Tenda wema uende zako

Tenda wema uende zako

kwamtoro

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2010
Posts
4,922
Reaction score
3,245
Usisubiri shukrani. Ilikuwa pasaka ya mwaka 2007 usiku wa saa saba usiku. Nilikuwa natokea kwenye mizunguko ya pilikapilika ya pasaka kama ilivyo kawaida ya sikukuu ndani ya bongo. Nilifika kawe bus stand tayari kwa kushuka ndani ya dalalala. Punde kijana moja ambaye alikuwa ndani ya daladala amekaa katika kiti cha wanafunzi alikwapua pochi ya dada ambaye ilikuwa na simu pamoja na fedha. Dada kwa kweli alionekana kuchanganyikiwa.

Baada ya mimi kuangalia mchezo mzima nilibaani kulikua kuna uwezekano mkubwa wa konda na kibaka wapo kitu kimoja. Abiria wenzangu walishuka kila moja akisema hili na lile. Ila hata moja akuweza kutoa ushirikiano mpaka mwisho. Namaanisha kila moja alichukua time zake. Mimi japo sina tabia ya unoko, ila kwa hili nakajiapisha lazima nimsaidie huyu dada mpaka dakika ya mwisho. Nikasema hapana as long as a man hata nikikesha nje kesho hama noma still holiday, jumatatu ya pasaka.

Nikamnongoneza yule dada komaa nao hapa mimi naenda kuripoti police. Yule dada kweli alifanya nilivyo mwagiza. Nilimwambia asikae kimya ili ajaze watu bus ishidwe kugeuza. Nakumbuka nilitoka speed kali mpaka kituo cha police Kawe.

Nafika pale nikaona kuna askari ofisi ya mkuu wa kituo. Ila kiukweli huyu askari alikuwa mzito kidogo, sikupata shida kufahamu nini sababu, ilikuwa pasaka day.

Punde nikapewa askari kwenda kawe stand. Kufika tukawasomba dereva na kondo. Kufika konda na dereva ki ukweli walikuwa mafundi sana wa kujieleza. Maskini dada alikuwa siyo fundi wa kuzungumza. Nikasema hawa jamaa wasinitanie. Nikawa mimi ndio mzungumzaji kupita hata mshitaki. Baada kufungua kesi, tuliambiwa tutoke njee. Punde konda walimfanyia upelelezi wa kipolisi. Wakati tupo njee konda alitoka na askari moja. Nilimwangalia konda nikabaani siyo yule ambaye alikuwa mzungumzaji, uso mwekundu, amekuwa mpole.

Tukaanza safari ya kwenda kumkamata mwizi wa dada, hapo majira kama ya nane usiku. Pita pita vichochoro vya kawe, amina mwizi wa dada huyo mikononi mwa polisi. Mida ya saa tisa mimi huyo nikaachana na dada yeye akiwa anaambatana na wezi kuelekea kituoni.

Dada akanishukuru sana, akaniomba namba ya simu ila nilimjibu sina kwa sababu alionyesha kama ana nia ya kunipa asante kwa term kama ya pesa hivi.

Ikapita miaka kadhaa. Mwaka 2012 mwezi wa tatu ajira yangu akikomaa kwa mwajiri wangu. Kwa bahati mbaya ilikuwa ghafla na sikuwa nimejiandaa.

Balance yangu ilinisukuma miezi kadha shida ikapiga hodi. Nikaaza kupeleka CV zangu sehemu mbalimbali pamoja na makampuni ambayo yanawatafutia watu ajira kama Erolink wapi. Maisha yakawa tyte kinoma. Familia ilikuwa inaniangalia, ilikuwa kila kukicha napiga kwata town na mbaasha wangu wa kaki.

Niliona mimi kama mwanaume nisichague kazi, ikanibidi nijichanganye sehemu za ujenzi, kupiga zege. Siku niliofika kwa mara ya kwanza nilikuta vijana wengi sana wanasubiri kuanza kufanya kazi. Daa hapo kulikuwa na harufu ya bangi tu, vijana wamekomaa kweli kweli. Ikanibidi nimtafute mkubwa wao. Nikamwomba nipige zege pale. Da jamaa akaniambia subiria. Akaenda kuwaeleza wale vijana da walipo niangalia walicheka sana. Waliniona legelege sana mwisho wa siku sikupata kibarua nikarudi home. Kila nikiangalia salio linayoyoma ajira sina. Home ratiba ya mlo moja ikaingia, kila siku mwendo wa mboga za majani dagaa na thamani ya chakula ikawepo maradafu.

Nakumbuka mwezi wa nane kiukweli ndio siku ya salio langu kuisha kabisa ndipo nilipo pata miujiza. Nipo town naelekea imalaseko kuulizia ajira, punde prado likapaki mbele yangu hapo njaa inaniuma vibaya jasho linatoka mpaka chumvuchumvi inabaki katika ngozi yangu.

Dada moja mrembo akafungua kioo cha gari yake. Mara kaka habari, nikaitikia nzuri. Vipi unanikumbuaka, nikamweleza sura yako very familia kwangu ila siyo mbaya tukikumbushana tumeonana wapi. Unakumbuka kawe niliibiwaga pochi. Nikamwambia ndio dada, nimeshakukumbuka. Akaniuliza, vipi unaenda wapi? Nikamweleza naenda imalaseko. The way nilivyo kuwa aikumpa tabu kufahamu kwamba ni mtu ambaye na tatizo.

Akafungua mlango twende. Brake ya kwanza ikapigwa salender bridge club. Dada akajiagizia sato tu. A
 
Kweli Mungu hamuacha mja wake... Mshukuru Mwenyezi Mungu...

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Mkuu watu wanatoa misaada kwa kutanguliza nini atapata. Mwenzako akipata tatizo saidiana naye.
 
Dah mambo ya Profesa J wa mitulinga............!
 
Mshukuru Yesu kwa Muujiza wake wa Pasaka.. Hata Yule Mwizi waliesulubiwa naye alipata bahati ya kwenda Mbinguni
 
Hakuna Kama mungu!
Na wewe gusa mioyo ya watu mungu apate kuinuliwa kupitia Kwako!
 
Its a touchable story kwelikweli.Sometimes you may not imagine kwamba ni true story but inaonyesha bado kuna part 2 nadhani na part 3 hivi. BADO NASUBILI PART ZINGINE MKUU.
 
mhh dizain CHAI CHUNGU kaja kivingine haya mi taisoma kesho unmalizie yote sawa???
 
Last edited by a moderator:
nimejikuta nimeacha kufanya kazi ghafla....aya kaka nangojea part 2
 
Back
Top Bottom