Tendwa aionya tena CHADEMA...

Tendwa aionya tena CHADEMA...

Haujamwelewa Tendwa maana yake, ngoja ni jaribu kuifafanua hii kauli kidogo, hawa jamaa ni hatari sana, akikwambia 20% pass basi ujue ni 40 or 60%. Kuna vitu wanakuwa wanavificha, ndo maana tunawaita binadamu hawa 'wakoloni weusi'.

Anachozungumzia Tendwa hapa ni kujaribu kuhalalisha uwepo wa green guard kwa sababu moja kuu. Whatever thing that will be done by green guard, kwa namna moja au nyingine watachakachua ili ukweli usijulikane, so hakuna atakaye kamatwa.

On the other side, anamaanisha kwamba red guard wakifanya kitu chochote, wao watashitakiwa, kwa sababu sheria haiwaruhusu. In the worst case, Tendwa anamaanisha kwamba CDM mkipigwa nyamazeni, kwani inauma?.

Hivi hawa wazee wa ccm kwa nini wanapenda kudhani kwamba watz ni watu wajinga sana? Kama shida ya kuwa na vikundi vya kujilinda ni kuripoti tu kwenye vyombo vya dola sasa kunahaja gani ya kuwanavyo? what is point? Si mtu tu yeyote anaweza kufanya hiyo kazi, kwani CDM si wanawapenzi wengi tu kwenye mikutano?

Swala la kujilinda ni pamoja na kuarrest, kutiapingu na hata ikiwezekana kujeruhi ikiwa mtuhumiwa anania ya kukudhuru. Hauwezi kuniambia mimi eti jambazi kanikosakosa shaba, alafu nikijicheck na shaba mfukoni, eti nisimdhuru hata kama nikipata mwanya kwa sababu its against the law. Kudadadadadadeki!!!!!

Hizi ndo sheria gani? Au ndo zile sheria kama za kisultani. Kule Saudi Arabia kunamwanamke alikwenda kushitaki kwamba amebakwa akakamatwa yeye na yule aliyembaka, kisa, wamefanya mapenzi nje ya ndoa, mwanamke amefungwa miezi kumi nasita mwanaume kumi na mbili. Mantiki iko wapi hapo?
 
Anazungumziaje haya makambi yanayofundisha ulinzi, usalama na ukakamavu kupiga wapinzani, kama inavyoelezewa hapa kwenye kitabu cha 'Sera za Msingi za CCM' ukurasa wa 87na kwenye cheti cha wahitimu.

Anataka aletewe na mtaala wanaofundishiwa!
 
Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1374693357.668403.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1374693357.668403.jpg
    81.8 KB · Views: 175
  • ImageUploadedByJamiiForums1374693382.490371.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1374693382.490371.jpg
    74 KB · Views: 148
  • ImageUploadedByJamiiForums1374693404.861841.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1374693404.861841.jpg
    113.5 KB · Views: 158
CHADEMA walishamuona huyu propangidist wa CCM kitambo sana. Mwaka jana, Septemba 10, wakamtangaza adui wa demokrasi nchini.

"Aliongeza kuwa katika mfumo wa vyama vingi, viongozi wenye mamlaka ya kiserikali wasipokuwa makini katika kutoa matamko yao wanaweza kuhatarisha usalama wa nchi na kuelezea kauli za Tendwa kuwa haziwezi kuvumiliwa na watu wanaoitakia mema Tanzania.

“Kumuendekeza Tendwa kwa kauli zake ni kuliandaa taifa na maafa makubwa kwa kuwa anachoongea hakilingani na hadhi yake ya kuwa mlezi wa vyama vya siasa na katika hili tumeamua kutoshirikiana naye kwa namna yoyote mpaka atakapoomba msamaha na awe amejirekebisha,” alisema Mbowe.

Alisema CHADEMA itaendelea kufuata sheria na iko tayari kukutana na karani katika ofisi ya msajili kuliko kuhudhuria kikao kitakachoitishwa na Tendwa ambaye alimuelezea kuwa anatumiwa au anajipendekeza kwa watawala na kusahau majukumu yake kama mlezi wa vyama vyote.

Alisisitiza kuwa kwa udhaifu unaoonyeshwa na msajili huyo, Kamati Kuu ya CHADEMA imemtangaza kuwa adui namba moja wa demokrasia nchini na kwamba hafai kuwa katika nafasi aliyo nayo."

Gazeti la Tanzania Daima.
 
CCM, wao wanawaza labda chadema watalipiza lile bomu la arusha , wamesikia tu neno UKAKAMAVU tayari wamelipuka , sisi hatuko huko kitu kimo kwenye maandishi ni msisitizo tu na tafakuri zenye hekima
 
Msajili wa vyama vya Siasa nchini amewaasa wanachama na viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutumia muda wao kufanya shughuli za siasa ili kuchangia maendeleo ya nchi badala ya kutumia uwezo na muda wao kubuni mambo yanayoleta mtafaruku na kuhatarisha amani ya nchi.

Pia amepinga tamko la chama hicho la kuanzisha mafunzo ya kujilinda kwa vijana wake nchi nzima.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam na kusainiwa kwa niaba ya Msajili wa vyama vya siasa Sisty Nyahoza alisema kuwa hajawahi kuruhusu CHADEMA au chama chochote cha siasa kufanya mafunzo ya ukakamavu au mafunzo ya kutumia nguvu ya aina yoyote kwa wanachama wake au mtu yeyote yule.

Anaongeza kuwa CHADEMA wanaruhusiwa kuanzisha vikundi vya kujilinda lakini hawaruhusiwi kuanzisha mafunzo ya kutumia nguvu kwaajili ya kujilinda kama walivyotangaza katika mikutano yao ya hadhara kwani ni kinyume na Demokrasia na Katiba ya Jamuhuri ya Muungano.

Nyahozo ametoa ufafanuzi kuhusu vikundi vya ulinzi na usalama vilivyopo katika Katiba ya Vyama vya Siasa kwamba vikundi hivyo haviruhusiwi kufanya mafunzo ya kutumia nguvu ya aina yoyote katika kutekeleza majukumu yao.

Bali wajibu wao ni kutoa taarifa wa vyombo vya Dola pale wanapo sikia au kuona uhalifu ukitokea na wala sio kupambana na wahalifu au watu wanaotaka kuwadhuru kama tamko la CHADEMA la tarehe 9 mwezi huu linavyo sema.

"Hakuna maelezo yoyote katika Katiba ya CHADEMA yanayoruhusu kutumia nguvu kufanikisha shughuli za kulinda mali na Viongozi wa Chama. Ni vyema wananchi wote waelewe kuwa Sheria za Nchi zimeweka masharti maalumu kwa Vyama Vya Siasa kutokana na umuhimu wa vyama hivi katika kudumisha aman utulivu na umoja wa Kitaifa", alisema Nyahoza.

Alisema kuwa kutokana na Ibara ya20(2)C ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1997 inasema kuwa "Bila kujali masharti ya ibara ya (1) na (4),haitakuwa halali kwa chama chochote cha siasa kuandikishwa ambapo kutokana na katiba au sera yake:-kinakubali au kunapigani matumizi ya nguvu au mapambano kama njia za kufikia malengo yake ya kisiasa.

Nyahoza alimaliza kwa kuwataka CHADEMA kuacha kutekeleza mpango walio tangaza wa kuanzisha makambi ya kufanya mafunzo ya kujilinda kwa vijana wao nchi nzima,kwani kufanya hivyo ni kukiuka sheria za nchi na endapo watashindwa kutii agizo hilo hatua za Kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Mwisho.
 
nitarudi, kwani JF sasa kwenye simu tamu kweli hongera zao ma incharge kwakuiweka poa

Tendwa kaishachoka kama simba zeee.
 
Tendwa ni kihiyo, hajui kazi yake.

Anadhani msajili Wa vyama Ni taasisi ya CCM!
 
Vijana hebu muwe na huruma na huyu Kikongwe , kwa umri wake hastahili hata kuvuta sigara yenye kichungi bali anastahili KIKO .
 
Tendwa nahisi huyu mzee anazeeka vibaya....

  • siyo kazeeka vibaya bali katumwa huyu.
  • CCM wanataka kubaki madarakani hata kwa gharama ya kumwaga damu ya melfu ya watanzania
  • Na hiyo mbinu ya kawanyanyasa chadema kwa mabomu na risasi za moto zitaendelea mpaka uchaguzi ujao labda mataifa yaingilie kati lakini bila hivyo tutaendelea kushuhudia haya mpaka tutazoea kama wenzetu Pakistani na Iraq. kwani wasipofanya hiyo wanawezatoka madarakani hata kabla ya uchaguzi kwani asilimia kubwa ya watanzania wameshaikinahi hii serikali.
  • Gharama ya haya yanayofanywa na serikali kwa sasa ni kuingia mikataba ya rasilimali na maliasili isiyo na tija kwa taifa ili kufunga kauli za utetezi kutoka mataifa makubwa.
 
Nchi GANI DUNIANI VIONGOZI wa kuandikisha VYAMA wana NGUVU zaidi ya Wabunge... NCHI YETU CCM inawapa NGUVU yoyote atakayeipa MCHECHETO CHADEMA
 
Na Jennifer Chamila, MAELEZO

Msajili wa vyama vya Siasa nchini amewaasa wanachama na viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutumia muda wao kufanya shughuli za siasa ili kuchangia maendeleo ya nchi badala ya kutumia uwezo na muda wao kubuni mambo yanayoleta mtafaruku na kuhatarisha amani ya nchi.

Pia amepinga tamko la chama hicho la kuanzisha mafunzo ya kujilinda kwa vijana wake nchi nzima.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam na kusainiwa kwa niaba ya Msajili wa vyama vya siasa Sisty Nyahoza alisema kuwa hajawahi kuruhusu CHADEMA au chama chochote cha siasa kufanya mafunzo ya ukakamavu au mafunzo ya kutumia nguvu ya aina yoyote kwa wanachama wake au mtu yeyote yule.

Anaongeza kuwa CHADEMA wanaruhusiwa kuanzisha vikundi vya kujilinda lakini hawaruhusiwi kuanzisha mafunzo ya kutumia nguvu kwaajili ya kujilinda kama walivyotangaza katika mikutano yao ya hadhara kwani ni kinyume na Demokrasia na Katiba ya Jamuhuri ya Muungano.

Nyahozo ametoa ufafanuzi kuhusu vikundi vya ulinzi na usalama vilivyopo katika Katiba ya Vyama vya Siasa kwamba vikundi hivyo haviruhusiwi kufanya mafunzo ya kutumia nguvu ya aina yoyote katika kutekeleza majukumu yao.

Bali wajibu wao ni kutoa taarifa wa vyombo vya Dola pale wanapo sikia au kuona uhalifu ukitokea na wala sio kupambana na wahalifu au watu wanaotaka kuwadhuru kama tamko la CHADEMA la tarehe 9 mwezi huu linavyo sema.

"Hakuna maelezo yoyote katika Katiba ya CHADEMA yanayoruhusu kutumia nguvu kufanikisha shughuli za kulinda mali na Viongozi wa Chama. Ni vyema wananchi wote waelewe kuwa Sheria za Nchi zimeweka masharti maalumu kwa Vyama Vya Siasa kutokana na umuhimu wa vyama hivi katika kudumisha aman utulivu na umoja wa Kitaifa", alisema Nyahoza.

Alisema kuwa kutokana na Ibara ya20(2)C ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1997 inasema kuwa "Bila kujali masharti ya ibara ya (1) na (4),haitakuwa halali kwa chama chochote cha siasa kuandikishwa ambapo kutokana na katiba au sera yake:-kinakubali au kunapigani matumizi ya nguvu au mapambano kama njia za kufikia malengo yake ya kisiasa.

Nyahoza alimaliza kwa kuwataka CHADEMA kuacha kutekeleza mpango walio tangaza wa kuanzisha makambi ya kufanya mafunzo ya kujilinda kwa vijana wao nchi nzima,kwani kufanya hivyo ni kukiuka sheria za nchi na endapo watashindwa kutii agizo hilo hatua za Kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

××××××××××××××

Kwahiyo jambazi mbakaji akimwendea huyu Tendwa atakuwa na uwezo wa kutulia tu wakati yule mhalifu akiwabaka yeye na familia yake na kuwaibia vitu vyao akisubiri kutoa taarifa polisi kuwa Mrisho (jina la kubuni la jambazi) kaja na kanifanyia uhalifu huu ili polisi waanze kuchukua hatua za kisheria? Sipati picha ya scene hiyo na vile itavyokuwa kichekesho hata kwa Jambazi mbakaji huyo na polisi wangmuona zuzu tu. Kama hiki ndicho anatata mtu yoyote yule afanye, aje kwangu kuleta vurugu aone kama sitawapelekea kichwa chake polisi ili waje wachukue mzoga uliobaki. kujilinda/mtu au watu ni haki yao ambayo si ya kujadiliwa hata na hayawani. Imagine hata kuku anafurukuta akichinjwa alafu tendwa aseme hakuna kutumia nguvu! subutu!!!! anathibisha tu ubaya wa hongo ya cheo .CDM imarisheni haraka hiyo RED BRIGADE yenu.
 
Movie yenyewe unaifahamu au unaisikia? Mie nilishawahi kuiona, ya Kihindi:

Jamaa mmoja, MGOGO akiwa uwanja wa Fundi Selemala na Mama Kubwa, mara ukafika muda wa jamaa kufika kileleni, ghafla kuangalia pembeni, akaona nyoka anamsogolea taratiiibu. Jamaa akaanza kujitetea......

" weee nyoka weee, shiiii shiiiii, tuache bwana wenzio tumalizie basi, ishiii ishiii......" Nyoka akambusu kalio, akaondoka.

green-and-yellow-snake-wallpaper-220x123.jpg

Nchi nzima sasa imegeuka bongo movie
kila siku toleo jipya
 
kuna majina nikiyaona kwenye media hata kabla ya habari najua ni 'scrappy coco': tendwa,muhongo,mulugo,....

Mkuu ndebile umemsahau mizengo pinda naye ni dizaini hizo hizo za akina tendwa, muhongo, mulugo hawa watu ni majanga bila kumsahau mwigulu na nape.
 
Hapa mimi nimechoka kabisa. Msajiri anasema vyama vinaruhusiwa kuanzisha vikundi ila visitumie nguvu kujilinda bali wajibu wao ni kutoa taarifa. Kuna haja ya kuwa na kikundi kwa ajiri ya taarifa tu?
 
Anabweka tu huyo lakini hawezi kung'ata kwa vile hana meno!!!!!!
 
Back
Top Bottom