Tendwa Atoa Tamko Dhidi ya CHADEMA na CCM

Tendwa Atoa Tamko Dhidi ya CHADEMA na CCM

issenye

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2011
Posts
3,795
Reaction score
5,253
TendwaMuda%2814%29%281%29.jpg

Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa

Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, amesema amesikitishwa na vurugu zilizotokea katika shughuri za kisiasa mkoani Jumapili iliyopita kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kusema kuwa ni ukiukwaji wa masharti ya usajili wa vyama vya siasa.

Katika taarifa yake jana, Tendwa alisema kifungu namba 9(2)(c) cha sheria ya vyama vya kisiasa ya mwaka 1992 kikisomwa pamoja na kifungu 5 (b)(i) kama kilivyorekebishwa mwaka 2009 kinakataza vurugu, fujo, matumizi ya nguvu na uvunjifu wa amani wa aina yoyote na kuwa ni kosa la jinai linalopaswa kufanyiwa kazi na mamlaka.

Tendwa alisema matukio kama hayo yanatengeneza taswira mbaya ya siasa nchini na kushusha heshima na imani ya wananchi kwa vyama vya siasa.

Alisema ofisi ya msajili inachukua suala hili kwa kuvihusisha vyama husika ili ipate ukweli na undani wake na iweze kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria.

Alisema,ofisi yake inavikumbusha na kuviasa vyama vya siasa kuheshimu sheria za nchi, sheria ya vyama vya siasa na maadili ya vyama vya siasa.

Viongozi na wafuasi wa vyama hivyo walipigana hadharani wakigombea uwanja wa kufanyia mikutano.

CHANZO: NIPASHE
 
MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, amesikitishwa na vurugu zilizotokea mkoani Dodoma Februari 3, mwaka huu zilizohusisha wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana Dar es Salaam, Tendwa alisema kazi yake ni kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa, ya mwaka 1992 na maadili ya vyama vya siasa yanayokataza vurugu, fujo na matumizi ya nguvu na uvunjifu wa amani.

"Nimesikitishwa na vurugu zilizotokea Dodoma, nachukuwa fursa hii kuutaarifu umma wa Watanzania kuwa mimi kama msimamizi wa utekelezaji wa sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992, nimesikitishwa sana na vurugu hizo," ilisema sehemu ya taarifa ya Tendwa. Alisema kufanya vurugu, fujo, matumizi ya nguvu na uvunjifu wa amani wa aina yoyote, ni ukiukwaji wa masharti ya usajili
wa vyama vya siasa.

"Kifungu cha 9(2)(c) cha sheria ya Vyama vya Siasa, 1992 kikisomwa pamoja na kifungu 5 (b)(i) cha sheria ya Vyama vya Siasa kama ilivyorekebishwa mwaka 2009. "Vurugu, fujo, matumizi ya nguvu na uvunjifu wa amani wa aina yoyote pia ni kosa la jinai ambalo linapaswa kufanyiwa kazi na mamlaka husika," alisema Tendwa.

Alisema ni vyema ieleweke kuwa matukio kama hayo yanatengeneza taswira mbaya ya siasa nchini na kushusha heshima na imani ya
wananchi kwa vyama vya siasa. Tendwa alisema ofisi yake inalichunguza suala hilo kwa kuvihusisha vyama husika, ili ipate ukweli na undani wake na iweze kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria.

"Ofisi ya msajili inavikumbusha na inaviasa vyama vya siasa vyote kuheshimu sheria za nchi, sheria ya vyama vya siasa na maadili ya
vyama vya siasa," alisema.

Source. Mtanzania.
 
Hivi Tendwa atastaafu lini!?
 
ndiomaana twataka katiba mpya kwa katiba hii unampa kesi ya wizi wa mahindi ya ngedere aiukumu nyani????tendwa anawajibika kwa mamlaka ya juu ambayo ni ccm sasa tutegemee nini hapa??? upuuz mtupu suluisho katiba mpya .....
 
Kwani mipaka ya msajili wa vyama vya siasa haikomi tu baada ya chama kusajiliwa?
 
Fujo tarehe3 tamko la kukemea linatoka tarehe7, alikuwa anasikilizia upepo ama?
 
Tendwa, waweza kukaa kimya na wala watu wasikufikirie kabisa kwa sababu husemi uyasemayo katika uhalisia. Ninadhani ni vile tu unadhani unategemewa kusikika!!!

Sheria za nchi hutungwa, husimamiwa, na huchukua mkondo wake!!! La kwanza limefanyika na ndio maana unaweza kutaja hivo vifungu husika. Haya mengine mawili ndipo kuna taabu. Si wewe wala Polisi mnaweza kusimamia vifungu hivi. Ni kwa sababu mnafanya kazi kwa niaba ya CCM. Na sheria haiwezi kuchukua mkondo hasa pale CCM anapokuwa mmoja wa walaumiwa. Nitaurejesha hapa;

a) Kuchomwa kwa nyumba ya kada wa CCM Igunga.
b) Kumwagiwa tindikali kwa kada wa CCM Igunga.
c) Kuuawa kwa mfuasi wa CCM Iramba Magharibi (kwa Mh. Madelu)
d) Kuuawa kinyama kwa kada wa CHADEMA Arumeru.
e) Kupigwa na kujeruhiwa kwa wabunge wa CHADEMA Mwanza.

Unapojitokeza na kuzungumzia sheria kufuata mkondo kwa mambo madogo kama kugombea uwanja wa mkutano, huku ukiacha mambo makubwa kama hayo, humtii wasiwasi yeyote kuwa una upendeleo. Lakini hata hivo, onesha sheria hizi zinawezaje kuchukua mkondo badala la kusema tu "nimesikitishwa"!!!
 
Fujo tarehe3 tamko la kukemea linatoka tarehe7, alikuwa anasikilizia upepo ama?

CCM wanatafuta pa kutokea sasa, na hakuna pengine ila ni kwa Tendwa tu kwani wamekwisha ona upepo wa nguvu ya Wananchi tumeligundua tayari hilo li Tendwa na CCM yao...
 
MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, amesikitishwa na vurugu zilizotokea mkoani Dodoma Februari 3, mwaka huu zilizohusisha wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana Dar es Salaam, Tendwa alisema kazi yake ni kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa, ya mwaka 1992 na maadili ya vyama vya siasa yanayokataza vurugu, fujo na matumizi ya nguvu na uvunjifu wa amani.

"Nimesikitishwa na vurugu zilizotokea Dodoma, nachukuwa fursa hii kuutaarifu umma wa Watanzania kuwa mimi kama msimamizi wa utekelezaji wa sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992, nimesikitishwa sana na vurugu hizo," ilisema sehemu ya taarifa ya Tendwa. Alisema kufanya vurugu, fujo, matumizi ya nguvu na uvunjifu wa amani wa aina yoyote, ni ukiukwaji wa masharti ya usajili
wa vyama vya siasa.

"Kifungu cha 9(2)(c) cha sheria ya Vyama vya Siasa, 1992 kikisomwa pamoja na kifungu 5 (b)(i) cha sheria ya Vyama vya Siasa kama ilivyorekebishwa mwaka 2009. "Vurugu, fujo, matumizi ya nguvu na uvunjifu wa amani wa aina yoyote pia ni kosa la jinai ambalo linapaswa kufanyiwa kazi na mamlaka husika," alisema Tendwa.

Alisema ni vyema ieleweke kuwa matukio kama hayo yanatengeneza taswira mbaya ya siasa nchini na kushusha heshima na imani ya
wananchi kwa vyama vya siasa. Tendwa alisema ofisi yake inalichunguza suala hilo kwa kuvihusisha vyama husika, ili ipate ukweli na undani wake na iweze kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria.

"Ofisi ya msajili inavikumbusha na inaviasa vyama vya siasa vyote kuheshimu sheria za nchi, sheria ya vyama vya siasa na maadili ya
vyama vya siasa," alisema.

Source. Mtanzania.

Na atoe tamko pia juu ya yaliyofaywa na wanachama na wapenzi na wafurukutwa wa CCM kung'oa bendera kutoka kwenye milingoti yake za vyama vya Chadema na CUF huko Mlandizi Kibaha. Yote yalifanywa na wafuasi hao wa CCM baada ya kupewa maelekezo na Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi wa CCM A. Bulembo
 
Tendwa tatizo lililopo ni kwamba anafanya kazi kwa maelekezo ya waliompa huo ulaji,sasa kama muda wake ulishaisha na hadi leo yuko ofcn kwanza ni uvunjwaji wa katiba na pili ni kwa maslahi ya magamba,so lazima mwisho wa hii conclusion itakuwa Chadema ndo walioanzisha ugomvi,nawaachieni mtaona wenyewe
 
Hivi watu wengine hawawezi kufanya kazi kimya kimya? Kama ameridhika kuwa kuna sheria zimekiukwa si achukue hatua? Mayowe ya nini?
 
Amemsahau Kingunge mwaka 2005 alivyomwambia aache chokochoko maana kaajiriwa na Serikali ya CCM!
 
Back
Top Bottom