Tendwa Atoa Tamko Dhidi ya CHADEMA na CCM

Tendwa Atoa Tamko Dhidi ya CHADEMA na CCM

Sijui hajui kuna hili inaendelea.......maskini tendwa pensheni inamponza

RAGE KUPELEKWA MAHAKAMANI
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime amesema kuwa wanaandaa jalada la kuhusika kwa Mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage kwa ajili ya kuliwasilisha kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).


Kamanda Misime alisema jana kuwa wako mbioni kukamilisha jalada hilo ili walipeleka kwa DPP kwa ajili ya kufikishwa mahakamani."Ni kweli tumepokea malalamiko ya Chadema na tunaandaa malalamiko ili kuwasilisha kwa mwanasheria na Serikali," alisema Misime.


Hayo yamekuja kutokana na vurugu zilizotokea kati ya wafuasi wa Chadema na baadhi ya wabunge wa CCM, akiwamo Rage wakati walipokuwa wakigombea mlingoti wa bendera kitendo kilichosababisha watu watatu kujeruhiwa katika tukio hilo wikiendi iliyopita mjini Dodoma.
Hata hivyo, Rage amekana kuhusika na vurugu hizo akisema anaamini uchunguzi kuhusu tukio hilo utamuweka huru kabla au baada ya kufikishwa mahakamani kwa sababu hakushiriki wala kumpiga mwanaChadema aliyetangaza kumshtaki.


"Sikumpiga. Historia yangu inaonyesha kuwa sijawahi kushiriki vitendo vya vurugu wala mapigano kwa sababu yoyote ile. Mimi siyo mhuni wa kupiga mtu. Nilichofanya ni kumlinda yule kijana asipigwe na wanaCCM waliojaa hasira kwa yeye kuingilia mkutano wetu," alisema Rage, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Simba.


Alisema kada wa Chadema ndiye chanzo cha vurugu hizo zilizoishia kwa kujeruhiwa na wanaCCM baada ya kuvamia eneo la mkutano wa chama hicho.


"Baada ya kuona kitendo hicho, mimi pamoja na Mwenyekiti wa CCM wa Iringa, Deo Sanga, kama viongozi tulimfuata kijana yule na kumsihi asifanye hivyo baada ya kuona vijana wa CCM waliokuwapo eneo lile wanaanza kupandisha jazba ambazo tusingemudu kuzizuia, lakini hakutusikilizwa," alisema.


Rage alisema baada ya kuona kijana huyo anaanza kushambuliwa na wanaCCM ndipo alipolazimika kuingilia kati kuwaamulia na kumkinga asipigwe na mawe na majabali yaliyokuwa yameshikwa na wanaCCM, ambapo kijana huyo alifanikiwa kuchomoka na kukimbia.


Alisema kabla ya vurugu, kundi dogo la wafuasi wa Chadema lilikuwapo eneo la mkutano wakiwa na bendera ya chama hicho bila kufanya vurugu yoyote, ambapo yeye aliwasihi kuwaacha wasikilize sera za chama hicho kwani mkutano ulikuwa wazi kwa wananchi wote bila kujali itikadi za vyama.


Hata hivyo, picha zilizopigwa na kuchapishwa kwenye vyombo vya habari zilimwonyesha Rage na wafuasi wa CCM wengine wakiwa katikati ya vurugu hizo na juzi uongozi wa Chadema Wilaya ya Dodoma ulitangaza kumburuta mahakamani mbunge huyo kwa tuhuma za kujeruhi, kung'oa na kuharibu mali za chama hicho kikuu cha upinzani nchini.


Kauli ya Rage imetokana na kitendo cha uongozi wa Chadema wa Wilaya ya Dodoma kutangaza nia ya kumshtaki baada ya kumpiga kada wao.
Makada wa CCM na Chadema walipigana Jumapili iliyopita wakati wa maadhimisho ya miaka 36 ya CCM mjini Dodoma.


Vurugu hizo zilizuka baada ya wafuasi wa Chadema kukasirishwa na kitendo cha vijana wa CCM kung'oa bendera yao wakati wakiendesha mkutano kwenye eneo la Mwanga Baa mjini Dodoma.
Wafuasi hao wa Chadema walilazimisha kurudisha bendera yao wakati mkutano ukiendelea, ndipo makada wa CCM waliojumuisha wabunge wa Jamhuri ya Muungano walipoamua kuwapiga kwa kuwarushia mawe wafuasi hao na kusababisha kuumia kichwani kwa kada wa Chadema.


Wabunge wa CCM waliokuwa katika tukio hilo ukiacha Rage ni pamoja na Seleman Jafo, Said Mtanda, Mary Chatanda na Nyambari Nyangwine.


Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumzia suala hilo alimtetea Rage, akisema alikuwa akiamua ugomvi huo na kama isingekuwa yeye mauaji yangetokea.
"Hakuhusika yeye alikuwa akiamua ugomvi na kama asingekuwepo mauaji yangetokea," alisema Ndugai.


Katibu wa Wabunge wa CCM, Jenista Mhagama alisema kwamba hajapata taarifa za kuwapo kwa tukio hilo.
 
ukimuunganisha tendwa makinda na ndugai unaona ombwe la kitaifa kwenye taasisi muhimu zinazo shikiliwa na watu wenye mahaba yaliyopindukia kwenye udhaifu wa kiutendaji.
 
we tendwa tulisha kuzoea. unapoona CCM wanahusika katika kuvunja sheria taratibu na kanuni, unaiunganisha na chama kingine ili usonekane na waliokuteua kwamba unawaharibia. Lakin pia,badala ya kulaumu aliyechoma moto unaulumu moto uliowashwa!!! Acha kulalamikia matokeo, bali kilichosababisha. na wito huu nautoa kwa wote wenye fikra mgando na kuwalaumu wabunge wa pande zote(upinzani na ccm), chanzo kikuu ni kiti cha spika kutotenda haki.

Bwana Samuel Sitta aliwahi kusema kuwa aliondolewa kwenye kinyanganyiro cha uspika na mafisadi, na hii inadibitishwa na hali inavyoendelea ndani ya bunge chini ya makinda. makinda ameshindwa kabisa kuendesha vikao vya bunge ama kwa makusudi ama kwa influence ya waliomuweka au kutokimudu kiti na kushindwa kuzitafsiri kanuni za bunge.uamuzi mgumu usipofanyika katika hili sina hakika kama tutafika, na kama tutafika siamini kama tutafika salama.

Nawashauri wabunge wote bila kujaliitikadi zenu kufanya uamuzi sahihi wa kumuondo spika makinda kwa ajili ya kulinda heshima ya bunge na nyie wenyewe wabunge. Bunge linaitwa eti ''bunge letu tukufu''!!!!! nashindwa kuelewa hadi sasa utukufu huo upo? Wabunge mnjiita 'waheshimiwa, mbona hiyo heshima siioni? unshindwa kuelewa hata mawaziri nao ni watu wa hovyo kabisa.

Waziri anasimama anamuita mbunge eti hana akili, unajiuliza huyu ni waziri wa namna gani? Kwa mfano, ukilinganisha wapiga kura waliomchagua waziri nahodha, na waliomchagua machemuri hakuna hata uwiano. waliomchagua vuai ni kama watu wa kata moja kwenye jimbo la machemuri.

H
oja yangu ni kwamba kaulii za matusi na dharau miongoni mwa watu wanaojiita waheshimiwa ni aibu kwao wenyewe na bunge.
 
jk alikuwa anafanya kampeni hadi saa moja na nusu usiku na aliufyata..
 
Tendwa ni KARANI tu hana lolote,,, alikuwa amepotea sana kwenye jamii na sasa kapata jukwaa kutukumbusha kuwa bado yupo...

Mh Tendwa usajili wa CHAUMMA ni lini? Sisi Masalia hatuna pa kutokea 2015 tuwahishie mzee...
 
Kuku wa kuchora! hadonoi, hachakui wala hatagi.....
 
Alipaswa aitwe Teendwa na sio Tendwa! Alilikosea jina lake yeye mweneywe.
 
TendwaMuda%2814%29%281%29.jpg

Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa

Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, amesema amesikitishwa na vurugu zilizotokea katika shughuri za kisiasa mkoani Jumapili iliyopita kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kusema kuwa ni ukiukwaji wa masharti ya usajili wa vyama vya siasa.

Katika taarifa yake jana, Tendwa alisema kifungu namba 9(2)(c) cha sheria ya vyama vya kisiasa ya mwaka 1992 kikisomwa pamoja na kifungu 5 (b)(i) kama kilivyorekebishwa mwaka 2009 kinakataza vurugu, fujo, matumizi ya nguvu na uvunjifu wa amani wa aina yoyote na kuwa ni kosa la jinai linalopaswa kufanyiwa kazi na mamlaka.

Tendwa alisema matukio kama hayo yanatengeneza taswira mbaya ya siasa nchini na kushusha heshima na imani ya wananchi kwa vyama vya siasa.

Alisema ofisi ya msajili inachukua suala hili kwa kuvihusisha vyama husika ili ipate ukweli na undani wake na iweze kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria.

Alisema,ofisi yake inavikumbusha na kuviasa vyama vya siasa kuheshimu sheria za nchi, sheria ya vyama vya siasa na maadili ya vyama vya siasa.

Viongozi na wafuasi wa vyama hivyo walipigana hadharani wakigombea uwanja wa kufanyia mikutano.

CHANZO: NIPASHE

katiba mpya itusaidie kutuondolea watu kama tendwa kwenye nafasi nyeti kama ya msajili wa vyama siyo chama
 
mmh! kwan kwenye siasa huwa kuna kustaafu? c had wafie humo? halafu kwan hlo tamko ni kwa vyama vya sias au ni kwa chadema mbona kwenye fujo walikuwa wote why tamko kipewe chama kimoja?
 
Katika watu vilaza wanaokula pesa za serikali bure huyu naye yumo..sijui kazi yake akishasajili chama anafanya nini...labda facebook...maana sioni, sisikii na wala hainiingii akilini.Sawasawa na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi anayesubiria jimbo liwe wazi au miaka 5 uchaguzi aanze kuchezea excel namna ya kuchakachua......
 
Tendwa toothless dog inapokuja kwa fujo zinazoasisiwa na ccm. Na inapokuja kwa vyama vya upinzani anajidai kujua vifungu na kutoa vitisho kibao.
Simpendi sana huyu baba anadhoofisha democracy!
 
Kwanza Tendwa yuko ofisini kinyume vya sheria kwani muda wake umekwisha.
Aache kurukia mambo asiyo yajua kama Chadema ndo waliofanya vurugu iweje Rage ndie kafunguliwa chages?? Babu umesha zeeka kalee wajukuu gamba wewe!
 
watu wamkumbushe bwana tendwa kwamba mambo yanayotokea ndani ya bunge hawawezi kuingiliwa na mihimili mingine zaidi ya rais kuvunja bunge na kuitishwa uchaguzi mwingine. Angalizo hili ni kwa mujibu wa katiba. Aidha hakuna jinai yoyote miliyofanyika ndani ya ukumbi wa bunge isipokuwa wabunge walionyesha hisia tofauti tu. Kama amekereka sana anachoweza kufanya ni kumshauri rais avunje bunge. Vingimnevyo hizi ni porojo na kelele za 'chura' zisizoweka kumzuia 'tembo' kunywa maji mtoni.
 
Huyu ni kibogoyo aliyetengewa nyama ya mifupa,hana msaada wala faida yoyote kwa taifa hili,kwani hata kazi yake haijui.Kwanza jina lake lenyewe linaonyesha hatakiwi.GO2HELL TEENDWA.
 
Kuna vurugu nyingine zinatokeaga ambazo cdm wanakuwa wamechoka kuvumilia vituko na manyanyaso ya serikali, basi matamko na kesi zinakuwa za moja kwa moja zinaelekezwa kwa cdm, watafunguliwa mashtaka, watawekwa ndani, watasota inavyokusudiwa. Vurugu na uvunjifu wa amani ukiwa na picha ya ccm moja kwa moja, utaona viongozi wanavyoanza kuzunguka, oh, shiria itachukua mkondo, bla bla kibao. Mkondo utachukuliwa lini?
 
Huyu ni kibogoyo aliyetengewa nyama ya mifupa,hana msaada wala faida yoyote kwa taifa hili,kwani hata kazi yake haijui.Kwanza jina lake lenyewe linaonyesha hatakiwi.GO2HELL TEENDWA.
 
Back
Top Bottom