anahojiwa, yeye akajibu "unajua tatizo la hivi vyama vya wenzetu shida yao wana taka chama tawala kitoke madarakani..." hopeless!
 
mke anamwezesha mme kula mpaka anashiba halafu mme amwache mke umewahi ona wapi?
 
tendwa kuifutaa CUF ni sawa na wewe kwenda kwa mfale nakumfukuza malkia,CUF ni mke wa CCM ati
 
Chama kina mgombea Urais Padri hicho ndo cha kufutwa kwanza.Waislamu wamekwisha amka sasa hivi endeleeni kuimba mapambio hadi kwenye majukwaa ya siasa mkidhani mtapata kura za kanisani pekee yake zitawafikisha.
 
Tendwa anacho fanya ni kukenua na kutuonesha mwanya wake, na kula pesa ya wananchi, sioni umaana wowte wa yey kuwa hapo...kuna siku alikuwa anahojiwa, yeye akajibu "unajua tatizo la hivi vyama vya wenzetu shida yao wana taka chama tawala kitoke madarakani..." hopeless!

'yeye kazi yake sio kutenda na asipoangalia atatendwa tu...'
 
Weka Ushahidi

Waulize jamaa zako huko sumbawanga mpaka radio yao ilikuwa inapiga Kampeni.kikwete na Aesh washkuru mungu, kwani hujawahi kusikia kuna wakatoliki mpaka leo wamefukuzwa dini?
 
Angeanza kukifuta chadema ambacho kampeni za 2010 zilihamishiwa kanisani.

Hivi mnafikiri Chadema ikipiga kampeni Makanisani mziki wake mtauweza! Kama Mapadre, Maaskofu na wachungaji wote wakiamua kuubili uzuri wa Chadema makanisani nani atasimama? Kwa taarifa yako kuna sehemu hapa nchini serikali ikisema fanya hivi na padre akasema msifanye, watamsikiliza padre kuliko serikali.
 
Vyama vyetu vya upinzani vinasikitisha sana.
CCM iliponazisha mfumo wa vyama vingi ilitegemea vitaudwa vyama vyenye malengo mazuri na taifa, lakini unfortunately ndio vimeibuka CUF na Chadema.
 
Chama kina mgombea Urais Padri hicho ndo cha kufutwa kwanza.Waislamu wamekwisha amka sasa hivi endeleeni kuimba mapambio hadi kwenye majukwaa ya siasa mkidhani mtapata kura za kanisani pekee yake zitawafikisha.

Ndugu yangu usiseme usilolijua. Hapa Tanzania tushukuru Mungu viongozi wa dini ya Kikristu wanauelewa wa juu. Wakiamua kupiga kampeni Makanisani kusupport chama chochote hakuna atakayeweza kukipinga. Unafikiri kama Mapdre wangeamua kupiga kampeni kanisani viongozi kama Kagasheki wangekuwa wabunge?
 
Chama kina mgombea Urais Padri hicho ndo cha kufutwa kwanza.Waislamu wamekwisha amka sasa hivi endeleeni kuimba mapambio hadi kwenye majukwaa ya siasa mkidhani mtapata kura za kanisani pekee yake zitawafikisha.
Mkuu mbona unapaparika kama bisi jikoni!lipumba hasafishiki na dr.slaa sio padri
 
Hivi mnafikiri Chadema ikipiga kampeni Makanisani mziki wake mtauweza! Kama Mapadre, Maaskofu na wachungaji wote wakiamua kuubili uzuri wa Chadema makanisani nani atasimama? Kwa taarifa yako kuna sehemu hapa nchini serikali ikisema fanya hivi na padre akasema msifanye, watamsikiliza padre kuliko serikali.

'kuna waraka flani hivi wa chadema na kanisa kama skosei ni kanisa katoliki mkuu ulienea sana tu hivi ulishawahi kuusoma.............ilikuwa ni kuelekea kipidi cha pili cha kandanda i.e to 2010,uliwahi kuuona'
 
Lipumba akiwa kwenye nyumba ya ibada alidhibitisha kuwa mwaka 1995 aliombwa agombee Urais ili kuwakilisha watu wa Imani yake. Pia Mwaka 2010 Yeye na viongozi wa dini yake walizunguka nchi nzima ili kumuokoa Kikwete dhidi ya mziki mzito wa CHADEMA. Pia Amewataka watu wa dini yake wajipange mwaka 2015 ili waokoe jahazi kupitia CUF.

Sasa kwa MANENO KAMA HAYO YA LIPUMBA ni wazi kwamba CUF ilianzishwa maksudi kwa ajili ya watu wa imani fulani. CUF ni sawa na Chui alievaa ngozi ya Kondoo. Mimi niliwahi kuvutiwa na Sera za LIPUMBA wakati fulani.

Kwa ushahidi wa wazi kama huo, TENDWA UNASUBIRI NINI KUFUTA CHAMA HIKI HATARI AMBACHO HAKIWAKILISHI WATANZANIA WA IMANI ZOTE?

Anasubiri maelekezo kutoka juu!
 
Back
Top Bottom