Tendwa aionya tena CHADEMA...

Tendwa aionya tena CHADEMA...

mwaikenda

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2011
Posts
903
Reaction score
144
Na Jennifer Chamila, MAELEZO

Msajili wa vyama vya Siasa nchini amewaasa wanachama na viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutumia muda wao kufanya shughuli za siasa ili kuchangia maendeleo ya nchi badala ya kutumia uwezo na muda wao kubuni mambo yanayoleta mtafaruku na kuhatarisha amani ya nchi.

Pia amepinga tamko la chama hicho la kuanzisha mafunzo ya kujilinda kwa vijana wake nchi nzima.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam na kusainiwa kwa niaba ya Msajili wa vyama vya siasa Sisty Nyahoza alisema kuwa hajawahi kuruhusu CHADEMA au chama chochote cha siasa kufanya mafunzo ya ukakamavu au mafunzo ya kutumia nguvu ya aina yoyote kwa wanachama wake au mtu yeyote yule.

Anaongeza kuwa CHADEMA wanaruhusiwa kuanzisha vikundi vya kujilinda lakini hawaruhusiwi kuanzisha mafunzo ya kutumia nguvu kwaajili ya kujilinda kama walivyotangaza katika mikutano yao ya hadhara kwani ni kinyume na Demokrasia na Katiba ya Jamuhuri ya Muungano.

Nyahozo ametoa ufafanuzi kuhusu vikundi vya ulinzi na usalama vilivyopo katika Katiba ya Vyama vya Siasa kwamba vikundi hivyo haviruhusiwi kufanya mafunzo ya kutumia nguvu ya aina yoyote katika kutekeleza majukumu yao.

Bali wajibu wao ni kutoa taarifa wa vyombo vya Dola pale wanapo sikia au kuona uhalifu ukitokea na wala sio kupambana na wahalifu au watu wanaotaka kuwadhuru kama tamko la CHADEMA la tarehe 9 mwezi huu linavyo sema.

"Hakuna maelezo yoyote katika Katiba ya CHADEMA yanayoruhusu kutumia nguvu kufanikisha shughuli za kulinda mali na Viongozi wa Chama. Ni vyema wananchi wote waelewe kuwa Sheria za Nchi zimeweka masharti maalumu kwa Vyama Vya Siasa kutokana na umuhimu wa vyama hivi katika kudumisha aman utulivu na umoja wa Kitaifa", alisema Nyahoza.

Alisema kuwa kutokana na Ibara ya20(2)C ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1997 inasema kuwa "Bila kujali masharti ya ibara ya (1) na (4),haitakuwa halali kwa chama chochote cha siasa kuandikishwa ambapo kutokana na katiba au sera yake:-kinakubali au kunapigani matumizi ya nguvu au mapambano kama njia za kufikia malengo yake ya kisiasa.

Nyahoza alimaliza kwa kuwataka CHADEMA kuacha kutekeleza mpango walio tangaza wa kuanzisha makambi ya kufanya mafunzo ya kujilinda kwa vijana wao nchi nzima,kwani kufanya hivyo ni kukiuka sheria za nchi na endapo watashindwa kutii agizo hilo hatua za Kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

××××××××××××××

NIMEMEPITIA TAMKO LA TENDWA HILO HAPO JUU NA NIKAPATA TAFAKURI IFUATAYO:
1. KUMBE TENDWA ANARUHUSU VIKUNDI VYA KUJILINDA KATIKA VYAMA NA NDIYO MAANA ALISAJILI KATIBA ZA VYAMA INCLUSIVE CHADEMA AMBAYO MSAJILI AMEKUWA AKITOA MATAMKO YASIYO NA TIJA.
2. TENDWA KARUHUSU VIKUNDI HIVI KWA AJILI YA KULINDA VIONGOZI WA CHAMA NA MALI ZA CHAMA,

UJINGA UPO HAPA
A) Tendwa ameshindwa kufafanua nini maana pana ya neno "nguvu" na je utajilinda bila nguvu? na je kama ni vikundi kwa ajili ya kujilinda Chadema walitamka lini kuwa watatumia " nguvu" kujilinda na kuwalinda viongozi wa chama"
Naomba tendwa atoe ufaafaunizi mpana kama mwanasheria juu ya nini maana ya neno "nguvu" (Broader interpretation of the word " nguvu") na je nini tofauti kati ya "ukakamavu" na "nguvu"

Ofisi imepwaya ya msajili kwa hili inadhihirisha namna gani nchi ina viongozi vilaza kama mbunge wa kipindi kile pale temeke.....KIHI......
 
huyu babu kavurugwa sasa kama mtu anamfanyia fujo ataenda polisi kwanza bila kujitetea? na kwa dunia ya sasa huwezi kujitetea bila kuwa fiti babu kwa ujumla wake kavurugwa. VIVA CDM VIVA M4C
 
Haya ndiyo madhara ya kuwa na Msajili mwenye umri wa miaka 70 Ofisini.
 
yaani ameruhusu vyama kujilinda, lakini haruhusu kuanzisha vikosi vya kujilinda!!!! Da kazi tunayo
 
Tendwa anafanya kazi kwa mkataba, Kwa kuwa yupo pale kwa mkataba, amekosa sifa za kisheria kusajiri au kufuta chama chochote cha siasa
 
Tatizo linakuja pale Msajili wa Vyama vya Siasa anapogeuka Msemaji wa Chama Tawala aidha kwa Makusudi ama kwa bahati mbaya...
 
Huyu anachotetea ni ujira wake tu hana faida yoyote ktk TZ hii zaidi ya hasara.
Watu kama hawa ni wa kuuwa mapema sana coz wanaleta hasara kubwa ktk taifa.
 
Bado nasoma na kurudia rudia sijaona hasa gist of the matter.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
kuna majina nikiyaona kwenye media hata kabla ya habari najua ni 'scrappy coco': tendwa,muhongo,mulugo,....
 
Hata hivyo kwa nini asaini msaidizi na asisini Masjili mwenyewe?
 
You know what is insernity...

Naona ameanza kuongeza maneno mengine kisha kujitafutia hukumu. This guy has completely lost any moral authority, if at all he ever had before. Matokeo yake, hata ofisi yake yote itaanza kutafsirika kama alivyo yeye mwenyewe.

Tamko la CHADEMA lililotokana na maazimio ya Kamati Kuu, lilisema hivi;


4:0. Uchaguzi wa Madiwani.

Kamati Kuu imepokea taarifa kuhusu ushiriki wa CHADEMA katika Uchaguzi wa Madiwani uliofanyika tarehe 16/06/2013 katika kata 22.

 Kamati Kuu imeipongeza Sekretarieti na uongozi wa Kanda mbalimbali za CHADEMA kwa maandalizi mazuri katika Uchagzuzi huo uliosababisha CHADEMA kuwapokonya CCM ushindi katika kata 4 ilizokuwa imeshinda katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010. Kamati Kuu imewapongeza wananchi kwa kuipatia CHADEMA kura asilimia (47.7%) dhidi ya CCM (49%) na (3.3%) za CUF.

 Kamati kuu imesikitishwa na vitendo vya fujo walivyofanyiwa viongozi, wagombea pamoja na Wanachama mbalimbali katika sehemu mbalimbali palipo fanyika Uchaguzi. Kamati Kuu imesikitshwa na kulaani vitendo hivyo vikiwemo vya watu kukatwa mapanga , kuchomwa visu na kubakwa kwa akina Mama na vijana wahuni walioandaliwa na Chama cha Mapinduzi
 Kamati Kuu imelaani vitendo hivyo vya kinyama vilivyofanywa mbele ya jeshi la polisi na Wakuu wa Wilaya.

 Ili kukabiliana na vitendo vya fujo vinavyofanywa na vijana wa CCM dhidi ya wagombea, Wanachama na viongozi wa CHADEMA, Kamati Kuu imeagiza kwamba kitengo cha ulinzi cha Chama “Red Brigade” kiimarishwe zaidi kwa kuhakikisha kuwa vijana wote wa Red Brigade Nchi nzima wanapewa mafunzo maalum ya UKAKAMAVU yatakayoandaliwa katika Makambi maalum katika mikoa yote.

@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@

Aya ya mwisho hapo kwenye tamko, ndiyo inayowahangaisha.

Sasa unaweza kulinganisha na hicho kinachosemwa kwenye tamko eti la ofisi ya msajili wa vyama. Baada ya ushahidi mfululizo kutolewa na kuibana serikali, ofisa wa dawati la propaganda nje ya Lumumb! amekurupushwa tena kuja kuropoka lolote.

Ofisi zingine za umma zinadhalilishwa sana.
 
Tatizo linakuja pale Msajili wa Vyama vya Siasa anapogeuka Msemaji wa Chama Tawala aidha kwa Makusudi ama kwa bahati mbaya...

Ni ofisa wa dawati la propaganda nje ya Lumumba. Baada ya kujidhalilisha yeye vya kutosha sasa anadhalilisha tu ofisi ya umma, anayoikalia kinyume cha sheria.
 
Back
Top Bottom