Tembosa!! Bado nina Shida kubwa..Niamue nini?

Tembosa

Tembosa

JF-Expert Member
2,984
2,000
Wana MMU,

hasa wale wanaofuatilia hili jambo langu
Kwa ukaribu, niendelee kuwashukuru sana kwa
Ushauri ambao mmeendelea kunipa,

Wengine mlinishauri moja kwa moja na wengine
Mlidiriki kuja hadi PM kuonyesha kuguswa kwenu
Na mambo yanayoendelea katika maisha yangu,
na asanteni sana
Kwani mliniambia kuwa nimo kwenye maombi yenu.
Pia naomba kwa wale ambao mlishauri na sikuweza kufuata ushauri wenu
Msiache kendelea kunishauri, ninawaomba..

Kama nilivyowaahidi kuwa Jumapili nilipanga kwenda kuonana na
Mama Vane ili anisaidie katika ushauri na niliamua kuuvaa moyo wa ujasiri
Kweli kweli kwani hili halikuwa jambo dogo kwangu.
Sasa ile jumamosi nilifikiria sana ningewezaje kuonana na

Huyu mama kwani sikuwa na mawasiliano naye.
Nilifikia maamuzi niende kusali kanisa la nyumbani pale mtaa wa Neema
kwani na wao husalia hapo na mimi niliwahi kusali sana hapo kipindi sijaanza kujitegemea,
nikiamini ningeweza kukutana na Mama V kwa urahisi,
sema rohoni nilipata shida sana kuwa nitamwanzaje na isitoshe lazima angekuwa na mume wake pale kanisani.

Nilipiga moyo konde na kujipa ujasiri kuwa I have to do this,
kama nilivyowaambia mwanzo,
ni lazima nitafute suluhu ya hili walau basi na mimi niishi kwa amani hata kama siyo kwa furaha,
nikiwa na amani at least ingesaidia na ningeweza kufanya mambo mengine ya kimaisha.
Basi nikampigia simu
Yule cousin wangu (niliyekuwa naishi naye pale home kipindi kile),
hope Tyta na watu8 mnamkumbuka.

Nikamweleza kuwa kesho(jumapili) nitakuja kusali Neema ibada ya kwanza
ambayo huwa inaingia saa moja asubuhi.
Akaniambia hamna shida na nikaribie,
sikumweleza kabisa dhamira yangu ya kwenda kusalia pale hiyo jumapili,
kwani tokea nihame sijawahi kabisa kufanya hivyo.

Jumapili asubuhi ikafika na nilijitahidi sana kuwahi kuamka ili niwahi Mbezi,
sikuwa na Gari so ilinilazimu
Nikapande daladala,
na nilifanya kila kitu kwa wakati,
Nilifanikiwa kufika maeneo ya kanisa na ibada ilikuwa bado haijaanza
Sasa nikawa nasalimiana na baadhi ya waumini pale,
ambao nilikuwa nawafahamu
Hapo bado sijawa stable kabisa,
sijui ujasiri wangu uliishia wapi,
nikajiona kama mtoto kidogo niahirishe lile kusudio langu,

Wakati naendelea kusalimiana na wale waumini ambao walikuwa hawajaingia kanisani gafla nilisikia mtu akiniita, nilishtuka sana alikuwa Mama yake Vanie,
alikuwa yupo na kijana mmoja mdogo na kasichana kengine kadogo dogo tu!
Nikamsogelea nakumsalimia,
akaniuliza habari za siku nyingi?
Nikamwambia ni nzuri tu!
Mama huku anatoa sadaka kuwapa wale watoto akamwambia
Yule wakiume akamtafutie Bahasha yake.
Wakaenda,
mimi bado nimesimama pale

Enhee kijana bado unafanya kazi kule Temeke?
Nikamwambia ndiyo mama,
Ahaa! Akaniuliza unahabari kuwa Vanessa alikuwa amelazwa hospitalini?
Nilishtuka kidogo,
kalazwa!!

Akaniambia ndiyo alilazwa kama siku 3 hivi pale Muhimbili,
nikauliza tatizo ni nini?
Kabla hajanijibu akaniuliza kwani baada ya ibada unashughuli gani?
Nikamwambia nilipanga kwenda kuwasalimia wazee wangu,
akaniuliza kwa hiyo leo utashinda Mbezi au?
Nikamwambia ndiyo nimepanga kufanya,
akaniambia kabla hujaondoka naomba upite pale nyumbani tuongee kidogo..

Muda wa ibada ulikaribia kabisa ilibidi tuanze kuingia kanisani,
nikamwambia mama Vanessa nitaenda kwake mchana.
Hapa tayari akili ilianza kunikaa vizuri kwani nilijua Huyu Mama kuna kitu kashaambiwa na mtoto wake….
 
Last edited by a moderator:
Joseph

Joseph

JF-Expert Member
3,522
1,225
Haiwezekani unataka ushauri halafu humalizi habari yako,kulikuwa na haja gai ya kuandika nusu wakati uwezo wa kutoa habari kamili unao?
 
Heaven on Earth

Heaven on Earth

JF-Expert Member
37,163
2,000
haya ngoja nisubiri clip ya 2
 
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
53,137
2,000
shem nitahitaji historia fupi ya hii topic
Duuuh!!! shem mtihani huo maana stori ni ndefu...

Jamaa alipendana na msichana anaitwa Vannesa, inaonesha walipendana kweli kwani mapenzi yao walianza ile kama kaka na dada...

Jamaa alivuka vikwazo vingi ikiwemo mikwara toka kwa kakaze Vannesa, pamoja na hayo kuna siku jamaa alipigana na kaka yake Vannesa baada ya kushindwa kuvumilia kumuona Vannesa wake anaadabishwa na kakaye...

Siku hiyo baada ya Vannesa kudundwa na kakaye, mtoto wa kike alitaka kujichoma kisu na aliyemuokoa Vannesa asijichome kisu ni mpwa wa huyu Tembosa...

Stori ikaenda weeee, hadi ambapo Vanessa alikuwa anahitaji kuolewa lakini bwana Tembosa hakuwa kajipanga kuwa mume mtajiwa...

Hata Vannesa alipompa last chance, Tembosa aligoma kabisa na kutoa go-ahead kwa Vannesa kuolewa na kidume mwingine tu...

Mtoto Vannesa hatimaye akaolewa na mtu mwingine na kitendo hicho kikaukwaa moyo wa Tembosa hadi kudiriki kutokupenda tena maishani pia akawachukia sana wanawake tokea wakati huo...Kuna mahali anakiri kuwa mpenzi wake mkubwa kwa sasa ni gambe...(mambo ya nani kamwaga ulabu wangu, nauliza hahaha)...

Stori ikaendaaaa weeee, Vannesa kuna wakati akawa anaenda Dubai kibiashara na akampa mwaliko bwana Tembosa, laini Tembosa akachomoa...

Baadaye Vannesa akarejea kutoka Dubai, lakini akiwa na habari nzuri ya ujauzito na mzigo huo bibiye Vannesa alidai ni wa Tembosa (kuna wakati hawa watu walidinyana...)...

Hiyo siku Vannesa aliyotoka Dubai, Tembosa alimpokea bibiye pale Mbezi Mwisho kituo kipya na wakaenda zao Kibaha kwenda kupeana michapo ya ujauzito wa Vannesa...hapo Vannesa kumbe ana lake jambo, ameshajiandaa kimwili na akili kwenda kutoa tunda kwa Tembosa

Shem, kufika Kibaha mida ya usiku usiku wakati wanajiandaa kula tunda la mzeituni, bwana Tembosa si akashangaa kukuta Vannesa kafunga kigodoro tumboni...kumbe Vannesa hakuwa ujauzito wala nini ilikuwa ni tego tu mtoto wa kike badala ya maji aseme mmaaa...

Tembosa kuona hivyo akili ikamtoka, akampa kichapo Vannesa hadi mtoto wa kike akazimia ila baadaye akazinduka. Baada ya kuzinduka Tembosa akamkokota bibiye hadi kwenye gari halafu huyoooo akakanyaga mafuta kurudi Mbezi.

Kufika Mbezi akamwacha solemba bibiye Vannesa, yeye akaenda zake kwa mshikaji wake kubonyea kwa usiku huo hata siku zilizofuata...

Sasa baada ya siku hiyo Tembosa ndio kachanganyikiwa, anataka kwenda kumsemea Vannesa kwa mama yake...eti Vannesa kazidi kumganda kama kimavi cha mapera wakati ni mke wa mtu!!!

Sasa endelea na stori...
 
Husninyo

Husninyo

JF-Expert Member
23,777
2,000
Duuuh!!! shem mtihani huo maana stori ni ndefu...

Jamaa alipendana na msichana anaitwa Vannesa, inaonesha walipendana kweli kwani mapenzi yao walianza ile kama kaka na dada...

Jamaa alivuka vikwazo vingi ikiwemo mikwara toka kwa kakaze Vannesa, pamoja na hayo kuna siku jamaa alipigana na kaka yake Vannesa baada ya kushindwa kuvumilia kumuona Vannesa wake anaadabishwa na kakaye...

Siku hiyo baada ya Vannesa kudundwa na kakaye, mtoto wa kike alitaka kujichoma kisu na aliyemuokoa Vannesa asijichome kisu ni mpwa wa huyu Tembosa...

Stori ikaenda weeee, hadi ambapo Vanessa alikuwa anahitaji kuolewa lakini bwana Tembosa hakuwa kajipanga kuwa mume mtajiwa...

Hata Vannesa alipompa last chance, Tembosa aligoma kabisa na kutoa go-ahead kwa Vannesa kuolewa na kidume mwingine tu...

Mtoto Vannesa hatimaye akaolewa na mtu mwingine na kitendo hicho kikaukwaa moyo wa Tembosa hadi kudiriki kutokupenda tena maishani pia akawachukia sana wanawake tokea wakati huo...Kuna mahali anakiri kuwa mpenzi wake mkubwa kwa sasa ni gambe...(mambo ya nani kamwaga ulabu wangu, nauliza hahaha)...

Stori ikaendaaaa weeee, Vannesa kuna wakati akawa anaenda Dubai kibiashara na akampa mwaliko bwana Tembosa, laini Tembosa akachomoa...

Baadaye Vannesa akarejea kutoka Dubai, lakini akiwa na habari nzuri ya ujauzito na mzigo huo bibiye Vannesa alidai ni wa Tembosa (kuna wakati hawa watu walidinyana...)...

Hiyo siku Vannesa aliyotoka Dubai, Tembosa alimpokea bibiye pale Mbezi Mwisho kituo kipya na wakaenda zao Kibaha kwenda kupeana michapo ya ujauzito wa Vannesa...

Shem, kufika Kibaha mida ya usiku usiku wakati wanajiandaa kula tunda la mzeituni, bwana Tembosa si akashangaa kukuta Vannesa kafunga kigodoro tumboni...kumbe Vannesa hakuwa ujauzito wala nini ilikuwa ni tego tu mtoto wa kike badala ya maji aseme mmaaa...

Tembosa kuona hivyo akili ikamtoka, akampa kichapo Vannesa hadi mtoto wa kike akazimia ila baadaye akazinduka. Baada ya kuzinduka Tembosa akamkokota bibiye hadi kwenye gari halafu huyoooo akakanyaga mafuta kurudi Mbezi.

Kufika Mbezi akamwacha solemba bibiye Vannesa, yeye akaenda zake kwa mshikaji wake kubonyea kwa usiku huo hata siku zilizofuata...

Sasa baada ya siku hiyo Tembosa ndio kachanganyikiwa, anataka kwenda kumsemea Vannesa kwa mama yake...eti Vannesa kazidi kumganda kama kimavi cha mapera!!!

Sasa endelea na stori...
shem ahsante sana. hii story ni ya kweli au ni kama ndoto za Mentor?
 
Last edited by a moderator:
M

Mr Rocky

JF-Expert Member
15,195
2,000
watu8 kashapotea na hao akina ram na Heaven on Earth wanaosubiri watasubiri sana na leo lazima wang'atwe na mbu kusubiri
 
Last edited by a moderator:
Husninyo

Husninyo

JF-Expert Member
23,777
2,000
Shem stori ni stori tu (mbona za kihindi huwa tunadanganywa lakini muvi mpya ikitoka tunayooo), mtunzi anasema ni ya kweli...
mimi za kihindi huwa siangalii shem. wale majamaa wanapenda sana kulia lia.
 
M

Mr Rocky

JF-Expert Member
15,195
2,000
Hahah...kaka nimetokezea huku kwa kuwa shem wangu hapo juu kaniita.

Hii movie ya kihindi sijui mhusika atakufa au ataangukiwa na ukuta
Tunasubiri hapa watu8 tupate muendelezo
 
Last edited by a moderator:

Forum statistics

Threads
1,424,523

Messages
35,065,865

Members
538,009
Top Bottom