Wakili Mashaka Ngole aibwaga ACT Wazalendo Mahakamani, akiwakilisha Chama cha Cuf katika kurudisha jengo la ofisi lililoporwa huko Kilwa.

Wakili Mashaka Ngole aibwaga ACT Wazalendo Mahakamani, akiwakilisha Chama cha Cuf katika kurudisha jengo la ofisi lililoporwa huko Kilwa.

Boveta

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2019
Posts
3,267
Reaction score
3,970
Code:
THE CIVIC UNITED FRONT(CUF- Chama Cha Wananchi-Cuf 

CUF- Chama Cha Wananchi imepata ushindi kwenye Kesi iliyofunguliwa na ACT- Wazalendo ya kudai Ofisi ya CUF Wilaya ya Kilwa kwamba ni mali yao waliyopewa na Seleman Bungara (BWEGE).

Mahakama jana Julai 30,2025 imetupilia madai hayo (Madai Na. 10 ya 2024) na kuthibitisha kwamba Ofisi hiyo ni mali ya CUF- Chama Cha Wananchi kutokana na vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapo na Wakili wake Mashaka Ngole. Mapema mwaka jana ACT -Wazalendo walivamia eneo la CUF- Chama Cha Wananchi na kuanza kujenga na kuandaa tukio la Uzinduzi wa Ujenzi huo haramu lililopangwa kuongozwa na Mhe. Othman Masoud Othman kwa kutumia Mamlaka yake kama Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, mpango ambao ulizimwa vibaya na CUF- Chama Cha Wananchi na kupelekea wavamizi hao kukimbilia mahakamani.

HAKI SAWA NA FURAHA KWA WOTE!


Eng. Mohamed Ngulangwa 
Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma 
CUF- Chama Cha Wananchi 
Julai 30, 2025

HAKI SAWA NA FURAHA KWA WOTE!
 
Back
Top Bottom