Tembosa!! Bado nina Shida kubwa..Niamue nini?

Tembosa!! Bado nina Shida kubwa..Niamue nini?

Nashukuru Husninyo na naomba nikusalimie pia
nasubiri hii movie ya kihindi hapa

hii movie ya kihindi muhusika atazaa halafu yule mtoto atakuja kuwa stelingi kwa muda, atakufa ila ataacha mtoto mmoja, atarevenge.....
 
Last edited by a moderator:
Duuuh!!! shem mtihani huo maana stori ni ndefu...

Jamaa alipendana na msichana anaitwa Vannesa, inaonesha walipendana kweli kwani mapenzi yao walianza ile kama kaka na dada...

Jamaa alivuka vikwazo vingi ikiwemo mikwara toka kwa kakaze Vannesa, pamoja na hayo kuna siku jamaa alipigana na kaka yake Vannesa baada ya kushindwa kuvumilia kumuona Vannesa wake anaadabishwa na kakaye...

Siku hiyo baada ya Vannesa kudundwa na kakaye, mtoto wa kike alitaka kujichoma kisu na aliyemuokoa Vannesa asijichome kisu ni mpwa wa huyu Tembosa...

Stori ikaenda weeee, hadi ambapo Vanessa alikuwa anahitaji kuolewa lakini bwana Tembosa hakuwa kajipanga kuwa mume mtajiwa...

Hata Vannesa alipompa last chance, Tembosa aligoma kabisa na kutoa go-ahead kwa Vannesa kuolewa na kidume mwingine tu...

Mtoto Vannesa hatimaye akaolewa na mtu mwingine na kitendo hicho kikaukwaa moyo wa Tembosa hadi kudiriki kutokupenda tena maishani pia akawachukia sana wanawake tokea wakati huo...Kuna mahali anakiri kuwa mpenzi wake mkubwa kwa sasa ni gambe...(mambo ya nani kamwaga ulabu wangu, nauliza hahaha)...

Stori ikaendaaaa weeee, Vannesa kuna wakati akawa anaenda Dubai kibiashara na akampa mwaliko bwana Tembosa, laini Tembosa akachomoa...

Baadaye Vannesa akarejea kutoka Dubai, lakini akiwa na habari nzuri ya ujauzito na mzigo huo bibiye Vannesa alidai ni wa Tembosa (kuna wakati hawa watu walidinyana...)...

Hiyo siku Vannesa aliyotoka Dubai, Tembosa alimpokea bibiye pale Mbezi Mwisho kituo kipya na wakaenda zao Kibaha kwenda kupeana michapo ya ujauzito wa Vannesa...hapo Vannesa kumbe ana lake jambo, ameshajiandaa kimwili na akili kwenda kutoa tunda kwa Tembosa

Shem, kufika Kibaha mida ya usiku usiku wakati wanajiandaa kula tunda la mzeituni, bwana Tembosa si akashangaa kukuta Vannesa kafunga kigodoro tumboni...kumbe Vannesa hakuwa ujauzito wala nini ilikuwa ni tego tu mtoto wa kike badala ya maji aseme mmaaa...

Tembosa kuona hivyo akili ikamtoka, akampa kichapo Vannesa hadi mtoto wa kike akazimia ila baadaye akazinduka. Baada ya kuzinduka Tembosa akamkokota bibiye hadi kwenye gari halafu huyoooo akakanyaga mafuta kurudi Mbezi.

Kufika Mbezi akamwacha solemba bibiye Vannesa, yeye akaenda zake kwa mshikaji wake kubonyea kwa usiku huo hata siku zilizofuata...

Sasa baada ya siku hiyo Tembosa ndio kachanganyikiwa, anataka kwenda kumsemea Vannesa kwa mama yake...eti Vannesa kazidi kumganda kama kimavi cha mapera wakati ni mke wa mtu!!!

Sasa endelea na stori...
mkuu inabidi Tembosa awe anaku consult kabla hajapost,maana umesummarize vizuri sana...
 
hii movie ya kihindi muhusika atazaa halafu yule mtoto atakuja kuwa stelingi kwa muda, atakufa ila ataacha mtoto mmoja, atarevenge.....
Husninyo wacha tuendelee kuangalia mwisho wake utakuwaje na then tujue sterling anakufa au anajirusha kutoka kwenye ukuta au anafanyaje
 
Last edited by a moderator:
Husninyo wacha tuendelee kuangalia mwisho wake utakuwaje na then tujue sterling anakufa au anajirusha kutoka kwenye ukuta au anafanyaje

hahahah, ngoja tuone. mie ntakuwa nachukua summary kwa shem langu la ukwehe maana kufatilia siwezi.
 
Last edited by a moderator:
mimi za kihindi huwa siangalii shem. wale majamaa wanapenda sana kulia lia.

Heheh!!! basi shem utakuwa umezoea sana kuangalia muvi a kina Van Damme ambao wao ni kutoa kichapo mwanzo mwisho...
 
...Ibada iliisha kama saa nne kasoro hivi,
baada ya kumaliza ibada mtu wa kwanza kuongea nae
alikuwa my cousin nilimjulia hali pale,
yeye alikuwa ana kikao pale kanisani so alibaki.
mi sikuwa na haja tena ya kuonana na mama v,
nilenda zangu nyumbani moja kwa moja.
Nilimkuta mdogo wangu na housegirl wazee wangu
hawakuwepo walienda kusalia Makabe,

Nilisalimiana na mdogo wangu,
wakaniandalia chai pale na baada ya chai..
sikuwa na cha kufanya tena so nilikaa pale sebuleni huku na chat
kupitia simu yangu nikiwa na vuta vuta muda,

Mawazo yangu yote ilikuwa juu ya wito
niliokuwa nimepanga na nikawanajiuliza ni katika
mazingira gani nitakayokuwa nazungumza na mama V na ni nini yeye
alipanga kuniambia na mimi nitajieleza vipi
kama nitalaumiwa kusababisha Vanie alazwe hospitalini.

Pia nilijaribu kuhusisha ishu ya kibaha na kulazwa kwake hospitalini
Nilatafakari sana na kichwani mawazo yalikuwa mengi kupita kiasi.
Kwenye saa sita hivi wazee wangu walirudi kutoka kanisani,
Nilidhani labda na wenyewe walikuwa wanajua juu ya Vane
kulazwa hospitalin, nilitamani kumwuuliza mama lakini
Akili ikaniambia hapana, itakuwaje nikimuuliza na yeye aseme hajui
kitu ingekuwaje?
je, muendelezo wa maswali yake ningeuweza?
Niliamua kumute tu na kukaa kimya kama hakuna ninachokijua,

Nilitumia muda ule kuwaelezea Wazee wangu juu ya likizo na
Niliwaambia kuwa jumatatu, yaani jana ningesafiri.
Tukaendelea na stori stori pale huku muda ukisonga
Ilipofika saa saba kama na robo hivi, mdogo wangu alitenga msosi,
it was lunch time, japokuwa mimi sikuweza kula, nilikula kiduchu sana
Walivyoniuliza kulikoni nikatoa kisingizio cha kunywa chai muda mfupi
uliopita, ila haikuwa sababu bali mawazo lukuki.

Kwenye saa nane na nusu niliaga pale home, kwa minajili
ya kuna sehemu nakwenda na sitarudi tena pale, sikutaka kabisa
mtu ajue kama nilikuwa naenda kwa wazazi wa ex girl wangu as kila
mtu pale nyumbani alikuwa anajua juu ya mahusiano yangu na yeye kabla hajaolewa.

Nilienda vizuri tu nikabisha hodi nikafunguliwa geti
Aliyefungua ni mdogo wa Vanie wakiume,
akanisalimia, nikamuuliza kama mama yupo akasema yupo
ndani, kabla sijamwambia akamwambie kuna mgeni wake, Mama alitokea
Akanikaribisha! kuna viti pale nje nikawa nimekaa
cha kwanza kuuliza niliuliza kama mzee yupo, mama akaniambia hayupo,
Kuna project anaifanya huko Iringa ana kama siku 4 hivi..

Mama akaanza kuniambia unajua Vanessa anamatatizo makubwa sana,
matatizo!! nilihofu kidogo nikamuuliza mama kwani
Anasumbuliwa na nini? akaniambia kwani hakuna ninachokijua?
Duh hapo nikawa dilema kidogo kwa kweli kwani hata mimi
sikujua huyu Mama anajua nini so sikuwa tayari kufunguka
moja kwa moja,
nikamjibu mi mbona sijui?

Mama akaniambia Mwanangu! kuwa tu muwazi kwangu
mimi najua!
mhhh!! mtihani huu sasa, ilibidi nimrudishie mama swali
kwani unajua nini?
akaniambia ujue nilitumia nguvu nyingi sana kuinusuru ndoa ya mwanangu..
Mtoto wangu yuko kama kachanganyikiwa sasa,

Na mimi nikaanza kuona huruma jinsi mama alivyoniambia
naona Mtoto wangu yuko kama kachanganyikiwa
Nikamuuliza tena mama kulikoni aseme hivyo?
Ndiyo akaanza kunisimulia yaliyojiri..

Akaniambia ile jumatatu usiku kama saa sita hivi,
Wakiwa wamelala walisikia honi zikipigwa sana getini kwao,
Basi wakawa wameamka kuangalia ni nani huyo anapiga honi
tena zile za kiusumbufu kabisa, basi walipofungua geti dogo kuangalia
Ni gari ya Vanessa,
Mzee alivyoitambua alifungua geti wakati ule,
akaingia akashuka, mama aligundua kuwa Mtoto wake hakuwa sawa kabisa.
Sasa wakati Wanajaribu kumuuliza kulikoni usiku wote huu,
V alianguka kitu kilicholeta mshtuko mkubwa kwao
kwani alikuwa hajawaambia chochote kile,
Mzee alimwambia kijana wake awashe Gari waende Hospitali
Vane alianguka lakini hakuzimia na alikuwa anawatizama tu,
Wakaamua kwenda Hospital, wakati huo huo mama akawa anampigia simu
Mume wake lakini hakumpata hewani.

Ndiyo akakumbuka kuwa hakuwepo Tanzania, wakati anasafiri aliwaaga wote.
Mama akapata wazo la kumpigia simu dada wa dukani, ikapokelewa akamuuliza Vane
Katoka hapo nyumbani anatatizo gani?
yule dada akamjibu mbona kaondoka mapema na ametuaga kuwa anakuja kwako.
Mama akamuuliza alikuwa mzima? dada akamwambia ndiyo tena ndiyo alikuwa ametoka Dubai,
akatuambia anakuja kwako kuna vitu anawaletea, halafu atakuwa na mazungumzo na wewe, hivyo hatarudi
hapa nyumbani leo. Binti akauliza kuna nini mama? au amepata ajali?
Mama akamwambia nitawajulisha kesho.
Wakawa wamefika kwenye kazahanati kamoja hivi kapo pale Mbezi,
Ila yule daktari wa zamu akawashauri wampeleke Muhimbili
Baada ya kugundua sehemu ya kichwa chake imevimba,

Inabidi afanyiwe vipimo vikubwa,
Wakafika muhimbili ila kuna daktari mmoja akawaambia hana
shida so ikabidi wasubirie pakuche ndiyo afanyiwe vipimo, ila walimwekea drip kwa lengo la
kumwongezea nguvu,
ilionekana kaishiwa nguvu kabisa.
Hapo ilikuwa inaenda kwenye saa tisa.
Ile drip ilimsaidia sana Vanessa na aliweza hata kumsalimia mama yake ile asubuhi
Pale hospitalini.

Akaendelea na Matibabu na kwa bahati nzuri alirecover vizuri,
Mama yake alikuwa anamwacha awe vizuri ndiyo amsimulie, wakati huo
mume wake alikuwa kashafika tena hadi hospital kwani,
mzee asubuhi alipita nyumbani kwake kuwapa taarifa juu ya bosi wao kulazwa
hospitalini.
Hapo V alikuwa kashamwomba sana mama yake kuwa mume wake akifika
amwmbie kuwa ni malaria tu! na hata madaktari waliombwa sana na V waseme ni malaria, ule uvimbe pale kichwani asingeushtukia mapema na ilibidi avae kilemba,
wakati mume wake anafika pale hospitalini jumatano asubuhi kila kitu kilikuwa kimesetiwa.

Mama anaendelea kunisimulia....(ngoja ni post kwanza) nitaendelea na clip ya mwisho.
 
Mimi huwa napotea kabisa halafu narudi baadayeee...hapo naisoma stori yote na ndio huwa inanoga


Bora aise maana hii ya kusubiri ni issue unasubiri na haiji bora nipotee kabisa mkuu watu8
 
Last edited by a moderator:
:::::::::::::::::::kama vp tumsusieeee....!!!!
 
Bora aise maana hii ya kusubiri ni issue unasubiri na haiji bora nipotee kabisa mkuu watu8

Naam kaka...naona jamaa anakuwa anishia kwenye zile sehemu muhimu utadhani Dr Isaac Maro wa Njia Panda
 
Heheh!!! basi shem utakuwa umezoea sana kuangalia muvi a kina Van Damme ambao wao ni kutoa kichapo mwanzo mwisho...

shem mimi naangalia comedy tu. nicheke nijiongezee siku zakuishi.
 
Enhee endelea mkuu....halaf dizain matha keshapewa mchongo mzima na V.
 
Basi ile jumatano hali yake iliendelea kuimarika
Na alhamisi asubuhi aliruhusiwa kutoka hospitalini
Ila mama alimwomba mume wake V aende nyumbani kwake kwa ile siku moja,
yaani akae pale ile alhamisi afu ijumaa kama atakuwa vizuri zaidi
ndiyo arudi kwa mume wake,
Mume hakuwa mbishi aliruhusu

so Vane ndiyo akapata muda wakumsimulia mama yake
akamwambia kuhusu mimi akamwadisia historia yangu mimi na yeye,
Tena mama akaniambia kumbe hata ile kazi ya UNHCR aliiacha kwa ajili yangu.
V alimsimulia mama yake mambo kibao, lakini naona hakumwambia juu ya kutaka kuzaa na mimi,
Na hakumwambia kama mimi ndiyo nilimpiga, alimwambia alienda kupunguza mawazo na wine
akalewa akaanguka ndiyo akapata yale maumivu ya kichwa,
kitu kilichomfanya mama yake aone kama ndiyo amechanganyikiwa,
kwani katika maisha yake yote V hajawahi kutumia Vileo..

Na hakutaka tena kurudi kwa mume wake, ila mama yake alimsihi sana
Arudi na amwombe sana Mungu huyo Pepo m'baya aliyeingilia ndoa yake ashindwe.
Mama ananiambia kuwa alitumia busara na neno la Mungu kwa kiasi kikubwa sana kumshawishi
mtoto wake arejee kwa mumewe kwani walikuwa hawajakosana na wala hawajagombana.

Baada ya yote hayo sasa Mama akaanza kuniambia lengo la
yeye kunitaka mimi niende pale kwake, sema hakujua kama na mimi nilikusudia kuonana nae.
Nilikuwa mpole, mama akaniambia hivi umeshaokoka?
dah, sikuweza kujibu swali hili..
mama aliniambia kijana wangu Shetani ananguvu sana na usikubali akushinde
hata kidogo
usipomkataa kabisa katika maisha yako hakika atakutumia vibaya sana,
Hasa kuanzisha migogoro mikubwa katika familia zetu,
Mama akaniambia yeye anachokiona ni kuwa V anataka kuachana na Mumewe kisa mimi.
Akaniambia hata kama umeshindwa kunijibu kama umeokoka au lah! ila nadhani
utakuwa unafahamu baadhi ya maneno ya mungu haswa juu ya yale yanayounganishwa na Mungu huko juu
mbinguni hapa duniani atalaaniwa yule atakayeyatenganisha.

Akaniuliza kwani wewe katika maisha yako una mpango gani?
Mbona mpaka sasa hujaoa? unategemea kuoa lini?
Mama alinisihi kwa upole kabisa, akaniambia V anapata sana nafasi ya kukuwaza
wewe kwa sababu hujaoa,
sidhani kama ukioa anaweza kukufikiria kama anavyofanya sasa.
Mwanangu mimi Ni mama na Naweza kuelewa hisia za mtu mapema sana.
Akaniomba sana niheshimu ndoa ya mtoto wake, alihisi kuwa nilikuwa na mawasiliano na V.
Mama akanisihi sana Niwe na Mke!! na itakuwa mwarobaini wa V kutulia katika ndoa yake..
nilishindwa kumwambia kuwa sina mpango wa kuoa. kwa sababu nilikuwa nimeshasomewa vifungu kibao vya biblia.

Alinihubiria mengi sana sana..
nimeondoka pale saa kumi na mbili kasoro,
Mawazo ya mama V yalikuwa yanakita sana akilini, na nilisema sitakunywa pombe kabisa ile siku
lakini ilifika saa mbili usiku uzalendo ulinishinda, nilitembea kwa miguu hadi kwenye kabaa kamoja kapo pale korogwe kanaitwa Marangu Inn, nilijikuta nakunywa pombe mpaka kama saa 6 iviusiku.
akili ikiwa mbwii na baada yapo hata sikumbuki ni nani aliyenileta home kwangu!!

nilizinduka saa 1:20 asubuhi nilikuwa na tiketi ya Kilimanjaro basi la saa kumi na mbili.
ila sikutaka kabisa kuahirisha safari yangu nilioga, ila bado nilikuwa na hangover..
sikujali kiume nikaingia road nikachukua boda boda hadi ubungo.
Nikatimba kwenye ofisi za kilimanjaro express nikawaambia basi limeniacha
nilijidai kumind pale ili wanirekebishie, sema jana hata abiria hawakuwa wengi sana wakawa wamenifaulisha kwenye gari ya saa mbili na nusu.

Nikaja zangu huku niliko.
Bado natakafakari kwa kina sana maneno ya Mama Vanie..
Wadau sina hisia za kuoa kabisa!! na ninajiuliza sana je, hata nikioa inaweza kuwa suluhisho?
Kinachosumbua hapa ni Back memories zitafutikaje?

Ushauri wenu tafadhali..
Tyta, watu8, Mr Rocky, miss chagga 'Valentina', Heaven on Earth Mentor.. na wengine wote.....ushauri wenu tafadhalini
 
Back
Top Bottom